Hii ya kubadilisha KM za gari hivi ni kweli ipo? Kuna gari namba BAC ina KM 38900 TOYOTA KLUGER jamaa anaiuza

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
3,360
5,802
Nimepata mashaka makubwa sana baada ya kutizama hizo kilometre na usajili wa gari yaani gari imesajiliwa muda mrefu lakin imetembea km chache sana nika muuliza kulikoni gari inausajili wa BAC wa muda mrefu lakini gari imetembea km chache kiasi hiki? Akanijibu tangu imenunuliwa ilikuwa haitumiki sana.

Lakini nikaingia mashaka baada ya kuikagua gari kifupi bodi bado ina muonekano mzuri lakin nikakagua vitu vichache kama Excelerator pedal na breack, kidogo vimechakaa kwamba vimetumika sana pia vitu vidogo vidogo vingine vinaonesha kama gari imetumika sasa hapo nimebaki njia panda.

Sasa naomba wajuzi wa hizi mambo wanisaidie maana kuna mtu akanambia hiyo gari watakuwa wamechezea ODO wamerudisha nyuma KM kwa namna fulan sikupingana na ushauri wake hasa kwa mazingira hayo, hebu mnisaidie inawezekana kufanya mchezo huo kweli?
 
Mchezo huo upo 100% hapa Tanzania hasa ukinunua kwa mtu asiye mwaminifu/vishoka au madalali, pia kuwa mwangalifu sana unapenda kwenye show room za hapa kwetu mtaani magari mengi yamefanyiwa utundu huo wa kurudisha nyuma Km ili gari ipate sko kwa bei ya faida kubwa.

Kabla ya kununua gari kama hiyo jiridhishe na historia yake toka kwa watu waliokaribu nay , peleleza gereji gani ilikuwa inapelekwa toka kwa watu kama houseboy wa nyumba hiyo, watoto wa nyumbani hapo, majirani na hasa vijana wa mtaani watakupatia details zote muhimu kuhusu mwenendo wa gari husika.

Mwish kabisa take trouble ya kupata document halisi zilizoleta hiyo gari nchini na umjue muuzaji toka huko ilikokuwa then contact him na akiwa na ushirikiano atakupa mre details.
 
Mchezo huo upo 100% hapa Tz hasa ukinunua kwa mtu asiye mwaminifu/vishoka au madalali, pia kuwa mwangalifu sana unapenda kwenye show room za hapa kwetu mtaani magari mengi yamefanyiwa utundu huo wa kurudisha nyuma Km ili gari ipate sko kwa bei ya faida kubwa,
..
Shukran kwa ushauri
 
9
Washa usikie injini ina semaje au ukipata fundi anaye jua gari tena hakikisha hupo naye karibu na unamjua maana kuna watu wanatabia ukipeleka fundi wanampa chake kukuthibitishia kuwa gari aina tatizo
Asante kwa ushauri
 
Nimepata mashaka makubwa sana baada ya kutizama hizo kilometre na usajili wa gari yaan gari imesajiliwa mda mrefu lakin imetembea km chache sana nika muuliza kulikoni gari inausajili wa BAC wa muda mrefu lakini gari imetembea km chache kiasi hiki ? Akanijibu tangu imenunuliwa ilikuwa haitumiki sn

Lakini nikaingia mashaka baada ya kuikagua gari kifupi bodi bado ina muonekano mzuri lakin nikakagua vitu vichache kama Excelerator pedal na breack, kidogo vimechakaa kwamba vimetumika sana pia vitu vidogo vidogo vingine vinaonesha kama gari imetumika sasa hapo nimebaki njia panda

Sasa naomba wajuzi wa hizi mambo wanisaidie maana kuna mtu akanambia hiyo gari watakuwa wamechezea ODO wamerudisha nyuma KM kwa namna fulan sikupingana na ushauri wake hasa kwa mazingira hayo, hebu mnisaidie inawezekana kufanya mchezo huo kweli?

Kaondoa moja ya mwanzoni Km sahihi ni 138900.
 
Nimepata mashaka makubwa sana baada ya kutizama hizo kilometre na usajili wa gari yaan gari imesajiliwa mda mrefu lakin imetembea km chache sana nika muuliza kulikoni gari inausajili wa BAC wa muda mrefu lakini gari imetembea km chache kiasi hiki ? Akanijibu tangu imenunuliwa ilikuwa haitumiki sana...
Hii kitu inafanyika kila mahali labda kàma umenunua mpya kwa maana ya Zero Km, kama huamini nenda showroom yoyote, ulizia gari, waiwashe then soma Odometer utakuta ina range 50,000- 70,000km kwa asilimia kubwa kisha sikiliza mngurumo wa engine, kama ni mzoefu utajua tu kuwa imechezewa. Yaani nngurumo wa engine na odometer havina uuhusiano.

La mwisho, angalia kwenye safety belt kunakuaga na sticker au hapa mlangoni kwa chini (nashindwa kukueleza), kunakua na sticker inayoonyesha km gari ilikuja nazo though wengi wale waliobobea huwa wanazitoa, ukikuta wametoa hio label weka mashaka.

Ushauri, usinunue gari Tz kwa ushawishi wa uchache wa km, angalia bajeti yako, umuhimu wako wa kutaka gari muda huo, uzima wa body na kama Haina ajali na legal documents. Huu ni ushauri binafsi
 
Washa usikie injini ina semaje au ukipata fundi anaye jua gari tena hakikisha hupo naye karibu na unamjua maana kuna watu wanatabia ukipeleka fundi wanampa chake kukuthibitishia kuwa gari aina tatizo

mkuu nakuomba PM, nimeshindwa kukutumia msg. nina shida serious
 
Nimepata mashaka makubwa sana baada ya kutizama hizo kilometre na usajili wa gari yaan gari imesajiliwa mda mrefu lakin imetembea km chache sana nika muuliza kulikoni gari inausajili wa BAC wa muda mrefu lakini gari imetembea km chache kiasi hiki ? Akanijibu tangu imenunuliwa ilikuwa haitumiki sana...
Kwa kifupi kurudisha kilometers ni jambo lipo kabisa.

Sasa kama unataka kununua gari second hand especial kama hiyo kuna vitu vya kuangalia.
1. Bado hiyo injini iko kwenye ubora?
2.Body
3.Bei iendane na gari anayokuuzia ...Gari kama hiyo kilometers si kitu cha kuongelewa tena.
Bibi Mzee ni Bibi Mzee hata kama hakufanikiwa kupata Mtoto ...hawezi jiita msichana.
 
Hahahaha huwezi kuondoa moja, sema kapunguza kijinga, unaweza kupunguza around 50,000 kutegemea na hali ya Gari na usajili wa gari. Huyo aliyepunguza ni boya
Waswahili bwana sio watu wazuri ni ujanja ujanja kila mahali
 
Nafikiri 99% utakuwa sahihi mkuu au itakuwa ndio kazi yako inayokuweka mjini....

Jamaa yangu alishawahi kufanyiwa huo Uhuni ndio nilikuja kumtonya gari ilikuwa na km chini ya 50000,wajapenga walivyotuma B/L nikamwambia anitumie Chassis number ,nikaingia online kuisearch ile Chassis ikanipa link ya hiyo gari ilikuwa Tradecarview inauzwa,kuifungua hiyo link nikakuta kweli ni gari ile ile ila km zilikuwa halisi ni zaidi ya laki baada ya kuangalia vizuri ni kwamba wajanja waliomuuzia walifuta tu moja ya mwanzoni na kubakiza digits za mbele.
 
Kwa kifupi kurudisha kilometers ni jambo lipo kabisa.
Sasa kama unataka kununua gari second hand especial kama hiyo kuna vitu vya kuangalia
1. Bado hiyo injini iko kwenye ubora?
2.Body
3.Bei iendane na gari anayokuuzia ...Gari kama hiyo kilometers si kitu cha kuongelewa tena.
Bibi Mzee ni Bibi Mzee hata kama hakufanikiwa kupata Mtoto ...hawezi jiita msichana.
Nashukuru kwa ushauri
 
Jamaa yangu alishawahi kufanyiwa huo Uhuni ndio nilikuja kumtonya gari ilikuwa na km chini ya 50000,wajapenga walivyotuma B/L nikamwambia anitumie Chassis number ,nikaingia online kuisearch ile Chassis ikanipa link ya hiyo gari ilikuwa Tradecarview inauzwa,kuifungua hiyo link nikakuta kweli ni gari ile ile ila km zilikuwa halisi ni zaidi ya laki baada ya kuangalia vizuri ni kwamba wajanja waliomuuzia walifuta tu moja ya mwanzoni na kubakiza digits za mbele.
Hii hatari sana sasa wapi kuna usalama maana YARD nako nasikia ujanja ujanja tu , mkononi nako ujanja ujanja tu labda sasa niagize mwenyewe japan
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom