Hii tabia ya wabunge wa Chadema kutohudhuria mikutano ya maendeleo ya Rais Magufuli itaisha lini?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,571
Wakati Rais Magufuli alipofanya ziara na mikutano katika mikoa ya Iringa na Morogoro wabunge wote wa kanda hiyo walishiriki kikamilifu.

Miongoni mwao ni Rev Msigwa, Prof J, Suzan Kiwanga, Lijualikali na yule Devotha Minja walihudhuria lakini wabunge wa kaskazini hasa Arusha wamekuwa hawashiriki.

Rais anaongea na wananchi jimboni kwako wewe mbunge haupo maana yake ni nini?!.......hata Nassari anamuiga Lema bila kutafakari kwa kina.
Acheni hii tabia bhana kama vipi mjiuzulu tuchague wawakilishi sahihi!
 
We waache tuu..dawa yao kwenye sanduku la kura come 2020..wala usiumie bila sababu...dawa ipo jikoni.sababu wananchi tunaona.. na kwa sasa maendeleo yanaletwa na serikali ya JPM. After all Mbungeee hatuletei chochote..hana msaada sana sana tunaendelea kumlisha yeye na tumbo lake tuu
 
Ziara za jiwe mara nyingi huwa ni za nia nzuri ya maendeleo. Pindi anapofungua mdomo huanza kana taratibu lakini hatimaye hufikia kilele fulani cha mzuka na crescendo. Hapo ndo huwa anaanza kuharibu ziara yote kwa vijembe, kejeli na matusi ya kisiasa hasa kwa wabunge wa upinzani.

Kwa kweli mbunge akijua kuwa mkuu anakuja anajua kwa hakika kuwa kejeli, vijembe na matusi ya kisiasa yako kwa menu kwa hiyo wanaamua; wacha mzee apige siasa mwenyewe bana akitoka twaendelea!

Mmmmm! Hii dhana nayo inafikirisha!
 
Ubunge ni uwakilishi usisahau hilo!

Ninawadharau sana viongozi wa cdm wanaohudhuria mikutano ya Magufuli. Hiyo inayaitwa kufungua miradi ya maendeleo ni sehemu ya kampeni za ccm na ni sehemu Magufuli anayotumia madaraka yake kuwadhalilisha wapinzani. Uzuri wananchi wa Arusha wameshajua aina ya siasa chafu za Magu wala hawashoboki naye na huwa wanawashangaa viongozi wa cdm wanaohudhuriwa hiyo mikutano ya siasa chafu. Kusanyeni wanaccm kwenye hiyo mikutano na mmeachiwa uwanja wa kuunga mkono siasa chafu za Magu. Wananchi wa Arusha wana maendeleo kabla hata ya huyo magu, na hizo huduma wanazipata kwa hela zao na sio kwa kujinyenyekeza. Mmekwenda mmevaa uniform za ccm ilikuwa ni uzinduzi wa ofisi ya ccm? Watu wa huko vijijini ndio wanamshobokea rais na hizo siasa majitaka. Nawapongeza sana viongozi wa cdm kutokuhudhuria kwenye hizo hafla za siasa nyepesi.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom