Hii ya DC na kitoweo imekaaje jamani?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Date: 9/8/2009

DC: Nyama iliyokamatwa ilikuwa kitoweo cha Mwenge

Na Waandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Mvomero Fatma Mwasa, amesema kuwa nyama ya wanyama saba aina ya swala waliokamatwa na maafisa wanyapori kutoka kwa wawindaji waliowapata ndani ya hifadhi ya wanyama pori ya Wami Mbiki Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, walikuwa kitoweo kwa wakimbiza mbio za mwenge.

Akizungumza jana na Mwananchi alisema uamuzi wa kutafuta kitoweo hicho cha swala kwaajili ya shughuli ya mbio za mwenge ulifikiwa na kamati ya maandalizi ya mbio za mwenge.

Mwenge huo wa Uhuru ulikuwa mkoani humu kuanzia Agosti 27 hadi Septemba 2 mwaka huu.

Askari wa hifadhi hiyo waliwatia mbaroni watu wanne wakiwa na gari la serikali na wanyama saba aina ya swala wakidai wametumwa na DC Mwasa.

Mwasa alisema kwamba, hakumtuma mtu kwenda kuwinda mnyama wa aina yoyote katika hifadhi hiyo na kwamba hahusiki hata kidogo na uwindaji huo.

“Mimi sihusiki katika kashfa ya ujangili na taratibu za mwenge zinajulikana, ninachokataa ni kwamba sijahusika hata kidogo, sijui wameenda kuwindwa mbuga gani na mimi sijaenda,” alisema DC Mwasa na kuongeza:

Alisema uamuzi wa kutafuta wanyama ulitolewa na kamati ya maandalizi ambayo wajumbe wake ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (Ded), DC na hata jeshi la polisi na sio kama ni mtu mmoja tu.

“Kikao halali kilifanyika cha kamati, kumbukumbu za kikao zipo, idara husika ilipewa jukumu la kutafuta wanyama hao. Sijui walienda pori gani au kama kuna barua iliandikwa,” alisema DC Mwasa na kuongeza:

Wakati huo huo Jumuiya ya Hifadhi ya Manyama pori ya
Wami-Mbiki mkoani Morogoro imemshitaki mkuu huyo wa wilaya kwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili kwa njia ya simu, Katibu wa Jumuiya hiyo, Majaliwa Saidi Kayanda, alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya mkuu huyo wa wilaya kushinikiza jumuiya hiyo imtake radhi na kukanusha tuhuma zinazomkabili.

Katibu huyo alisisitiza kuwa jumuiya hiyo haiko tayari kuomba radhi na kukanusha tuhuma hizo huku akimtaka mkuu huyo wa wilaya kuomba radhi kutokana na tuhuma ya kuwatumia raia kuwinda katika msitu wa hifadhi wa Wami-Mbiki kinyume cha sheria.

Kayanda alisema kuwa wamelazimika kumshitaki kwa kumwandikia barua Waziri wa Maliasili na Utalii na nakala kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya za Morogoro na Pwani juu ya suala hilo ili kulitafutia ufumbuzi kutokana na kitendo cha mkuu wa wilaya hiyo kuwatisha viongozi wa jumuiya hiyo. Imeandikwa na Samuel Msuya na Venance George, Morogoro na Salim Said.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
armpit-smell.jpg
 
Yani kati ya ma DC vilaza huyu ni mmoja wapo, hii ndo kazi ya JK ya kuajili vilaza kama hawa kisa ndugu yake. sasa ona anayojichanganya hata kujieleza hajui. Sasa kama yeye pia ni mwanakamati kwa nini asibebe jukumu anabakia ooh, sio mimi niliowatuma ila kamati, ooh mi sijui hata msirtu walioenda wala sijui kama walipewa kibali, what a shame, and she is supposed to be a DC! Na huo mwenge wenu wa ccm utawafikisha kubaya, kwani walishindwa kununua ng'ombe kwa kutumia pesa zenu za kifisadi hadi mwende kuua wanyama pori na wakati ndo nyie nyie na serikali yenu ya kifisadi mnopiga kelele kuhusu kutunza mali asili, nimechoka mimi jamani, aibu tupu.
 
Siyo tu kuwa mwanakamati, DC ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mwenge (Wilaya). DED ni Katibu wa kamati na wajumbe ni WEOs, VEOs, Watalaamu, Wafanyabiashara (wawakilishi) etc. Hivyo ni kweli kuwa huyo DC ndiye aliyewatuma. Labda tuseme kwamba Afisa Maliasili (W) hakutoa maelezo mazuri namna watakavyowinda hao wanyama. DC yeye alimwachia DED na Afisa Maliasili walishughulikie nao wakavunja sheria. Hapo DC hawezi kujivua lawama hata kidogo.

DC anakosea zaidi kuitaka menejimenti ya hifadhi imwombe radhi, bali alistahili kuwapongeza kwa kazi njema na kuwaomba radhi kwamba kamati yake ilikosea kutofuata taratibu za uwindaji kwenye hifadhi.
 
Dawa ni kumkomalia mpaka mwisho ili iwe mfano kwa watawala wengine wasio environmental concious. Big shame kwa mtu wa ngazi ya juu kutoa idhini ya kuwinda wanyama ili wawe kitoweo ktk mbio za mwenge. Inamaana mbuzi,n'ombe,kuku,bata,samaki,maharage,kisamvu mmeshindwa kupata mpaka mkaue such a big number of wildlife? Hivi mpo serious kweli jamani? Hatutakubali kwa hili lazima tufikishane mbali tu. WWF-TZ,WCS,LEAT, JET amkeni tusaidiane ktk hili please. Tushikamane tutokomeze uharibifu huu nchini.
 
Wala JK hana kosa ktk hili. Rais kwanza anastahili kupongezwa kwa kujali jinsia ktk uteuzi, labda huyu mama kama aliwasilisha vyeti feki hili ni suala jingine na vyombo vya sheria vipo nadhani vinaweza kufanya kazi yake.

Kuhusu uwindaji bila kibali, hili ni kosa kwanza la wale waliokamatwa kwa sababu wewe unajua kwamba ili uwinde ktk game reserves lazima upate kibali. Kwa hiyo ilikuwa ni jukumu la waliotumwa kuomba kibali maliasili na utalii, lakini kama walikurupuka tu eti kwa sababu walitumwa na DC, wao ndo wajinga na wananstahili adhabu kali.

Hii ndo inayotufanya watanzania wakati mwingine tumlaumu rais kikwete lakini ukichunguza unakuta watendaji ndo wazembe na wengi wao ni vihiyo. Unapotumwa na mkuu wako wa kazi kitu fulani, siyo kwamba kakwambia usifuate sheria wakati unatekeleza majukumu yako yanayohusu kile ulichotumwa, labda awe amekupa barua kwamba fanya na usifuate sheria.

Tukio hili ndo linaonyesha kansa ya utawala wa CCM kwamba ukitumwa na boss basi usifuate sheria. Kumbuka yule mkurugenzi wa halimashauri fulani alikataa kulipia malazi ya ugeni wa makamuwa rais dk shein wilayani kwake kwa sababu sheria haimruhusu kufanya hivyo kwani msafara wa shein unalipiwa na serikali kuu, lakini DC wake asiye jua sheria alisha mshikia bango DED kuwa kafanya makosa.

Kwa hiyo kwa tukio hili watendaji wote wa umma lazima mjifunze kufuata sheria pale unapotumwa kufanya chochote na mtu yeyote hata kama ni rais, labda tu kama amekupa maandishi yanayosema usifutae sheria.
 
Kaka as long as wewe ni CCM hakika hata vyeti hawaangalii na hakuna mamlaka inaweza kukugusa . Unamkumbuka Chitalilo na vyeti vya ku foji ? Kesi iliishia wapi ? Na hao mawaziri je kaka ?
 
Back
Top Bottom