Hii tutaweza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii tutaweza

Discussion in 'Entertainment' started by Yo Yo, Jul 25, 2008.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Timu ya Taifa Pool yatangazwa kwa safari ya Swaziland
  Na Vicky Kimaro

  WACHEZAJI watano wa timu ya taifa ya pool wametangazwa rasmi jana tayari kwa safari ya Swaziland mwezi ujao.


  Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah aliwataja wachezaji hao kuwa ni Rajabu Matumla (Kinondoni 2), Edward Mgasa, Omary Akida (Kinondoni 2), Rajab Kajuna (Temeke) na Mohamed Jumanne (Mwanza).


  Alisema kampuni yake inaona fahari kubwa ya kudhamini timu inayoshiriki mashindano hayo ambayo Tanzania itashiriki kwa mara ya kwanza.


  ''Timu yetu itasafiri mwezi ujao kushiriki kwenda mjini Ezulwini kushiriki mashindano ya dunia,''alisema Butallah.


  ''Tunaamini wachezaji wetu wataiwakilisha nchi yetu vizuri na pia watapata fursa ya kuona jinsi nchi nyingine zinavyocheza mchezo wa pool,'' alisema.


  Wachezaji hao ni kati ya 10 ambao waliunda kikosi hicho cha timu ya taifa ya Pool kabla ya kuchujwa na kubaki watano.


  Kikosi hicho kitaondoka nchini Agosti 14 kuelekea Swaziland kwenye mashindao hayo yaliyopangwa kufanyika Agosti 14 hadi 23 yakisimamiwa na Chama cha Pool cha Afrika (AAPA).

  Tujaribu na draft,bao na karata
   
 2. senator

  senator JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2008
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kama wao wanaweza na sisi tushindwe tunanini!? Hope vijana wanafanya kweli ila inahitajika kupata japo mikanda ya video kuangalia jinsi wenzetu wanavyocheza isije ikawa kuna utofauti wa sheria tukaangua katika hilo.Nawapongeza TBL kwa kuushikia bango mchezo huu uzidi kuwa kwenye chat ya juu.
   
Loading...