Hii yaweza kuwa sababu ya CHADEMA kumkubali Lowassa

Ungemueleza ukweli mkuu.
kwamba aliyekuwezasha kupata fedha za kununulia hayo mazaga ni ccm hiyo hiyo wanayoinanga!

Mimi sijawahi kupewa hela na CCM mkuu. Km unapewa ni wewe sio mimi. Wala sina haja ya kujikomba kwa haya majizi ya CCM na vibaraka wao
 
Katika karne hii ya soko huria na ujasiliamali tunaweza kudefine au kuiweka siasa kama njia mojawapo ya kiuchumi ama ujasiriamali.

Siasa ya sasa ni sehemu ya watu kujiajiri au kuinvest!

Siasa ni fursa ya kuneemesha mtu mmoja mmoja au kundi flani la wafuasi wa kisiasa.

Siasa ya sasa sio ile ya kina baba wa Taifa ikiyofocus katika kuhudumia wananchi na kuishi principles flani flani.

Siasa ya leo haifocus kwenye kukamata dola na kuishi kwa prestige pekee.

Utangulizi huo utanipeleka katika hoja yangu ya msingi.

kuna tuhuma zilizowahi kutolewa kwa chadema kuonekana kama saccoss badala ya chama cha siasa.

Tuhuma hizi zaweza kuwa kweli kwani kwa muelekeo wa siasa za mbowe ni wazi alitaka kukifanya chadema kuwa brand flani hivi ya kuingiza fedha.

wakati tunaingia na mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 tulishuhudia kuzuka kwa mavazi au vito mbalimbali vyenye rangi za au alama za chadema kama vile Tshirt,kofia,skafu,magwanda na vinginevyo vya aina hiyo.

products hizi zilikuwa haziko rasmi kama mali ya chama bali kila mbinifu ndani ya chadema hasa maeneo ya Arusha na Moshi alitoka kivyake.

Jambo hili liliendelea katika harakati zote za chadema mikoani.

Na katika mwaka huu wafanyabiashara wadogowadogo hasa hasa jijini Arusha walijiandaa vyema kwa kuandaa mavazi na vito mbalimbali ambavyo walitarajia kuviuza kwenye mikutano ya kisiasa hasa hasa ile ya chadema.

Nimetembelea madocs(viduka vya nguo) mbalimbali na kujionea Tshirt,kofia,magwanda,masweta na skafu zikiwa zimetundikwa sambamba na zile nguo za kichina.

Namuona mbowe kama mjasiliamali mjanja kwani ameona kuna soko kubwa la kuuza mavazi na vito mbalimbali kwa kumerge brand ya chadema na ile ya Team lowassa.

hapa tunajionea sticker za magari na vito vinginevyo vikianza kuuzwa mjini.

Huu ni ujasiliamali wa hali ya juu sana na inafaa tumpongeze kwa hilo.

Kimsingi Chadema chini ya mbowe kimeamua kusimama katika misingi ya soko huria.

Kwa ufupi chadema haikujiaandaa au kuwa serios kushika dola bali imejikita katika kuwafaidisha wajasiliamali wadogo na wakati.

Hivyo watanzania wasione shida katika kuamua ni chama kipi kitasimamia siasa classical vs siasa za soko huria!!

Chadema iko gulioni wakati ccm imejikita katika siasa za kuwalinda wajasiliamali,wakulima,wafugaji,wavuvi na wafanyakazi.

HII NI TAFAKARI YA jingalao

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!

Sasa tatizo kwako nini? Wewe si chama cha siasa mliojiandaa kushika dola achaneni Na hao wajinga saccos! Kipi kinakusukuma wewe hadi uandike makala yote hii? Saccos Na chama chenu cha siasa wapi Na wapi? Mnaonesha jinsi msivyojiamni mna mchecheto unawasumbua!
 
Nimesoma ujumbe wako mpaka mwishooo nikashawishika kukurudi juu nilisome jina lako nikakuta unaitwa JINGALAO, ha! Ha! ha nakweli umeandika ujinga mtupuuu

Rejea msemo wa wa "KIZURI CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA" Halafu usubirie kofia na T-shirt za bure kutoka kwa CCM, Huku za CHADEMA zikiuzwa na bado watu wanazinunua
 
Mimi sijawahi kupewa hela na CCM mkuu. Km unapewa ni wewe sio mimi. Wala sina haja ya kujikomba kwa haya majizi ya CCM na vibaraka wao
Umrpataje hela kama sio mfumo mzuri unaosimamiwa na ccm?

Kama unaingiza kipato cha kunua blueband na mazaga mengine na hata kuwa na fadha za kuweka bundle kwa nini usikubali kuna mfumo uliokuwezesha?

Inaelekea ulichokuwa unakipata hukushare na wazazi wako ndio maana wanailaumu ccm badala ya kukulaumu.

wewe umeifanyia nini serikali ya ccm ili uanze kutamba kwamba haijawaletea maendeleo wazazi wako?

EL unatemtetea amewaleta nini wazazi walioko monduli??ambao nao watakuwa wanailaumu ccm?

Tafakari!
 
Mimi simtetei EL mkuu. Magufuli unayemtetea ameleta nini Chato? Mbona mnahangaika sn na EL? Kwani wagombea wengine wa Urais km akina Mtikila, Fahmu Dovutwa n.k hakuwaona? Ni EL ndiye anawatia kiwewe nini mkuu?
 
Nimesoma ujumbe wako mpaka mwishooo nikashawishika kukurudi juu nilisome jina lako nikakuta unaitwa JINGALAO, ha! Ha! ha nakweli umeandika ujinga mtupuuu

Rejea msemo wa wa "KIZURI CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA" Halafu usubirie kofia na T-shirt za bure kutoka kwa CCM, Huku za CHADEMA zikiuzwa na bado watu wanazinunua

Umesema vizuri mkuu.Ccm watengeneze sare nzuri na kuanza kuziuza!

Ila linapokuja suala la kuchagua kiongozi ni tofauti sana na kutafuta mrembo wa Tanzania au bidhaa bora nchini.

Chadema ijigeuze kuwa kikundi cha wajasiliamali na wafanyabiashara kwa kuwa kuongoza nchi ni zaidi ya hapo!
 
Mimi simtetei EL mkuu. Magufuli unayemtetea ameleta nini Chato? Mbona mnahangaika sn na EL? Kwani wagombea wengine wa Urais km akina Mtikila, Fahmu Dovutwa n.k hakuwaona? Ni EL ndiye anawatia kiwewe nini mkuu?

Leo tuko kibiashara zaidi!hayo unayoyataka yatajibiwa na yalishajibiwa.

Naona mko katika kutangaza biashara na sio mgombea urais.

Hata diamond angejiunga chadema kwa sharti la kuutaka urais mngempa!
 
Leo tuko kibiashara zaidi!hayo unayoyataka yatajibiwa na yalishajibiwa.

Naona mko katika kutangaza biashara na sio mgombea urais.

Hata diamond angejiunga chadema kwa sharti la kuutaka urais mngempa!

Sisi mgombea wetu hatumtangazi. Yeye anauzika, anajitangaza mwenyewe. Watu waliojitokeza jana ni salamu tosha. Jana watu mlijinyea ndio maana leo mmeamka na propaganda za kipuuzi za kila namna. Bahati nzuri humu JF watu wengi ni welewa. Upuuzi wote tutawajibu. Endeleeni kuandika propaganda humu ndani, ndivyo mnavyotusaidia kufanya kazi ya uenezi na mgombea wetu anapata publicity kubwa. Kibaya chajizetembeza, kizuri chajiuza. EL anajiuza mwenyewe, na ndio maana mnahangaika kujaribu kuzuia. Mambo si shwari hata rafiki zng vigogo ndani ya CCM wamekiri
 
Lowasa ni Kimbunga ccm lazima wakae hawana jinsi japo wapo busy kubuni mbinu za kuiba kura .
 
Hahahaaahahaaa...

Kujua Kwako kusoma na kuandika kweli ni BURE kabisaaa, kwa maana hakukisaidii kwa chochote.!

EL anauzika mbaya, thamani yake ni kubwa sana Mkuu.

Nikuambie tu Mkuu, EL tayari ni raisi.. Tunachokifanya ni kufuata utaratibu uliowekwa step by step, Kama sio kufuata utaratibu angekua ameshaapishwa.
 
Wakuu naomba nieleweke kwa hili.

Juzi ijumaa niliamua kwenda kijijini kuwasalimia wazazi wangu,na nilibeba baadhi ya vyakula kwa ajili yao. Nilipofika na kuwajulia hali,nikamuuliza baba je unaonaje mwenendo wa siasa nchini? Naona bado mnaipenda CCM iliyowalea na kuwaletea maendeleo.

Kwakweli nilisikia sauti ya mwanamke akilia huko jikoni,nikamuuliza baba ni nani analia? Akaniambia naona unataka laana ya mama yako mzazi kutokana na hayo maneno yako. Baba akaniuliza kwa hasira: huo mkate umeununua shillingi ngapi? Nikamwambia 2000/= akaendelea na hiyo blueband,kahawa na maziwa ya Nido na cocoa vimetengenezwa wapi? Nikamwambia Kenya.

Baba akasema inamaana Tanzania hatulimi kahawa? Hatufugi Ng'ombe? Kwanini tutengenezewe vitu na wakenya? Nikakosa jibu, kisha akaniambia sasa kwanini unatutukana sisi wazee wako kuwa tumeletewa maendeleo na CCM? Ni maendeleo yapi hayo? kwanini vijana mnatuona hatuna akili? Nashukuru Wife aliniombea msamaha,ikabidi tuage na kuondoka.

Wazee wetu wanasema kwa sasa ni zamu ya vijana hivyo nao watawaunga mkono vijana ili watimize ndoto zao kwa kuchagua vyama vya kimageuzi! Wengi nilioongea nao wamesema nyumbani kwa sasa wao bado wameendelea kuwa tegemeo la uchumi wa familia hadi kuwatunza vijana wao wa umri mkubwa kwa sababu tuu hawana vyanzo vya kipato!
 
Kwenye content sijaona umemtaja Lowasa kama title yko inavyosema hivyo hujielewi bado una ganzi ya mafuriko ya jana. Umetaja sana t shirt , gwanda na kofia za CDM, ni kweli zinauzwa kwa bei ghari na zinanunulika sana tena sana. Una akili gani ya kutokutambua sababu ya mtanzania kuvaa nguo ya CCM na kuzomewa mtaani! Hujui kwa nini nguo za ccm haziuzwi sokoni badala yake zinagawiwa bure na bado hazitakiwi! Ganzi ya mafuriko inakudhuru sana, itisha conference ufanye maamuzi magumu.
 
Macho hayaoni kile ubongo usichakifahamu!!
 
Back
Top Bottom