Hii trend (wanawake kuwa Juu) inatishia mstakabali wa Jamii yetu hapa Dar/TZ!

Hayo unayoyasema ndicho nilichomaanisha na ndiyo maana nikauliza Je matokeo yake yatakuwa nini? Kwa maana ukweli ni kwamba hawa Wanawake mara nyingi hawakubali kuwa na mahusiano na Mwanaume ambaye yuko chini yao kielimu, mapato n.k na hivyo hii hupelekea kushindwa kupata mwenza na hali hii tayari inajitokeza hapa Dar ni kawaida kukuta Mwanamke miaka 30 hajapata mwenza, sasa ukiangalia bigger picture hauoni kama jamii yetu itaathirika huko mbele?

Kuna haja gani ya kuwa na mwanamume anayeshinda vijiweni kutwa kujadili mpira wa Ulaya wakat hana wazo la kutafuta pesa? Maisha bila pesa hayaendi kaka na ndo maana wanawake siku hz tumejiongeza. Tunatafuta zetu
 
si kweli kwamba wanawake ni wengi kuliko wanaume kwenye vyuo fanya utafiti kidogo,ila suala wanawake kuwa juu ya wanaume halijasababishwa na wanaume wenyewe bali limesababisha na siasa tulizopewa na wazungu ndoo maana unaona viti maalum bungeni vigezo vya kujiunga na vyuo mbalimbali vikilegezwa kwa jinsia ya kike pamoja na sera zote za women empowerment.
 
Tatizo haujui kuwa wanawake wanakuja juu na watakuja juu zaidi...

Wakati wanawake wapo busy kujinoa katika field zao na kuwa competitive ..
Wanaume wapo busy katika mipira ya ulaya na kuwafikisha wanawake vileleni...

Kuna thread ilishasema kuwa maongezi ya vijana wa sasa asilimia 90 ni upumbavu..

Sasa utawezaje kushindana na MTU anayejinoa masaa yote
Mipira ya ulaya na kuwafikisha wanawake vileleni.....nimefurahi sana
 
Ukiongea na wadada wengi sasa hivi, atakwambia ndoa hazina maana muhimu tafuta maisha yako, ili hata ukiolewa mwanaume hawezi kukunyanyasa, na hata akikufukuza atakuwa na pakwenda.

Kwa maana nyingine wadada wengi wanaona kwamba wanaume hutumia uwezo wa kiuchumi kama slaha ya kuwanyanyasa.. Sasa ili kwenda sawa wanaona wakomae kutafuta maisha, na hii imewafanya wengi wao akipata fursa kidogo atahakikisha anachomoka.....

Wanaume tusipijipanga watatuzidi kila kitu na huenda wakaanza kuoa badala ya kuolewa...
Ni kweli wanaume wengi ni wanyanyasaji katika ndoa na ukiangalia mdada kasoma unadhani atafanya nini zaidi ya kuwaza kutafuta hela na kujikwamua kiuchumi wakati mwanaume anahangaika na kuhonga michepuko? Tena watakuja juu zaidi kama hali itakuwa hivi.
 
Nimekimbilia kuifungua thread hii ili nijue mtoa mada anamaanisha nini mwanamke kuwa juu. Kumbe kimaendeleo!!
Nilijua amechoshwa na style Moja kila Siku.
 
Izo ni hisia tuuu
Kwanza kuajiliwa sio kuwa na ela
Wanaume wako very selective hawafanyi kila kazi
Wanawake wanajishighulisha maanake ni kuwa
Wanafanya hata kazi za low quality
Pil wanaume ndio wenye uchumi mkubwa
Unakuta mwanaume mmoja kawafungulia vimada wa 4 maduka kkoo
Kwaio msione wana shine n kutokana na sisi wanaume
 
Hahahaaaaa! Hii topic nimecheka sana, yaani pasua kichwa kwelikweli kwa sababu ina makengeza. Mtoa hoja alikaa chini na kuifrem, kawapa wadau wamsaidie jibu. Hebu apatiwe majibu ya hoja.
 
Back
Top Bottom