Hii ya watu DSM kukaa kimakabila ni uoga wa maisha au ndio mbinu za kulikabili jiji?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,570
15,319
Sijui kama duniani huko nako kuna huu mtindo.

Yaani imenichukua muda hadi kugundua asilimia karibu 60 ya majirani zangu ni watu kutoka Sumbawanga. Juzi nimejua tena wanaundugu.

Juzi nimepita Mtaa flani karibu na Eneo linaitwa Msingwa. Nashangaa karibu kila mwanamke ni mweupe na kama wanafanana. Kuulizia kumbe wametokea Singida. Na hadi kuna Mtaa unaitwa Singida.

Hapo bado
Wachaga Kimara
Wasukuma Kigamboni ndanindani.
Wakurya Mwanagati, Machimbo, Kitunda

Nimepita Kariakoo nako ni hivyo hivyo.
Kuna kamtaa wanauza tangawizi na vitunguu swaumu pale ni WAPARE mwanzo mwisho.

Kuna Congo kule waha kibao hadi kuna sehemu wanakatisha tiketi za basi la kwenda Kigoma (Sarato).
Kuna kamtaa walikuwepo wa Machinga wa kabila flani hivi wamejaa wao tu kiasi walikuwa wanaiba na kukaba hadi mchana na hakuna wa kujitetea maana wote pale Ndugu. Walikuwa wabakaba hadi wachina bila kujali wanajua taekwando au kung fu. Hii tuhuma niliipata kwa mwenyekiti mmoja wa wamachinga akawa anaandaa statergy ya kuweka Mlinzi pale hao mabwana wasije wakachafua chama chake cha wamachinga.

Sababu ya hii kitu nini?

Comfort zone watu hawataki kutoka nje ya box la kikabila?

Au uoga wa kupambana jeshi la mtu mmoja.
 
Ina maana sisi wakinga, wabena na wahehe...
Hatupo huko mjini? Mbona hujatugawia kaplot.
Hahahaha
Mkuu nyie so ndio nasikia ni matajiri wa Kariakoo. Mnatuajiri sisi tunaokuja kindugundugu
 
Sijui kama duniani huko nako kuna huu mtindo.

Yaani imenichukia Muda hadi kugundua asilimia karibu 60 ya majirani zangu ni watu kutoka Sumbawanga. Juzi nimejua tena wanaundugu.

Juzi nimepita Mtaa flani karibu na Eneo linaitwa Msingwa. Nashangaa karibu kila mwanamke ni mweupe na kama wanafanana. Kuulizia kumbe wametokea Singida. Na hadi kuna Mtaa unaitwa Singida.

Hapo bado
Wachaga Kimara
Wasukuma Kigamboni ndanindani.
Wakurya wanagati,machimbo,kitunda

Nimepita Kariakoo nako ni hivyo hivyo.
Kuna kamtaa wanauza tangawizi na vitunguu Swaumu pale ni WAPARE mwanzo mwisho.

Kuna Congo kule waha kibao hadi kuna sehemu wanakatisha tiketi za basi LA kwenda kigoma (sarato...).
Kuna kamtaa walikuwepo wa Machinga wa Kabla flani hivi wamejaa wao tu kiasi walikuwa wanaiba na kukaba hadi Mchana na hakuna wa kujitetea maana wote pale Ndugu. Hii tuhuma niliipata kwa mwenyekiti mmoja wa wamachinga akawa anaandaa statergy ya kuweka Mlinzi pale hao mabwana wakachafua chama chake.

Sababu ya hii kitu mini?

Comfort zone watu hawataki kutoka nje ya box LA kikabila?

Au uoga wa kupambana jeshi LA mtu mmoja.

Wamakonde, Wandengereko na Wangindo wameifanya Mbagala yote kuwa yao
Warangi inaonekana wanataka Kuuteka Mji wa Kawe kwani ni kama vile Kondoa yote imehamia
Wanyakyusa na Tabata yao
Wazaramo wameshajimilikisha kabisa Chanika
Wahaya na Tegeta Masaiti ni kama vile Kidole na Pete
Wazanaki na maeneo ya Mbweni hadi Mabwepande nadhani wana Jambo lao huko
Wasukuma na Mapori ya Kiluvya wameshaingia Mkataba labda pengine kwa Ulafi ( Umelo ) Wao wanapenda sana kuwa Jirani na Vichaka au Vyoo
 
Njoo buza tupo mixer hasa hapo kwa lulenge
Aisee nilikwenda pale Kiwalani dereva wa Uber alikuwa muoga hatari na mimi ndio mara yangu ya kwanza kufika. Manake tokea naondoka nyumbani naambiwa ikifika usiku huko unakula kelebu na kwara na kuporwa. Ila nilichokiona vigodoro mwanzo mwisho


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom