GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,379
- 108,436
Na hapa ndipo sehemu pekee ambayo CCM yangu inanifanya niipende kwani inajua mno kufanya 'Utafiti' hasa ule wa 'Kujitathmini' yenyewe ili baadae ijue jinsi ya 'Kumkabili' na 'Kumshinda' Mpinzani wake mapema tu. Na sasa nimeamini kuwa Siasa ni 'Sayansi' na kujua 'Mvumo' wa Kipindi husika ilimradi tu uweze Kupata 'Kura' za Kutosha kutoka kwa wale ambao hukuwa na uhakika nao.
Leo nikiri tu tena hapa kuwa GENTAMYCINE nilikuwa ni 'Mshabiki' mkubwa sana wa 'Mpemba' Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kuwa ndiyo angefaa kuwa Mgombea 'Urais' huko Kisiwani Zanzibar kuliko hata Dakta Hussein Ali Mwinyi kwakuwa nilijua kuwa angeweza 'Kuzizoa' Kura nyingi sana za Wazanzibari wenye Msimamo mkali na wengi pia Wapemba kutoka Kisiwani Pemba.
Hata hivyo pale niliposikia kuwa CCM Kimemaliza na Kufanya 'Mchakato' wake wa ndani ( na ambao nauheshimu na niliuheshimu ) na kuamua 'Kumpitisha' Dakta Hussein Ali Mwinyi mwanzoni 'niliumia' kwakuwa nilijua ya kwamba bado CCM ingeendelea kupata 'Upinzani' mkubwa kutoka Pemba kwa Wapemba. Lakini 'Ushauri' alioutoa leo Mwenyekiti Taifa nimeupokea kwa Furaha kubwa.
Kitendo tu cha Mwenyekiti Taifa ( CCM ) Dakta John Pombe Magufuli cha 'Kumuomba' tena 'Kiunyenyekevu' kabisa Mgombea wa 'Urais' CCM Zanzibar na ambaye iwe isiwe atakuwa Dakta Hussein Ali Mwinyi 'ateue' Makamu wa Pili wa Rais kutoka Kisiwani Pemba kwa Wapemba nimepokea kama ni 'Ushindi' kwa CCM lakini pia ni 'Pigo' wa Wapinzani na hasa ACT-Wazalendo.
Kwa Kauli tu na Ushauri alioutoa Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Magufuli sasa ni rasmi kuwa Wapemba kupitia Mpemba Wao Profesa Makame Mnyaa Mbarawa nao wamekumbukwa kwani Dakta Hussein Ali Mwinyi akishinda 'Urais' wake 'atamteua' Yeye ( Mbarawa ) kuwa Makamu wake wa Pili wa Rais hivyo 'Kuwafurahisha' zaidi Wapemba na Kuona kuwa nao sasa wamekumbukwa.
Hakika nitoe tu pongezi zangu kwa Timu nzima ya 'Utafiti' ndani ya 'CCM' kwani hapa imecheza 'Karata' nzuri sana na 'itajishindia' mapema kabisa.