adakiss23
JF-Expert Member
- Jan 23, 2011
- 4,477
- 4,270
Kuna video imesambaa mtandaoni ikimuonyesha Masanja Mkandamizaji na vijana wengine nadhani ni wafuasi wake katika kanisa lake lile liko pale Leaders club. Clip inaonyesha wako ktk shule fulani nmeshindwa kujua ni shule gani exactly lakini kwa mazingira inaweza kuwa Arusha, anaonekana Masanja anaomba na watoto wanaanguka kimapepo.
Hii kitu sio sahihi kabisa kwa mazingira ya eneo la elimu na pia kwa mazingira ya watoto wadogo. Sijui uongozi wa shule waliweka wapi akili na fikra zao kuruhusu hili.
Binafsi nmeona ni jambo lisilo na mantiki kabisa. Sioni kabisa logic ya hii kitu kabisa. Inaweza kuleta madhara ya kisaikolojia hapo baadae kwa wanafunzi na hata shule husika pia.
Tunajua jinsi baadhi ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu kutumia nguvu tofauti tofauti kujifanya wanakemea mapepo na watu wakianguka ovyo, huwa sijui lengo hasa ni lipi lakii kwa watu wazima wenye akili timamu ambayo hawajapelekwa pale kwa bakora, walienda kwa matakwa yao ni sawa.
Lakini kwa watoto wadogo kama wale hakika sio jambo sahihi kabisa. Unless hiyo shule iwe na shida fulani inayohitaji maombi kama yaliyofanywa na Masanja na watu wake.
Lakini kwa uchunguzi kidogo nimebaini ni kama tour huyu Masanja anafanya katika mashule kufanya anachokifanya. Hapa namaanisha kuzunguka katika mashule na kuombea na watoto kuanguka ovyo. Nadhani si sahihi na shule sio eneo sahihi kwa haya anayofanya Masanja.
Naona ni busara kwa wenye mamlaka kuzuia hii kitu kufanyika katika mashule.