Hii ya kufumaniwa na my wife wa mtu imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ya kufumaniwa na my wife wa mtu imekaaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mungi, Sep 17, 2011.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Sep 17, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  • September 8, 2011

  [​IMG]

  [​IMG]
  ...Ofisa baada ya kukutwa gesti na mke wa mtu.
  Na Mwandishi Wetu
  OFISA wa Mahakama ya Uhalifu wa Kivita nchini Rwanda (ICTR) iliyopo Arusha, Andrew Alexander Chuwa, amefedheheka baada ya kudaiwa kukutwa na mke wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Tausi ndani ya nyumba ya kulala wageni iliyopo jijini Tanga.

  Habari na picha kutoka chanzo chetu, zinabainisha kuwa ofisa huyo ambaye ni dereva wa ICTR, alipatwa na mkasa huo Septemba 2, mwaka huu kijua cha saa tano asubuhi.
  [​IMG]
  Waraka wa barua pepe uliotumwa chumba cha habari ulieleza kinagaubaga kuwa kunaswa kwa wawili hao kulitokana na harufu ya usaliti kumfikia mume wa mwanamke huyo ambaye jina lake linahifadhiwa.

  MAELEZO KAMILI
  Inadaiwa, Tausi ambaye anaishi Arusha na mumewe, alimuaga mwandani wake kuwa anaenda jijini Tanga kukata kiu ya kuwaona waliomzaa, jambo ambalo wa kufa na kuzikana wake aliliafiki.
  [​IMG]
  Hata hivyo, baada ya kueleza hilo na kupanga safari, wachungulia mambo ya watu ‘walimmegea za kitaa’ mume wa mwanamke huyo kuwa mkewe alikusudia kusafiri na Chuwa kwa lengo la kujinafasi naye.

  “Baada ya kuambiwa hivyo hakulaza damu, akaweka watu wa kumfuatilia mkewe, … kweli siku ya kuondoka aliambatana na yule mwanaume kwenye gari dogo la familia (Tausi) ambalo alisafiria kwenda kwao,” sehemu ya maelezo ilisomeka hivyo.
  [​IMG]
  KIZAZAA TANGA
  Kurasa za maelezo zilidai kuwa baada ya Tausi na Chuwa kuwasili jijini Tanga kwa mbwembwe, walitumia muda mfupi kuwasalimia wazazi kabla kwenda hoteli moja maarufu (jina kapuni) kujipumzisha.

  Kama kawa kama dawa, msemo wa vijana wa leo unavyobainisha, wapambe wa mume wa mwanamke huyo ambao walikuwa wamewezeshwa kufanya ukachero, walifanikiwa kujua chumba alichokodi Chuwa.
  [​IMG]
  “Walipogundua kuwa yule mwanaume alikuwa chumba namba 301 waliwapigia simu askari, wakaja kumkamata pamoja na yule mwanamke na kuwapeleka kituo cha polisi kati,” inaelezwa.

  CHUWA ATUPWA SELO
  Habari zinaeleza kuwa baada ya Chuwa kufikishwa puta kituoni hapo, aliwekwa selo tangu saa 5 asubuhi hadi saa 5 usiku, alipofanikiwa kupewa dhamana ambayo hata hivyo iliwashangaza ndugu wa mume wa Tausi.

  “Kwa kawaida dhamana hutolewa wakati wa kazi, lakini mtuhumiwa wetu alitolewa saa 5 usiku, tulipouliza tukaambiwa na maofisa wa polisi kwamba hakukuwa na kesi, kama si rushwa ni nini?” alihoji Shabani Juma.
  [​IMG]
  TAUSI ALONGA
  Tausi alipotafutwa kwa njia ya simu ya mkononi ili kujua kilichotokea, hakupokea badala yake alijibu ujumbe mfupi wa maneno kwa kusema “nitakupigia”. Hata hivyo hakutekeleza ahadi yake mpaka tunakwenda mtamboni.

  Kwa upande wa Chuwa, hakupatikana kwenye simu huku mume wa mwanamke huyo akieleza kuchanganywa na tukio hilo na kuomba muda wa kutafakari cha kufanya. Duru za kipolisi zimethibitisha tukio hilo.

 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Sep 17, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Dah! Nimeshawishika! Ngoja nifanye mpango kazi fasta!
   
Loading...