Hii tabia ya wamiliki wa mabasi yanayosafiri safari ndefu

Je kwa nini wanapenda kupeleka abiria kwenye hoteli za gharama kubwa sana na ambazo zipo porini kusipopatikana vyakula vya bei nafuu?

Juzi nilisafiri kutoka Morogoro kwenda shinyanga kwa usafiri wa basi ya Abood... baada ya kufika wilaya ya Bahi Dodoma, walishusha abiria kwa ajili ya chakula cha mchana mda wa saa tano na robo ivi.
Kutokana na safari yangu ilikuwa ya dharura na sikuwa na pesa nilipanga njiani nitumie pesa isiyozidi 3000/=
Tuliposhuka pale nilienda kuulizia wali nikaambiwa sahani ni 5000/=
Nikaona niachane nao nikaenda kununua andazi mbili nikatoa 2000 nikijua haizidi buku kwa zote mbili. Nikashangaa naambiwa andazi moja ni 1000 af bayaaa.

Hii tabia sio ya abood pekee ni mabasi karibia yote ya masafa marefu.

Je ni sahihi? Mana niliangalia abiria wengi hawakula na kati ya basi zima hawafiki 10 waliokula pale. Na abiria wanaopanda mabasi haya wengi ni wa kipato cha kawaida. Kwa upande wangu huu ni unyanyasaji wa abiria na wizi wa lazima
Achaga upumbafu unasafirije bila hela?halafu unapanga kula chakula cha elfu 3 bana
 
Hilo ndio jambo la kushangaza hiyo hela elfu tatu aliyosema hata yeye nyumbani kwake mlo mmoja haitoshi ila anataka itumike kwenye safari na itoshe
 
DAWA NI KUSAFIRI NA CHAKULA.BIBI YANGU HATAKI MASIHARA YEYE AKISAFIRI SAFARI NDEFU ANATENGENEZA CHAPATI ZAKE,ANAKAANGA NYAMA NUSU NA CHAI ANAWEKA KWENYE CHUPA.
YEYE HANA HABARI NA HAYO MAANDAZI YA BUKU
huyo ni baharia
 
Je kwa nini wanapenda kupeleka abiria kwenye hoteli za gharama kubwa sana na ambazo zipo porini kusipopatikana vyakula vya bei nafuu?

Juzi nilisafiri kutoka Morogoro kwenda shinyanga kwa usafiri wa basi ya Abood... baada ya kufika wilaya ya Bahi Dodoma, walishusha abiria kwa ajili ya chakula cha mchana mda wa saa tano na robo ivi.
Kutokana na safari yangu ilikuwa ya dharura na sikuwa na pesa nilipanga njiani nitumie pesa isiyozidi 3000/=
Tuliposhuka pale nilienda kuulizia wali nikaambiwa sahani ni 5000/=
Nikaona niachane nao nikaenda kununua andazi mbili nikatoa 2000 nikijua haizidi buku kwa zote mbili. Nikashangaa naambiwa andazi moja ni 1000 af bayaaa.

Hii tabia sio ya abood pekee ni mabasi karibia yote ya masafa marefu.

Je ni sahihi? Mana niliangalia abiria wengi hawakula na kati ya basi zima hawafiki 10 waliokula pale. Na abiria wanaopanda mabasi haya wengi ni wa kipato cha kawaida. Kwa upande wangu huu ni unyanyasaji wa abiria na wizi wa lazima
Sijaelewa Sasa hapo unawatuhumu Abood bus kwa lipi.. je wao ndio wamiliki wa hiyo sehemu ya chakula? maaana shida kumbe ni bei ya chakula njiani ingekuwa kama ni kwa njia ya DAR-ARUSHA ukawatuhumu Kilimanjaro Bus au Dar Express labda ingekuwa sawa kwa kuwa wao ndio pia wamiliki wa hotel mabasi hayo husimama
 
Hawa watu hufikiri wasafiri ni manyama fulani kutoka sayari ya pluto, hayajui bei ya vyakula na ni majinga yakiuziwa chakula chochoye kwa bei yoyote wananunua
Kwani lazima kununua chakula hotelini? Pika ugali nyumbani kwako ule njian, ukiharisha njian usilaumu mtu
 
DAWA NI KUSAFIRI NA CHAKULA.BIBI YANGU HATAKI MASIHARA YEYE AKISAFIRI SAFARI NDEFU ANATENGENEZA CHAPATI ZAKE,ANAKAANGA NYAMA NUSU NA CHAI ANAWEKA KWENYE CHUPA.
YEYE HANA HABARI NA HAYO MAANDAZI YA BUKU
Huyo Bibi ni zaidi ya professor tena nampongeza kwasabb anajua maisha kuliko Sisi wa miaka hii sikuzote kama unasafiri Safar ndefu jitahidi kuandaa chakula chako mwenyewe,hii inasaidia kubana bajeti pia hata kiafya ni vizuri kuwa makini na misosi ya njian
 
wnachofanya si haki ila mamlaka husika zimekaa kimya kuna hotel nyingi zinatoa chakula kwa bei nzuri lakini hawa wenye mahotel kwa sababu wanawapa madereva na makonda chakula bure pamoja na posho wanaamua kuwakamua abiria nyingine ndio maana rushwa kuisha tanzania ni ngumu
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom