Hii ya kuuza dola bureau de change kwa kitambulisho imekaaje

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
2,075
2,316
Naombeni kuuliza huu utaratibu wa kuombwa kitambulisho wakati wa kuuza dola bureau de change umekaaje. Bureau de change ni wakala wa Benki Kuu katika kukusanya dola ili ziingie kwenye mzunguko salama wa kibenki. Sasa, inakuwaje mtu anapeleka dola zake kuuza ili apewe shilingi anaombwa kitambusho? Je, kama hana kitambulisho azipeleke wapi.
Kwa mawazo yangu mtu anaponunua dola ndio aombwe kitambulisho ili ijulikane dola hizo zimeuzwa kwa nani.
Wadau mnaojua hili naombeni nieleweshwe.
 
Huo ndo utaratibu sema huwaga hauzingatiwi, nyingne unajaza na fomu kabisa.
 
india hununui rupees zao bila kitambulisho.. hela yoyote ukitaka badilisha unaombwa kitambulisho
 
m pesa mbona tunaonesha vitambulisho

inaonesha jinsi gani system haikua serious

katika utendaji wake
 
Kuna baadhi ya nchi za kusini mwa Africa kama SA, Botswana na Namibia unajaza fomu kabisa na pia unatoa copy ya passport yako nadhani ni utaratibu mzuri tu haswa kuepuka kutakatisha fedha haramu kutoka kwa watu wasiojulikana
 
Back
Top Bottom