Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 776
- 1,330
Binti Akwilina Akwilini amefariki ni mwezi na nusu sasa hatujasikia Askari waliosababisha kifo chake wakichukuliwa hatua wala yeyote yule kuwajibika kutokana na kifo chake kilichosababishwa na uzembe na matumizi mabaya ya vyombo vya dola.
Kikubwa Serikali walichoona wanaweza kuifanyia familia yake ni kugharamia msiba tena kwa 'kuwachoresha' ndugu zake kwenye mitandao(inauma). Kwa ninavyoijua Tanzania ndo imetoka hiyo. Wakihoji sana ni sisi jamii tutakaowaambia " kwani mkilalamika itamrudisha?"
Kwa mara nyingine tena juzi amefariki kijana Allen huko Mbeya na inasemekana kifo chake kina mkono wa wale wale wahusika wa kwa Akwilina ingawa tofauti na wale wa Akwilina ambao walikiri (Rejea: Polisi yakiri kupiga mtu risasi maandamano ya CHADEMA ) kabla ya kuyakana maneno yao, hawa wamekataa katu katu.
Cha kushangaza, Mkuu wa Wilaya William Ntinika ameahidi Serikali itagharamia msiba na kutoa magari ya kusafirisha wafiwa.
Hivi kama Serikali inashindwa kujua hitaji la mfiwa akiwa katika kipindi kigumu, hasa ambaye kifo cha mpendwa wake kimegubikwa na utata na hisia za unyama je itajua nini tunahitaji nini kama Watanzania?
Wafiwa hawa wanachotaka zaidi ya usafiri wa kwenda kuzika na chakula ni 'closure'. Wajue nini hasa kilitokea, nani alisababisha na ameishia wapi. Wanahitaji pole lakini zaidi wanahitaji SAMAHANI! Na si kuwazidishia unyonge na kuwafanya wajihisi hawawezi kuhoji kitu kwa kuwapa vimsaada.
Je, leo mkisababisha kifo cha mtoto wa jirani yetu Baba Furaha ambaye ana pesa za kukodi hata ndege kumsafirisha mwanae kwenda mkoani mtampa vimilioni vyenu mkitegemea 'yaishe'?