Hii siku ya wapendanao nimepooza, nimekubali

Maya Angelou

JF-Expert Member
Oct 19, 2019
1,081
2,487
Siku imeisha kama hivyo muhusika mkuu kimyaa ,hivi kweli inawezekana kuna upendo kweli hapa‍♀️design kama tunategeana nani amuanze mwengine sijui kwakweli sipati majibu

Maisha hayako fair pembeni kuna watu watatu wamekazana na Mimi leo lakini hata siwa feel imebidi tu niwe mpole,ninae taka anishobokee ndio kajikausha hivi kwanini mambo yanaenda hivi lakini

Mwaka jana muda kama huu nilikuwa nimepigwa mizawadi, ujumbe mzuri, dinner ya nguvu nikajihisi kama malkia dunia yote yangu siamini huu mwaka mambo yameanza hivi(nimeguswa )

Najua na yeye huko atakuwa kapata wishes kwa watu wengine ila akili yake yote ipo kwangu,mimi ndio Khumbu wake
Ila seriously wanaume jitahidini kuepress hisia zenu msipende kujibana bana haswa nyie wanaume wa kichaga mna nini lakini

Nina bahati mbaya ya kupata wachaga,bora wasukuma aisee wachaga mmenishinda tabia

Update
Haki jana nilikuwa na stress Asanteni kwa kunipunguzia stress walau nilikuwa nacheka japo ndani naumia
Jana usiku sa mbili akanitafuta kwamba alikuwa amebanwa na kazi ndio ametoka muda huo(hapa sijui nilikuwa napangwa au vipi)kwakweli sababu ya hasira nikashindwa kujibu nikachuna kimya.
Leo tume reconcile bahati week nzima yupo free kwaio tumeanza kavalentine ketu leo mpaka next week
Ila Jana nilikesha nasali mpaka asubuhi Kwaio ni valentine ya kwanza nimepiga mkesha bila kupenda
Kuna watu mna roho mbaya mlikuwa mnafurahiii
Hatuachaniii🥰
 
Kuwa mpole tu mkuu,leo ni jumapili kama jumapili zingine sisi ambao simu za wapenzi wetu zimeisha charge tokea saa 12 asubuhi inabidi kesho tuandamane hadi kwa Kiongozi wetu mh Pole pole na zawadi tulizonunua tumeamua kuweka bond ili tupate pesa kidogo ya kunywa supu asubuhi
 
Back
Top Bottom