Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Nimejaribu kufanya utafiti wangu binafsi na nimegundua kwamba sasa hivi TZ na hasa mji wetu wa Dar na kwingineko, Wanawake wako mbele sana kimaendelo klk Wanaume, hapa siongelei namba kiujumla bali naongelea trend, kazi nyingi zinazolipa vizuri leo hii hapa Dar wadada ndiyo wanazipata, jaribu tu kutembelea ofisi ambazo zinalipa vizuri kuanzia mabenki, Kampuni za Simu au hata NGO's utaona wadada kwa kweli ni wengi sana!
Sasa hii ni hatari kwa ustawi wa jamii yetu, tayari kuna vijana wengi leo hii wanalalamika hawapati wenza, yaani imekuwa ngumu sana kwa maana ikumbukwe kwamba Wanawake siku zote na hii ni Dunia nzima huchagua Mwanaume ambaye labda yuko naye sawa au ambaye (Mwanaume) yuko juu yake hasa kwenye kipato, Elimu n.k na jinsi mambo yanavyoonekna huko mbele hali itakuwa ngumu zaidi kwani ukienda vyuoni Wasichana ni wengi zaidi wanaosoma klk Wanaume hivyo tunahatari ya kuwa jamii ambayo Wanawake wana uwezo klk wanaume na hivyo hii kuathiri jamii yetu, nini kifanyike?
Ni swali gumu sana kwa maana siyo kosa la Wanawake hali kuwa hivyo kwani ni juhudi zao wenyewe na sasa wanakaribia kushika usukani wa nchi!
Sina jibu lkn ukweli ndiyo huwo!