Hii tahadahri ya uwepo wa mamba baharini imekaaje wakuu?

fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,891
2,367
Nimekutana na tangazo kutoka serikali ya mtaa Vijibwenibikitahadharisha wakazi wa vijibweni wanaopenda kwenda baharini pamoja na wavuvi wanaoenda kuvua samaki kuwa na tahadhari kwani kuna mamba huko.

Sasa nijuavyo mimi mamba anaishi kwenye maji baridi na sio ya chumvi kama ya bahari. Uwepo wake kwa sehemu kama ya Kigamboni ni dhahiri kuwa atakuwa katoka mbali kama sehemu zinapokutana mto Ruvu na bahari au Wami na bahari pamoja na mto Rufiji.

Lakini amewezaje ku-survive baharini au mamba anaweza kuishi maji ya aina zote ya bahari na mito au maziwa.

Kwa anayefahamu au mwenye taarifa zaidi kuhusu hili jambo maana linanipa mashaka sana.
 
fursa kwa watu wa dar, watuletee 'Lake Placid' ya kwanza kabisa Tanzania
umenikumbusha zamani saana hiyo movie ndio nilikuwa nimeanza maisha nimepanga chumba kimoja

ilikuwa kila nikiweka hiyo movie chumba changu kinajaa watoto nyingine ilikuwa inaitwa black water na primeval
 
Nimekutana na tangazo kutoka serikali ya mtaa Vijibwenibikitahadharisha wakazi wa vijibweni wanaopenda kwenda baharini pamoja na wavuvi wanaoenda kuvua samaki kuwa na tahadhari kwani kuna mamba huko.

Sasa nijuavyo mimi mamba anaishi kwenye maji baridi na sio ya chumvi kama ya bahari. Uwepo wake kwa sehemu kama ya Kigamboni ni dhahiri kuwa atakuwa katoka mbali kama sehemu zinapokutana mto Ruvu na bahari au Wami na bahari pamoja na mto Rufiji.

Lakini amewezaje ku-survive baharini au mamba anaweza kuishi maji ya aina zote ya bahari na mito au maziwa.

Kwa anayefahamu au mwenye taarifa zaidi kuhusu hili jambo maana linanipa mashaka sana.
Tusubiri MTU akiliwa tutafanya uamuzi wa kuleta Waganga na wachawi kutoka kanda ya ziwa waje watambike, maana wao wana uelewa mkubwa kuhusu mamba hasa maeneo ya UKEREWE MWANZA.
Mwaka wa uchaguzi huuuuuu. Unaweza ukakutana na FISI, Maeneo ya Kariakooo. Wasukuma tuoneeeni uhuruma khaaaaa
 
Google wanasemaje?

Crocodiles exist both in freshwater and saltwater, whereas alligators prefer freshwater environments
Aisee yan mm nilikua najua croc na alligators ni kitu kimoja tofauti ni majina tuu !! Sasa unanipa Home work aiseee
 
Crocodile, na Alligator, wote huishi katika maji baridi, na wala si maji ya chumvi.
Unaweza kukuta mamba katika sehemu ya mto unapoingia Baharini (delta) na si katika Bahari.
Mamba hawezi kuishi baharini kwa sababu nyingi tu. Moja wapo ni hii :- Mamba kufuatana na maumbile yake, hawezi kuwakwepa mapredators wa baharini samaki waitwao ' Barracuda' ambao ni hatari sana Meno yao ni kama misumari na pia wao huwa katika makundi, hivyo mamba akijiingiza Baharini ataishia kuwa chakula cha Barracuda.
 
Back
Top Bottom