Hii tabia ya Simba kulaghai kwa wachezaji wameanza lini?

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,689
2,000
Kuna hili suala limekuwa likitumiwa sana na Simba kwenye kulaghai wachezaji masikini wa Kitanzania.

Wenyewe wanasema "Ukicheza Simba ni sawa na kuwa njia panda ya ULAYA".

Nimemsikia yule beki wa kushoto aliyetoka Mbao FC someone Mlipili akihojiwa. Anasema kuwa amejiunga simba kwa kuwa unajua ni njia panda ya kwenda ULAYA.

Nikacheka na kujiuliza ' Hivi huyu dogo nani amemuaminisha kuwa ukicheza simba ndio una uhakika wa kuja kucheza Ulaya?. Hivi ni kweli ameahindwa kujiuliza yaliyomkuta Mgosi ambaye alijikuta akitupwa kwenye misitu ya DR Congo? Haoni jinsi Mkude anavyoendelea kuzeekea pale, amuoni Zimbwe JR na ubora wake wote hajawahi hata kuitwa Somalia akafanye trial?. Ni nani amemuaminisha kuwa akicheza pale simba kuwa yeye anaweza kufanikiwa kucheza soka la nje. Si watu wengine bali ni viongozi wa simba wanao walaghai hawa wachezaji.

Huwaga najiuliza ni wachezaji wangap ( kushinda Yanga SC) ambao Simba imewalea na kuwakuza mpaka wamefikia ubora wa kupata nafasi nje ya nchi?

Okey! wengi wanasema Samatta amepata nafasi ya kwenda nje kwa sababu ya kucheza simba, ila ukweli halisi ni kwamba kwa kipaji alichonacho Jamaa ni dhahiri asingekaa Bongo hata kama asingechezea simba. Licha ya kuwa pale simba alipita tu kwa nusu msimu.

Kuna jamaa nimemuuliza maswali kadhaa, kwanza "ni mchezaji gani ambayo simba wanajivunia kapitia simba na kupata nafasi nje ya Nchi?"
Akajibu "Samatta."

Nikamuuliza "|akini mbona YANGA amepita mtu kama NONDA"?

Hakuweza kuendelea kujibu kwa hoja, lakini ki uhalisia unajiuliza kwanini simba wanajisifu kutoa wachezaji nje ya nchi ikiwa hawajatoa wachezaji kuizidi Yanga.?

Wapenzi wengi wa simba hawawezi kujibu hili swali kwa ufasaha.

Hii inadhihirisha ni njama za ulaghai za baadha ya viongozi wa simba kuwafanya wachezaji waache kufuata ndoto zao za kutwaa MATAJI na kubaki simba wakiamini ipo siku watacheza ULAYA.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,597
2,000
Nadhani ungetueleza Kwanza ni kwanini Yanga FC hadi sasa hamjawalipa Wachezaji wenu Mishahara yao ya miezi mitatu ( 3 ) kisha ndipo ungehamia kwa Simba SC kidogo tungekuelewa Mkuu. Ila kila nikiangalia kwa jinsi Simba inavyosajili Kisayansi hivi sasa nina wasiwasi huenda Mzizima Derby au Ilala Derby ijayo ( Simba na Yanga ) rekodi mpya ikawekwa ambapo kuna kila dalili kuwa Yanga FC inaweza kufungwa na Simba SC kati ya Goli 8 au 9. Itunze hii post yangu tafadhali kwani nina uhakika kuwa litatokea.
 
ndemesi

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
380
250
Andiko lako limekaa kishabiki zaidi ila kiuhalisia simba ndio timu pekee inayojitahidi kuruhusu wachezaji kwenda kujaribu bahati zao nje ya nchi na wapo waliofanikiwa na wengine wakafeli na kurudi ikilinganishwa na klabu nyingine.Kwa mbali azam anafuata
 
Mbojo

JF-Expert Member
May 31, 2011
1,408
2,000
Jamaa ana matatizo sana huyu.
Hawa ni baadhi waliocheza ulaya.
1. Bobani
2.Okwi
3.Samatta
4.Kapombe. Hao ni baadhi ninao wakumbuka.kuna yule Mnaigeria aliyecheza simba kisha kapaa ulaya. Simba haijatoa nje tena wachezaji kwasababu ya kutocheza mechi za kimataifa.Naiona kesho ya hawa ulaya.
1.zimbwe Jr
2. Mkude
3.Ndemla kama watajituma kwenye mechi za kimataifa.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,597
2,000
Vizuri sana! Wewe ndio nakuhitaji simba imetoa wachezaji wangapi kwenda nje ya Nchi.?

Mbwana Samatta Poppa kumbe alitokea Yanga FC na kwenda Tou Puisant Mazembe? Kuna Mtu mmoja huko nyuma aliniambia kuwa waliwahi kufanya Tafiti moja ya Kisiri juu ya Matahaira wengi ambao wapo mijini na ikagundulika kuwa 99.5% ni Mashabiki / Wapenzi wa Klabu ya Yanga. Mwanzoni nilimkatalia sana ila kupitia huu Upuuzi / Upupu wako sasa ni rasmi nimekubaliana na huo Utafiti.
 
ndemesi

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
380
250
Vizuri sana! Wewe ndio nakuhitaji simba imetoa wachezaji wangapi kwenda nje ya Nchi.?
Mpaka sasa ni samata na okwi ndio waliouzwa na simba kwa timu za nje bila kumsahau kapombe ambae alienda France kabla ya kurudi azam.Waliofanikiwa kuruhusiwa kwenda kujaribu bahati zao na kufeli ni pamoja na Ajibu,Banda,kaseja n.k
 
demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,689
2,000
Mbwana Samatta Poppa kumbe alitokea Yanga FC na kwenda Tou Puisant Mazembe? Kuna Mtu mmoja huko nyuma aliniambia kuwa waliwahi kufanya Tafiti moja ya Kisiri juu ya Matahaira wengi ambao wapo mijini na ikagundulika kuwa 99.5% ni Mashabiki / Wapenzi wa Klabu ya Yanga. Mwanzoni nilimkatalia sana ila kupitia huu Upuuzi / Upupu wako sasa ni rasmi nimekubaliana na huo Utafiti.

Mhh si kwa povu hili....Jamani mkwasa mrudisheni Ajibu.
 
demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,689
2,000
Naomba unijie mchezaji wa kizazi hiki anayefanya vizuri ulaya akitokea Yanga.
Kwa kifupi tu.

Shaban NONDA alipitia Jangwani baada ya kuwa pale kwa zaidi ya msimu. Akawa na muda wake pale MONACO. Sasa amestaafu

Mbwana SAMATTA alipitia matopeni baada ya kuwa pale nusu msimu.

Ila alienda Genk.

Una swali hapo?
 
demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,689
2,000
Mpaka sasa ni samata na okwi ndio waliouzwa na simba kwa timu za nje bila kumsahau kapombe ambae alienda France kabla ya kurudi azam.Waliofanikiwa kuruhusiwa kwenda kujaribu bahati zao na kufeli ni pamoja na Ajibu,Banda,kaseja n.k
Kwanza kabisa kabla sijaanza kukutajia wachezaji wa Yanga waliokwenda nje naomba utambue kuwa Kapombe hakucheza hata game moja Caen kule Ufaransa.

Alienda kwa majaribio tu.
 
demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,689
2,000
Mpaka sasa ni samata na okwi ndio waliouzwa na simba kwa timu za nje bila kumsahau kapombe ambae alienda France kabla ya kurudi azam.Waliofanikiwa kuruhusiwa kwenda kujaribu bahati zao na kufeli ni pamoja na Ajibu,Banda,kaseja n.k
Umesema Mpaka sasa! Ngoja tumuongeze na Boban hapo juu ili wawe 3.

Shaba NONDA - Monaco

Nizar KHALFAN - Philadelphia Union (mls)

Mrisho NGASSA - Free state Stars (SPL)

Kpah SHERMAN - Mpumalanga Black Aces( SPL)

sweetlee

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
4,046
2,000
Kwa kifupi tu.

Shaban NONDA alipitia Jangwani baada ya kuwa pale kwa zaidi ya msimu. Akawa na muda wake pale MONACO. Sasa amestaafu

Mbwana SAMATTA alipitia matopeni baada ya kuwa pale nusu msimu.

Ila alienda Genk.

Una swali hapo?
Utakuwa una matatizo ya kutokuelewa ulichoulizwa. Nataka wa kizazi hiki kama ulivyomtaja samata.
Huyo samata katokea simba si vyura fc.Nataka akitokea vyura fc
 
sweetlee

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
4,046
2,000
Kwa kifupi tu.

Shaban NONDA alipitia Jangwani baada ya kuwa pale kwa zaidi ya msimu. Akawa na muda wake pale MONACO. Sasa amestaafu

Mbwana SAMATTA alipitia matopeni baada ya kuwa pale nusu msimu.

Ila alienda Genk.

Una swali hapo?
Naomba usinitajie Ngassa maana Hana alilofanya huko alipoenda zaidi ya kurudi nyumbani
 
Kipanga boy

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,278
2,000
Mi nakumbuka Simba kutoa mchezaji kucheza nje ilikuwa mwaka 2012 walipoitoa timu yao tanzania kwenda tunisia kucheza mechi za mabingwa afrika.

ila hawajawahi kuuza mchezaji hata wa daraja la nne ulaya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom