Hii tabia ya kukusanyika kuwazunguka watu wanaoongea na maspika itatutokea puani siku moja

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Oct 31, 2017
7,614
16,428
Niko mahali nimekaa mara naona gari limekuja ameshuka mzee mmoja ametoa maspika na makorokoro mengine na kuongea vitu visivyoeleweka. Mara wanyama wanacheza muziki mara ana dawa za kuwazuia wachawi.

Basi Watanzania wamezunguka wanasikiliza. Na hii tabia ipo karibu nchi nzima, watu tunapenda sana umbeaumbea.

Hivi mtu akiwa na nia mbaya akaja kwa gia hii hii akafanya mambo mabaya kama kulipua bomu, si tutakufa kizembe kabisa?

Halafu ifike mahali mtu akitaka kufanya kusanyiko apate kibali kinachoeleza ni nini hasa anataka kukifanya na atuonyeshe hicho kibali na kama anakuja na mambo ya kipuuzi kama ya huyu anayetupigia kelele sasa hivi, wazuliwe, ni usumbufu mkubwa. Pia tutakuja kufa kizembe.
 
dar kila siku kuna washamba wanaingia,mara atie dawa kwenye pepsi,mara sijui nina dawa ya kusafisha meno nk.

mandondocha yamezunguka kibao na anapigwa mtu hapo hapo kila siku.
 
Bora angekua anaongea vitu vya maana, ni upuuzi upuuzi tu.
Upuuzi upuuzi ndio unapendwa.

Kwa sababu hauumizi kichwa na wala hautishi watawala.

Ukianza kuongelea jinsi serikali ilivyoangusha mapato ya exports za kilimo kwa mwaka ulioishia Agosti 2019 kwa asilimia 55, kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania ya Oktoba 2019, kwa kiasi kikubwa kutokana na serikali kuingilia biashara ya korosho, watu wengi wataona habari zako hazina mvuto, lakini pia utaitiwa polisi kwa uchochezi.
 
Niko mahali nimekaa mara naona gari limekuja ameshuka mzee mmoja ametoa maspika na makorokoro mengine na kuongea vitu visivyoeleweka. Mara wanyama wanacheza muziki mara ana dawa za kuwazuia wachawi.

Basi Watanzania wamezunguka wanasikiliza. Na hii tabia ipo karibu nchi nzima, watu tunapenda sana umbeaumbea.

Hivi mtu akiwa na nia mbaya akaja kwa gia hii hii akafanya mambo mabaya kama kulipua bomu, si tutakufa kizembe kabisa?

Halafu ifike mahali mtu akitaka kufanya kusanyiko apate kibali kinachoeleza ni nini hasa anataka kukifanya na atuonyeshe hicho kibali na kama anakuja na mambo ya kipuuzi kama ya huyu anayetupigia kelele sasa hivi, wazuliwe, ni usumbufu mkubwa. Pia tutakuja kufa kizembe.
Milipuko
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom