Hii trend (wanawake kuwa Juu) inatishia mstakabali wa Jamii yetu hapa Dar/TZ!

Dume zima linalialia lipate haki sawa na wanawake... Yani mwanaume mzima unatamani mambo anayopata mwanamke nawewe uyapate? MAKONDA PITIA NA HUKU
 
Sasa kama unalipwa buku 7 kwa siku hapo Lukumba utaweza kushindana na mwanamke anaelipwa 1m kwa mwezi na kuendelea?
 
Hili ni janga la taifa sio DSM tu, watoto wa kiume wengi wanataka kuimba bongo fleva wawe kama Diamond, sasa kuwe na mkazo wa kuwasisitiza wanaume elimu kwanza.
inakera sana kila kijana kwa sasa ni msanii kibaya zaid kazi hawataki kufanya wanatakuwa kama diamond sana sana huko dar huku mkoani wanaimba na kufanya kazi
 
Athari zipi zinatokana na wanawake kuwa juu kielimu na kipato kuliko wanaume? Kudos kwa wanawake kujitambua na kupanga maisha yao acha wanaume wa Dar waendelee kushinda barbershops na kula chips mayai.
Kwasababu mleta mada amekuwa neutral nafikiri nasi tusiwe wepesi wa vihoja, tuwe neutral kwa maana kila kitu kina madhara yake hapa ulimwenguni na hili suala likiwemo
 
Tuliyataka wenyewe. Mungu alikuwa na maana kubwa kutupa sie wanaume uhusika mkuu ila kwa ujinga wetu tukapoteza msingi wake na sasa tunahaa. Kizazi hiki kimejawa na laana sana toka kwa muumba na huu ndo ukweli.
 
Wanawake wamefika hapo walipo kwa huruma zetu na upuuzi wa haki sawa, hivyo tuendelee kuwapa support tu kimapenzi, kikojozaji, kiwatoto, kibushoke na hata kimarioo kama ikibidi!
 
Nimejaribu kufanya utafiti wangu binafsi na nimegundua kwamba sasa hivi TZ na hasa mji wetu wa Dar na kwingineko, Wanawake wako mbele sana kimaendelo klk Wanaume, hapa siongelei namba kiujumla bali naongelea trend, kazi nyingi zinazolipa vizuri leo hii hapa Dar wadada ndiyo wanazipata, jaribu tu kutembelea ofisi ambazo zinalipa vizuri kuanzia mabenki, Kampuni za Simu au hata NGO's utaona wadada kwa kweli ni wengi sana!

Sasa hii ni hatari kwa ustawi wa jamii yetu, tayari kuna vijana wengi leo hii wanalalamika hawapati wenza, yaani imekuwa ngumu sana kwa maana ikumbukwe kwamba Wanawake siku zote na hii ni Dunia nzima huchagua Mwanaume ambaye labda yuko naye sawa au ambaye yuko juu yake hasa kwenye kipato, Elimu n.k na jinsi mambo yanavyoonekna huko mbele hali itakuwa ngumu zaidi kwani ukienda vyuoni Wasichana ni wengi zaidi wanaosoma klk Wanaume hivyo tunahatari ya kuwa jamii ambayo Wanawake wana uwezo klk wanaume na hivyo hii kuathiri jamii yetu, nini kifanyike?
Ni swali gumu sana kwa maana siyo kosa la Wanawake hali kuwa hivyo kwani ni juhudi zao wenyewe na sasa wanakaribia kushika usukani wa nchi!
Sina jibu lkn ukweli ndiyo huwo!

Sijui nikuambiaje! Ila wewe ni mwenye fikra hakinifu sana, hongera sana mkuu.
 
Jambo zuri wanawake nao wawe na kipato kizuri wawajengee na kuwanunulia magari waume zao
 
Naongelea bigger picture na siyo maisha ya Juma au Mwajuma bali naongelea mstakabali wa jamii yetu kwa ujumla wake kwamba kama Wanawake au Wanaume wanashindwa kupata wenza athari zake kwa jamii ni kubwa huko mbele na siyo kama Mtz xyz ana uwezo wa kupata Mwanammke au Mwanaume yoyote yule wkt wowote ule atakapo!
Kiufupi athari haiko direct the way u think, wanawake walio wengi wanapenda wanaume wenye fedha hivyo itafika point either wataolewa na wanaume wa watu walio na fedha zaidi yao au watazalishwa na hao hao wanaowazidi uwezo wa kifedha na kielimu
 
Japo sijafanya utafiti ukimleta dada yako sura mbaya sijui kama utaleta ushahidi huu tena uliouandika.
 
Hahaaa kweli mkuu hii obsession ya wanaune wa tz na mpira wa ulaya kwa sasa inakuwa kwa kasi na nadhani ni tatizo kwa kizazi chetu, mtu anajua details nyingi za wachezaji wa mpira, na klabu unakaa unajiuliza hivi hii ina relevancy gani kwa maendeleo yake na ya nchi.....???
Wanawake obsession yetu ni Wasafi classic, Zari kaandika nini Instagram, Diamond ame flirt na msichana gani but at least that's relevant to Tz, isn't it?
Isn't not
 
ninyi si mnabeti? pooltabke, kushangaa makalio makubwa, kuangalia mpira daily, wacha tufanye kazitujenge nchi! japo na sisi tunakosa wenza maana wanaume wengi ni tegemezi mabishooo kazi hawataki

Kuna mwimbaji aliimba "wanaume kama mabinti":(
 
Back
Top Bottom