HII YA KUFUNGIA Zahanati NI KWA MANUFAA YA NANI? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HII YA KUFUNGIA Zahanati NI KWA MANUFAA YA NANI?

Discussion in 'JF Doctor' started by Papa D, Jun 20, 2011.

 1. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wizara ya Afya imevalia njuga zahanati zisizokidhi viwango na kwa kiasi kikubwa imeathiri zahanati zinazohudumia watu maskini waliochoka haswa!!
  Uttata ni huu!
  Je, hawa watu wanaokagua na kufungia zahanati wanaweza kutoa tiba/hospitali mbadala wakati hizo lizizofungwa zikiwa kwenye maboresho?
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa kuliona hili.Ni kweli zahanati zetu zina matatizo.Lakini swali la kujiuliza ni kwamba ni nani aliyeacha hali i-deteriorate that much.Ni mamlaka hiyo hiyo inayofanya usanii huu wa sasa.And why now.Inashangaza kidogo.Ila nadhani agenda ni ile ile,to create crises ambazo zitatufanya to loose confidence in ourselves,tukose matumaini and therefore easy to rule and manipulate.This is characteristic of the Freemasons.
   
 3. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa wanaenda wilaya chache za mikoa. kama ni ukaguzi kwa nini wasifanye wilaya zoote za mkoa husika?
  1. wameenda mara wamekagua baaadhi tu ya wilaya
  2. wameenda mwanza wamekagua wilaya moja
  3. wameenda shinyanga wamekagua wilaya chache
  4. sasa wapo tabora wamefunga zahanati nyingi za jimbo la six!!
  Swali muhimu:-
  Kipi hatari kati ya madawa bandia yaliyozagaa hadi yale nyeti au hospitali zenye watabibu wenye kujituma na vifaa duni?
  Jamani wana JF hebu tuliangalie hili zaidi ya hapo panapoonyeshwa na hawa wakaguzi!!
   
 4. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,581
  Trophy Points: 280
  Hii imekaa vibaya sana, niliona wagonjwa wanavyohamishwa kutokana na zahanati kufungwa, kwa kweli haijakaa vizuri. Na wanakuwa wapi kungoja kufunga kwani hakuna wakaguzi, na hizo hela wanazotumia kusafiri huku na huko kwa nini zisitumike kuboresha mazingira ya zahanati zetu.
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Mazingira ya hizo zahanati kwa kweli inatisha!lakini tufanyaje kama serikali inashindwa kutoa huduma muhimu
   
 6. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mazingira kweli si mazuri na ni kweli kwa kuangalia viwango ni lazima zifungwe sasa oanisha hali hizi mbili:-
  1. Zahanati au kituo cha afya kipo kimoja na kinahudumia vijiji sita, imefungwa pamoja na zile za jirani yake hivyo kufanya vijiji 18 kukosa huduma ya afya kwa hiyo kutegemea hospitali ya wilaya ambayo haifikiki kirahisi kutokana na ubovu wa barabara au kwamba basi linaloenda huko kijijini ni moja na linaenda mara moja kwa wiki au kwamba vijiji vyote 18 vinategemea mtu mmoja anayemiliki gari aina ya land rover 109. Je, wangapi watasalimika ukilinganisha na wale waliokufa kwa kupata huduma duni katika hospitali zilizofungwa?
  2. Magufuli alitangaza miezi mitatu watu waondoke kwenye hifadhi ya barabara baada ya miezi mitatu alianza kubomoa, akazuiwa kwamba ni ubabe. Hawa jamaa hawajatangaza kama mwenzake na wanaendelea kufunga huku wakiacha ombwe la wananchi kujua watatibiwa wapi pale watakapougua. Je,, hiyo ni kwa manufaa ya nani? Je, kuzuiya ubomoaji wa nyumba zilizo kwenye hifadhi ya barabara ilikuwa ni kwa manufaa ya nani? Je hiyo haikufanyika kwa mujibu wa sheria za nchi? ?

   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  wanatafuta posho, safari nchi nzima unadhani mchezo wakirudi hapa bongo ni ma millionea.
   
Loading...