hii wapinzani kuzuiwa kufanya Mkutano Donge imekaaje ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hii wapinzani kuzuiwa kufanya Mkutano Donge imekaaje ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtu wa Pwani, Oct 16, 2010.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  jamani hii habari sijaielewa huyu anasema kweli au just ndio fitna zenyewe?

  iweje donge wakatae kufanyika mikutano ya siasa hule kwao?  source Michuzi

  ZENGWE LA KAMPENI JIMBO LA DONGE
  Habari Kaka Michuzi,

  natuai humzima na unaendelea vyema na libeneke.naomba uwape wadau hii ili waweze kuchangia maoni yao.

  Kulikuwa na tetesi na hatimaye mwaka huu yalirushwa rasmi matangazo katika baadhi ya vituo vya redio na wanaojiita wazee wa jimbo la donge kwamba hawataki mikutano ya kampeni jimboni mwao.

  Hali hii imedhihirika jana baada ya viongozi wa CUF kuhitilafiana na kikundi kidogo cha watu walioaminika kuwa wakaazi jirani na eneo ambalo lingefanyika mkutano jumamosi ya leo tarehe 16/10/2010, hivyo mkutano kufutwa ili kuepusha ghasia ambazo zingejitokeza.

  Shamhuna amekuwa nyuma ya kikundi kidogo cha wazee hapo jimboni kwake kuzuia demokrasia ikiwa ni pamoja na kura ya maoni iliyofanyika Julai 31 mwaka huu ambapo kura nyingi za hapana zilipatikana kupinga kuwepo na serikali ya kitaifa baada ya uchaguzi oktoba 2010 baada ya kuaminika kupiga kampeni ya kimya kimya.

  Mnamo kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005, Shamhuna alitumia nafasi yake kama naibu waziri kiongozi na waziri wa habari na utamaduni kuwaamrisha polisi kuzuia wanachama wa upinzani umbali wa maili 6 toka jimboni donge walikokuwa wakienda kuhudhuria mkutano wa kampeni hali iliyosababisha ghasia iliyoleta usumbufu na watu kadhaa kuumizwa.

  Tayari viongozi wa upinzani wameanza kutuhumu baadhi ya viongozi waandamizi serikalini kwa kubeza na hatimaye kuuhujumu muafaka uliofikiwa.
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Interesting...
   
 3. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Huo ndio upuuzi wa Wa Zenj, kutumiliwa na wanasiasa waovu,washari na wenye kama chuki Shamhuna. bila ya faida yoyote.
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  CUF walilikoroga na sasa wawe tayari kulinywa na waache kulialia. Huku wataka na kule wataka wasipoangalia kote watakosa kwani haiwezekani Zenji muwe marafiki halafu huku bara mwatoana macho ! Ati viongozi wa kitaifa hao hao wachekeana visiwani usiku, wanuniana bara mchana - ukisikia unafiki ndio huu ! Ndio maana wengine hatutaki upuuzi huo, HATUDANGANYIKI ! CUF na CCM lao moja !
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ni kweli wakuu, joto hili limekuwa kwa wiki nzima sasa Zanzibar...ikiaminika kuwa muhuni Ali Juma Shamhuna, mwakilishi aliyemaliza mda wake jimbo la Donge na wahuni wenzake anaowaita wazee wa Donge, wamepanga njama na serikali ya Wilaya ya kaskazini B, kuhujumu demokrasia na utawala wa sheria,unaotoa haki sawa kwa vyama vyote kutangaza sera zake, popote pale mradi taratibu zimefuatwa.

  Muhuni Shamhuna na wajinga wenzake, wameendeleza kile ambacho walikuwa wakikifanya tokea mfumo wa vyama vingi kuanza katika jimbo la Donge kuwa "siasa ni uhasama na chuki" hivyo kwao wao upinzani hasa CUF ni "maaduwi wa kuchukiwa na kuhasimiwa milele".
  Huu si mtazamo wangu bali ni hali halisi ya jimbo la Donge lilivyo, kwani hata wakati wa kura za maoni wananchi walipotoshwa makusudi wakiambiwa kuwa wakipiga kura ya ndiyo wanampeleka Maalim Seif ikulu, bila ya kujijuwa kuwa Zanzibar ni zaidi ya Maalim Seif na siasa za kivyama.

  Kwa uungwana na ustaarabu, na kuamini kuwa huu si mda wa kuendeleza siasa za malumbano na kuwapa faida maaduwi wa Zanzibar waliojificha ndni na nje yake, chama makini cha wananchi CUF, kinachokubalika Tanzania na Zanzibar, kimeamuwa kufuta mkutano huo katika jimbo hilo na kutumia njia mbadala ya kampeni ya nyumba kwa nyumba jimboni humo, katika mkakati wa makusudi kuwafunuwa vichwa ndugu zetu wa Donge, wanaopotoshwa na muhuni Ali Juma Shamhuna na wajinga wenzake wanaojiita wazee wa Donge.
   
Loading...