Hii ya kubadilisha KM za gari hivi ni kweli ipo? Kuna gari namba BAC ina KM 38900 TOYOTA KLUGER jamaa anaiuza

Mchezo huo upo 100% hapa Tanzania hasa ukinunua kwa mtu asiye mwaminifu/vishoka au madalali, pia kuwa mwangalifu sana unapenda kwenye show room za hapa kwetu mtaani magari mengi yamefanyiwa utundu huo wa kurudisha nyuma Km ili gari ipate sko kwa bei ya faida kubwa.

Kabla ya kununua gari kama hiyo jiridhishe na historia yake toka kwa watu waliokaribu nay , peleleza gereji gani ilikuwa inapelekwa toka kwa watu kama houseboy wa nyumba hiyo, watoto wa nyumbani hapo, majirani na hasa vijana wa mtaani watakupatia details zote muhimu kuhusu mwenendo wa gari husika.

Mwish kabisa take trouble ya kupata document halisi zilizoleta hiyo gari nchini na umjue muuzaji toka huko ilikokuwa then contact him na akiwa na ushirikiano atakupa mre details.
Si utahisiwa ni mwizi kwa kufatilia mambo yote hayo
 
Niliwahi kununua Kluger namba B kutoka kwa mbongo yenye km 56k. Mwanzoni niliamini amechezea ODO lakini baadaye nilijiridhisha kwa kuona kadi za service kwani zote alizitunza kwa kuzipachika kwenye switch ya wiper. Kwa hiyo gari namba B zenye kilometer chache zipo kweli cha msingi ni kujiridhisha kama ni kweli hizo km ni za halali.
Ulipigwa na Yeye alipigwa
 
Upo uzi fulani unatangaza magari hapa JF, gari zote hazina km 100,000.
 
Aliuziwa na Mbongo ambaye anaishi japan na anafanya biashara ya kuuza vitu used kama anavyofanya Chris Lukosi ,ila inaonekana na yeye aliiununua tradecarview na kumuuzia jamaa yangu.....km za trade carview ni zaidi ya laki ila alivyotumiwa B/L na mbongo km zilikuwa chini ya elfu 50...Tulivyofanya comparison tukagundua ile digit ya mwanzoni ndio aliondoa(kupunguza) zile nyingine zilibaki vilevile.

Gari za Japan nunua yenye km zaidi ya laki maana itakuwa imefanyiwa service nzuri.
Chief wewe ni fundi gari..

Maelezo haya nimeona kwenye mtandao wa kijamii, yanafanana asilimia 100 hadi hicho kisa cha jamaa yako ni 100%
 
Nimepata mashaka makubwa sana baada ya kutizama hizo kilometre na usajili wa gari yaani gari imesajiliwa muda mrefu lakin imetembea km chache sana nika muuliza kulikoni gari inausajili wa BAC wa muda mrefu lakini gari imetembea km chache kiasi hiki? Akanijibu tangu imenunuliwa ilikuwa haitumiki sana.

Lakini nikaingia mashaka baada ya kuikagua gari kifupi bodi bado ina muonekano mzuri lakin nikakagua vitu vichache kama Excelerator pedal na breack, kidogo vimechakaa kwamba vimetumika sana pia vitu vidogo vidogo vingine vinaonesha kama gari imetumika sasa hapo nimebaki njia panda.

Sasa naomba wajuzi wa hizi mambo wanisaidie maana kuna mtu akanambia hiyo gari watakuwa wamechezea ODO wamerudisha nyuma KM kwa namna fulan sikupingana na ushauri wake hasa kwa mazingira hayo, hebu mnisaidie inawezekana kufanya mchezo huo kweli?
Achana na hiyo gari tafuta pesa uagize yakwako...... Watu wana mambo ya kishenzi sana. Siajabu hata engine itakuwa haipo sawa.
 
Kwa total mileage ya 38,000 kms gari hiyo ni mpya kabisa..... Sasa ndio mtu akuuzie mkononi kwa bei ya kawaida?!
 
Hii hatari sana sasa wapi kuna usalama maana YARD nako nasikia ujanja ujanja tu , mkononi nako ujanja ujanja tu labda sasa niagize mwenyewe japan
Sio yard zote. Kuna yards zinareputation nzuri. Wanaingiza gari mpya kila baada ya miezi michache. Hawa kukubambikia ni ngumu.

Ila hizi yard za wadau wanaojaribu biashara ndio kuna upuuzi mwingi.
 
Zinashushwa hizo tena dakika chache tu.. mara nyingi wanacheza na namba za mwanzo! hiyo lazima ilikua 138900 au pengine hata 238900
 
Back
Top Bottom