Hii tabia ya wanawake watu wazima kuoga pamoja yaani bafu moja imekaaje?

Wanawake/wasichana wana mengi ya ajabu; mara wapakatane kwenye siti ya daladala, mara ukute wamesimama wanaongea ktk kundi mwenzie kamkumbatia kwa nyuma,nasikia hata nguo za ndani wanaazimana, hivi vitu hukuti kwa male.
 
Kishule shule tumeoga sana!
Ila sasa hivi nope nope!
Inapotokea kuna tatizo siwezi kusita kumwangalia mwanamke mwenzangu akiwa uchi.tena wala sitagundua kuwa hajavaa!
Ila kwa umri huu mtu aaanze tu kuvua nguo aoge mbele Yangu au Mimi mbele yake .mmmmmmh weird!
Just can't !
Ipo nidhamu fulani juu ya miili comes with age nafkr!
 
kawaida tu, mbona vyoo vya kiume vya baa ni ukuta ambao wanaume wote wanakojoa pamoja?:embarrassed:
 
Tunaoga tu sema siku hizii unaweza tamaniwaa na mwanamke mwenzio duniaa imeishaa
 
Watu wazima kuoga pamoja? Mtakuwa mmekutana wapi? Mie nina aibu sana. Siwezi.
 
Kwenye ndoo moja au?

huhuhuuu!

nimekumbuka enzi za mto MARA, wakati tukiogelea huku wanaume, kule unaona wanawake wameajiachia waaah!

tarrrrrrrtiiiibu kabisa unajibana kupiga chaaaaboo! huhuhuuu!
 
Tunaoga tu sema siku hizii unaweza tamaniwaa na mwanamke mwenzio duniaa imeishaa

Na kweli. Kuna article nilwahi soma kuhusu mwanamke anayefanyia wanawake wenzake massage anavyopata shida wakati mwingine..
 
Back
Top Bottom