Hii tabia ya Wanasiasa kujibishana na polisi isiachwe iote mizizi. Alianza Malima, Kigwangalla, Nape, Lissu na sasa Mbowe

Ni vema wanasiasa wakapewa elimu ya kutii Sheria bila Shuruti kwa sababu mabishano kati ya Polisi na wanasiasa sasa yameanza kuzoeleka na hilo si jambo jema.

Huko nyuma tumewahi kuwaona akina Adam Malima, Dkt. Kigwangalla, Nape, Sugu, Lissu, Mdee na Bulaya na sasa ni kiongozi mkuu wa upinzani Mbowe.

Kama Taifa nadhani kura mahali tunakosea, Tujirekebishe!

Maendeleo hayana vyama.
Sio kila kitu polisi anachofanya ni haki. Sio kila amri ya polisi ni haki au ni kisheria. Wao pia hutokea wakavunja sheria.
Na hasa kipindi hiki cha uchaguzi polisi wetu wanaweza kutoa amri zinazokingana na sheria.
 
Wewe unataka kusema kuwa viongozi wakuu wa vyama mbadala ni wadogo kuliko polisi???? Think again! Kulinda usalama siyo kuonea watu na siyo kusema uwongo!!!
 
Back
Top Bottom