Hii ya huyu waziri ni kiboko!

MONTESQUIEU

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
847
Likes
2
Points
0

MONTESQUIEU

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
847 2 0
Leo hasubuhi clouds kipindi cha magazeti nimesikia waziri wazamani wa mambo ya ndani ameenda ofisini kwa mbunge wa mwanza nymagana na kung`oa vitasa na kubeba picha ya rais kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe..

Je imekaaje hii?
 

MKURABITA

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2010
Messages
311
Likes
10
Points
35

MKURABITA

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2010
311 10 35
Leo hasubuhi clouds kipindi cha magazeti nimesikia waziri wazamani wa mambo ya ndani ameenda ofisini kwake na kung`oa vitasa na kubeba picha ya rais kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe..

Je imekaaje hii?
Masha ang'oa vitasa ofisi ya Mbunge Mwanza

Tuesday, 30 November 2010 01:46


Frederick Katulanda, Mwanza
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amehamisha vifaa mbalimbali vya ofisi ya Bunge Jimbo la Nyamagana, kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe kipindi uongozi wake. Akizungumza na Mwananchi jana, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, alisema baada ya kutoka Bungeni alikwenda kuingia katika ofisi hiyo, lakini baada ya kukabidhiwa alikuta vitasa vya mlango, simu ya mezani picha ya Rais na samani za kukalia vikiwa zimechukuliwa.

Kwa mujibu wa Wanje, baada ya kufuatilia aliambiwa kuwa vifaa hivyo viliondolewa na Masha kwa madai kwamba, alivinunua kwa fedha zake mwenyewe.

"Nimefuatilia kwa DAS (Katibu Tawala wa Wilaya) nikaambiwa amechukua Masha, nikafuatilia kwa Katibu Tawala wa Mkoa yeye alijibu kuwa naye alifuatilia suala hilo kupitia kwa Das na kupewaa majibu kama yangu, sasa sijajua ni kwa nini, ninavyojua ofisi haipaswi kukosa samani kwa vile kuna fedha za kununulia vitu hivyo," alisema.

Kwa Upande wake, Masha alikiri kuondoka na vitu hivyo na kwamba, asingeweza kuacha vifaa vyake binafsi katika ofisi hiyo.

Masha alisema vifaa alivyoondoka navyo ni vile tu ambavyo ni mali yake.

"Wakati naingia hapa nilikuta ofisi ikiwa na kiti kimoja na meza tu, vifaa vingine niliweka vyangu, kama kompyuta na meza zake, simu na samani nyingine kulingana na mahitaji yangu," alisema Masha.
Alisema Wenje anapaswa kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa wilaya, ili kupewa vifaa vya ofisi hiyo ambavyo yeye aliviondoa alikuwa havitumii kwa vile wao wanajua vilipo.

"Jamani vifaa vya ofisi anapaswa kuuliza ofisi ya mkuu wa wilaya, sasa kama anataka nimwachia na vyangu binafsi, mie nimetoa vyangu…hivyo vya ofisi vipo, nadhani amefika na kukutana na kiti kimoja na meza vile vingine vilivyokuwemo pia vilikuwa mali ya ofisi," alieleza Masha.

Hata hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza (RAS), Doroth Mwanyika, hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa nje ya ofisi, lakini ofisa mmoja wa ofisi yake alithibitisha kuwepo kwa malalamiko ya Wenje na kwamba, yalikuwa yakishughulikiwa.

Source: Mwananchi
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2007
Messages
4,736
Likes
88
Points
145

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2007
4,736 88 145
Sasa kama tunamruhusu mtu binafsi aeke vitasa vyake katika ofisi ya serikali tunategemea nini? Panatakiwa ipitishwe sheria kuwa mtumishi atatumia samani na vifaa alivyovikuta na kama ataingiza vya kwake itakuwa kama mchango wake na hataruhusiwa kuondoka navyo muda wake wa utumishi utakavyoisha.

Amandla.........
 

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2007
Messages
2,816
Likes
51
Points
145

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2007
2,816 51 145
Hii ndio aina ya Viongozi tunaowapa dhamana ya Kutuongoza. Kwani angeviacha angepungukiwa na nini? Usikute siku alipoviweka kulikuwa na sherehe ya kumshukuru kwa mchango wake!
 

zoeca

Senior Member
Joined
Nov 24, 2010
Messages
124
Likes
1
Points
35

zoeca

Senior Member
Joined Nov 24, 2010
124 1 35
upuuzi hivyo vifaa si aliviandikia vocha kwa taratibu za kiserekali na akalipwa? sasa kuchukua kunaonyesha alivyo fisadi
 

Forum statistics

Threads 1,203,553
Members 456,824
Posts 28,118,457