Hii tabia ya kukinga mafuta kwenye malori ya mafuta barabarani si sawa kabisa

leipzig

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
2,767
1,703
Nimekuwa nikishuhudia watu wakifungua na kukinga mafuta yaliyobaki katika malori ya mafuta,wengine wanafanya kazi vitendo hivyo mbele ya polisi wa usalama.

Kwa uelewa wangu naona sio sawa kwa vile wanasababisha mafuta kumwagika barabarani na pia uwezekano wa kutokea ajali endapo lori litaondoka pasipo kujua.

1481353647552.jpg
 
Wakale wapi?wao wanachuja mafuta ili wasije kukunyang'anya hako smartphone kako.
 
Sio sawa mkuu ila ndiyo washafanya mazoea hawa. Tangu enzi za Nyerere walikuwepo hawa. Waache wajiokotee mkate wao wa kila siku
 
Tukitazama kwa jujuu twaweza ona ni sahihi ili nao wajipatitie riziki zao ila kwa jicho la pili ni hatari sana kwa maisha yao na maisha ya wengine kwakuwa kama itatokea mtu kutupa kipisi cha sigara au ikatokea hitilafu yoyote inayoweza toa cheche za moto inaweza kuteketeza gari nyingi na kupoteza maisha ya watu na haswa ukizingatia foleni katika barabara zetu. Pia hawa ndugu zetu wanapofungua mifuniko ili wakinge mafuta kuna muda huwacha wazi pasi na kifunga jambo ambalo hufanya mafuta yaendelee kumwagika barabarani.
 
Hizo gari ziko empty.na zina automatic shutter valve.
 
inategemea na nchi hapa kwetu sio tatizo kwani ni mungu anatutazamia ajali zetu.
 
Back
Top Bottom