Hii wezesha wezesha ndio imetuletea na kina Anna Makinda?

Chura

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,345
2,296
NEC ya mh Lubuva ilianza ikatoa mgawanyo wa viti maalum ubunge kwa vyama vya siasa na sasa imetoa mgawanyo wa viti maalum kwa udiwani.

Viti maalum ni kwa ajiri ya wanawake ili kuondoa mfumo dume wa maamuzi ndo ikaja hiyo Sera ya kuwawezesha wanawake(women empowerment)
Huu mfumo ni mzuri kwa sababu Una lengo la kuleta uwiano wa kiutendaji Kati ya jinsia zote.

lakini tatizo mfumo huu nchini kwetu umekua wa kimazoea nafasi zinatolewa kimazoea zoea yani haijalishi muwezeshwa anaimudu hiyo nafasi au lah anapewa tu.

Kwa nchi masikini Kama Tanzania huu si wakati wa masihara yanamna hii yakuchaguana kwa kujuana juana yana athari Sana kwa maendeleo ya nchi yetu haijalishi muwezeshwa ana uwezo au la ila kwa kuwa muhusika ni Hawara, ndugu, Shemeji au mke wa fulani basi anatunukiwa muwezesho wa viti maalumu jaman bungeni pale sio nyumba ya ukoo ni mahali ambapo watanzania wanatetewa na kusaidiwa.

Kwa mfumo huu wa mazoea zoea ya kuwawezesha wanawake ndo CCM ikatuletea spika wa bunge anayemaliza mda wake Anna Makinda na kumtema mzee 6 kwa kigezo kuwa saa hivi tunataka m/mke matokeo yake Spika alishindwa kutenda haki kwa nafasi yake aliyonayo bungeni. Hakuwatendea haki wabunge wa vyama vya upinzani?.mbaya zaidi kiti chake kilipoonyesha wazi kuegemea chama na serikali ya CCM katika mijadala ya kitaifa na wananchi wake hali ilipozidi kuwa mbaya uvumilivu ulimshinda Pr Lipumba akayasema haya namnukuu.

" Spika amejionyesha uwezo wake mdogo wa kuongoza Bunge na akubali kushauriwa au kubadilika kifikra ili alinusuru Bunge lisiendelee kudharaulika ndani na nje ya nchi""

Rais aliyemaliza mda wake naye alituambiaga kimazoea zoea hivyo hivyo kuwa ntawaletea makamu wa raisi mwanamke na kweli katuletea mama Samia sina uhakika Kama Jk amewaletea watanzania mama huyu kwa kuwa anauwezo wa kuongoza au aliona kwa kuwa ni mwanamke basi ngoja tu nimuwezeshe na kwa hili nauachia mda uamue.

Hii tabia ya kuwezeshana ndo inaua weredi wa ufanyaji kazi wa wanawake nakujikuta wakifanya kazi ili kuwafurahisha waliowawezesha(pleasing the empowerer).

Mi nadhani huu mfumo wa viti maalum ungefutwa ili hizo pesa zikaongeze nguvu kuwasomesha wanawake wengi ili wengi wao nao waweze kukidhi vigezo vya kuongoza mihimiri inayounda taifa Kama bunge na serikari huku wakijua kuwa ni elimu na juhudi zao ndo zilizowafikisha hapo walipo na sio mtindo wakuwezeshana au nafasi hizi ziwe viti maalum kwa kundi maalum tu (special group) ...walemavu eg maalbino(albinos) na Wasioona(blind people)na makundi ili wakawakilishe makundi hayo kutetea na Kupigania sheria zinazo yahusu makundi hayo ...lakini mtu ana nguvu zake eti anapewa ubunge au idiwani huu ni ujinga wa kiwango cha platinum (stupidity of the plutinum peak).

Unajua kwa nchi Kama Marekan na mataifa mengine ya magharibi kwa yalipofikia hata yakifanya mizaha mizaha ya kuwezeshana sio mbaya Sana ukilinganisha na sisi.Sisi bado ni maskini mno tunahitaji uwajibikaji wa hali ya juu walau tuifikie hata Kenya kiuchumi ila tukiendelea kufurahishana kwa kuwa wezesha wake, mashangazi na dada zetu sidhani Kama tutafika kwenye maisha bora kwa kila mtanzania tuliyohaidiwa uko nyuma ila kwa ajiri ya mizaha Kama hii maisha bora kwa kila mtanzania yakageuka maisha bora kwa kila mtanzania kiongozi mbona China ni tajiri lakini haifanyi haya kwani China Ina wanaume peke yao??

Elimu na Juhudi zao ndo ziwaruhusu kupata Nyadhifa wanazozitaka lakin sio kuweshana.Mbona tuna mifano mizuri si ni juhudi na uwajibikaji ndo umewapeleka kina Mdee na Esther dodoma.

Tuwe na Sera kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania ila tukianza kutengeneza Sera kwa ajiri ya kuwafurahisha wamarekani kuwa na sisi na washirika wazuri wa demokrasia basi ni dhahiri tunatengeneza ndoto mpya ya maisha bora kwa kila mtanzania.

Unazizungumziaje nafasi za viti maalum je zina msaada wowote kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania?

Je, ungependa ziendelee kuwepo au zifutwe?

KARIBU
 
Back
Top Bottom