Hii ya jeshi kuomba billion sabini kuanzisha benki imekaaje?

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Hii ya jeshi kuomba billioni saba kuanzisha benki iko vipi hii? leo wameomba hizzo billioni sabini kesho hawatotuomba uhuru wetu kweli?
 
Hujaeleweka mkuu, wameomba wapi, kwa nani, ili iweje? Nani kaongea kwa niaba yao? Hawajatoa maelezo ya chanzo cha wao kuomba?

Well, je watakaonufaika na benki hii ni kina nani?
 
Kila kitu kinawezekana hii Bongo, ila tupe habari iliyokamilika ila tuelewe vizuri
 
Hii habari ni ya zamani sana wakati jeshi linaadhimiasha miaka ya kuzaliwa kwake. Mwmunyange alipropose mpango wa kuanzisha JESHI SACCOS ili kusaidia wanajeshi kupata sehemu ya kuomba mikopo bila bureaucracy. Sidhani kama ina tatizo lolote.
 
Waende wakaombe kwa Shimbo na asubirie huyo Shimbo siku tutakapo pata uhuru wetu na yeye atakuwa ni 1 tutakao wanyonga kwa uhujumi uchumi
 
Je ni sahihi jeshi kuwafanya ujasiliamali?

Ni sahihi sana, Jeshi la Ujerumani linamiliki night clubs, Jeshi la Croatia linasifika kwa kutengeneza juice ya passion, Jeshi la Canada limepata umaarufu mkubwa sana kwa kutengeneza vitafunio na tambi za paketi. Sioni tatizo kwa jeshi letu kufanya ujasiriamali, muhimu ni kuangalia kusiwe na mgongano wa kimaslahi na usalama wa wananchi.
 
Wala hujaeleweka mkuu. Toa ufafanuzi basi. Wameomba wapi? Ili waanzishe benki ya nini?

kama upo dar nenda lugalo kabla ujafika darajani angalia upande wako wa kushoto utaona jengo la benki ya ngome pamoja na saccos..
 
JWTZ wanataka kuiga kama jesh la Rwanda, kuwa na benk yao, so ile SACOS yao ya NGOME iwe bank, wel n wazo zuri wajiwezeshe kwa mikopo, mkulu anawayayusha ok its good. But hyo captal ni kubwa mno. Wapatiwe hata bi10, enough
 
benki itakayoanzishwa inalenga zaidi kumsaidia mwanajeshi na si jeshi kama jeshi..., kwa mfano.., mwanajeshi ana familia, anapenda watoto waende shule nzuri, ajenge, aanzishe biashara, basi anaomba mkopo ambao utakua na masharti nafuu.......

Kwa idadi ya wanajeshi nchini..., nusu yao tu wakiwa wateja wa benki hii..., benki itajiendesha kwa faida at the same time itatimiza lengo la kuwasaidia walengwa
 
siungi mkono jeshi kuwa na hiyo move.... kuna hatari kubwa sana mbele yetu hawa jamaa wanahodhi nguvu sana kwa sasa
 
Mimi naona imekaa fresh. Watu wawezeshwa wapate maendeleo kuogopana kuishe 2pate maendeleo. ndugu zangu ktk jfkuliko wanajeshi kuwa km meremeta Jeshi linatakiwa kiwe chombe kisafi 2kipata hawa marais wenye ambition kubwa ya wizi liweze kunyaganya nchi.
 
Wazo sio baya, lakini jeshi linatakiwa kufanya kazi ukiachia wachache wenye taaluma walio ktk vitengo vidovidogo jeshini, kama alivyo toa angalizo waziri mkuu mstaafu bw. Cleopa Msuya, kwamba jeshi letu halina kazi ya kufanya ipo haja ya kulitafutia kazi hata za kulima.
 
Je Wanajeshi wanaofikiria ujasiliamali wanaweza kupigana vita kwa moyo wao wote kweli? Kila mtu anataka kuwa tajiri hata wanajeshi nani atalinda nchi?
 
Waende wakaombe kwa Shimbo na asubirie huyo Shimbo siku tutakapo pata uhuru wetu na yeye atakuwa ni 1 tutakao wanyonga kwa uhujumi uchumi

Watoto wetu wananyimwa mikopo kwenda vyuo vikuu eti serikali inasema haina fedha ; jeshi linaomba fedha kuanzisha saccos zake nao wanaambiwa hakuna fedha , wakati sio siri tena kuwa mnadhimi mkuu wa jeshi letu SHIMBO ana shillingi trillioni tatu kwenye account yake huko bondeni!! Serikali kwanini haimlazimishi azirudishe kama walivyorudisha wale wahindi wa EPA halafu tuzitumie kuwasomesha watoto wetu. Naomba kuwasilisha wana janvi.
 
Hii habari ni ya zamani sana wakati jeshi linaadhimiasha miaka ya kuzaliwa kwake. Mwmunyange alipropose mpango wa kuanzisha JESHI SACCOS ili kusaidia wanajeshi kupata sehemu ya kuomba mikopo bila bureaucracy. Sidhani kama ina tatizo lolote.


Kazi ya Jeshi ni security, kazi za finances ni za financial institutions. Jeshi likitaka hayo basi liwasiliane na benki. Tunatakiwa kwenda mbele na si kurudi nyuma.
 
hawahitaji benk. kama wana saccos zao na kuna maduka yao duty free wanajinunulia mabati na furniture inawatosha.
 
Je Wanajeshi wanaofikiria ujasiliamali wanaweza kupigana vita kwa moyo wao wote kweli? Kila mtu anataka kuwa tajiri hata wanajeshi nani atalinda nchi?
mkuu wewe unaishi dunia gani? Jeshi ni ajira kama zilivyo ajira zingine. wanategemewa na ndugu kibao kwa ajili ya kuendeleza the so called extended family. wake up woman/man
 
Back
Top Bottom