mzee wa kijiwe
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 947
- 685
Vita dhidi ya madawa ya kulevya ambayo imetangazwa kwa mbwembwe na Mkuu wa mkoa wa Dar nahisi labda ni geresha tuu!
Kwanini nasema hivyo!
Kwa wanaoijua Dar watakubaliana na hoja zifuatazo
1. Unapotaja Dar kwanza picha ya kwanza ni Posta,,Ferri, na nk hapa ndipo ikulu ilipo kwa sasa kabla hawakimbia mji kwenda Dodoma, hapa ndipo makao makuu ya Polisi hata hiyo mnayoisikia inaitwa central IPO hapa, hapa ndipo viongozi wote lazima wapite Kama sii Mara mbili kwa siku basi hata Mara NNE.
2. Ni takribani wiki mbili sasa zimepita tangu zoezi hili la ki mazingamwe lianze kubamba vichwa vya baadhi ya radio zao,tvzao,magazeti yao!
3. Ukipita hapa Ferri Kama unaelekea Kariakoo kwa njia ya mwendokasi, kituo cha Posta ya zamani, hapa kuna genge narudia genge la vijeba wanavuta, wanajidunga hadharani madawa ya kulevya asubuhiiii mchaaaana wote tunawaona isipokuwa polisi tuu ambao muda wote tunapishana nao ndio hawaoni, kumbuka ni Mita Kama Mia mbili tuu kutoka hapa walipo hawa jamaa hadi hiyo central ya polisi ambayo kwa sasa imegeuka kuwa ya kina Manji.
4. Njoo hadi kituo cha Kisutu hapa ni kichekesho, baraza yote nyumba karibu tatu kabla ya Redcross building majamaa wamelala hoi na sindano zao mkononi, hatua Kama kumi tuu mbele yao nawaona polisi wapo bize kukamata bodaboda ili wakang'oe tairi, hawageuzi USO kuwaangalia hawa jamaa na hawa jamaa naona wanafahamiana sana na hawa polisi kwani hawana hofu hata kidogo! Udenda unawatoka unapopita na ka simu kwa smart phone wanataka wakupore, ukikaa vibaya wanachukua mbele ya polisi!
Niambieni ndugu zangu hii vita inapiganwa Dar IPI????
Kama kweli Magu anasoma mitandao, au makonda anajua kuna jf basi tembelea hayo maeneo unijibu vita hii ni ya kweli??
Wito wangu kwako msomaji orodhesha na wewe maeneo unayoyajua ambayo ni vijiwe vya madawa haya ya kulevya hapa Dar na usifanye kwa mazoea pita wiki hii tuambie jee wapo???
Asante