Hii tabia ya Kenyan media kutunga uongo kuhusu Tanzania ikiachwa, kuna siku watatutia vidole machoni!

Jorochere

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
995
2,000
Rais anaua Tanzania ? au kuna Tanzania mbili amabayo siijui ambae Rais anaua.
Umesema ungekuwa mwandishi wa BBC /ALJAZEERA usingeandika chochote kuihusu Tanzania hata kama ni ukweli ndio maana nikakuita mnafiki kwa sababu hujui majukumu ya vyombo vya habar ndio maana huwez hata kuwa mwandishi wa habar wa redio free....! Kuhusu watu kupotea na kuuawa kwenye familia ni nani wa kulaumiwa ........?
 

afnhondya

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
666
1,000
Kwanza ni kama wanatafuta huruma kwa wananchi wao. Na sbb kubwa ni kwamba miradi hii ikikamilika kweli ni Tz ndio tutanufaika ki uchumi zaidi kwa jinsi jiografia yetu na Kenya ilivo kwenda ktk Land locked countries.

Ndio ile vita ya uchumi inapiganwa sasa. Paskali unafikiri Wakenya hawataihoji serikali yao pindi wakiona uchumi wetu unapaa kutishia uchumi wao?

Wanachofanya hapo ni kutengeneza utetezi kabla ya kushitakiwa/kuhojiwa na wananchi wa Kenya.

As long as long hatuchukui chochote kilichochao kwa hila. Tutie PAMBA MASIKIONI VITA YA UCHUMI IENDELEE!!.
 

Wo shi niubi

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
1,067
2,000
Umesema ungekuwa mwandishi wa BBC /ALJAZEERA usingeandika chochote kuihusu Tanzania hata kama ni ukweli ndio maana nikakuita mnafiki kwa sababu hujui majukumu ya vyombo vya habar ndio maana huwez hata kuwa mwandishi wa habar wa redio free....! Kuhusu watu kupotea na kuuawa kwenye familia ni nani wa kulaumiwa ........?

Watu kupotea au mauaji yanayoendelea ni kweli serikali lazima ilaumiwe, na ni lazima ichukue hatua sio kulaumu ya kuwakamata wahusika wotem, point yangu ni kuwa ukiniletea habari kichwa cha habari ''Rais xxx anaua watu wake Tanzania '' ni report siwezi, huo sio uandishi ni upuuzi, na mwandishi mweye akili zake timamu hawezi fanya uandishi ule.
 

interconsult

Senior Member
Dec 8, 2017
114
250
Hakuna walichopika ni uelewa mdogo wa mambo. Wenzetu habar kama hiyo inaandikwa na kuripotiwa na mchumi mbobezi. Jiulize wew ni mbobez ktk maswala ya uchumi. Huyu ripota namjua ni mchum mahiri.wew ji cecemue tu
 

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
1,738
2,000
Huwezi kuilinganisha Kenya na Tz juu ya uhuru wa maoni. Tuwafikie hapo kwanza ndiyo tuanze kulalamika. Ama sivyo kila siku tutalalama kuwa wanatutukana. Sisi huku tumejaa unafiki katika habari na kutwezana ukuu kwenye upumbafu.
Paskali wewe pia unaweza ripoti habari yoyote ile ya Kenya.
 

Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,774
2,000
Hii ni tatizo la muda mrefu, nenda gazeti la TheEastAfrican, habari zote zinazohusu Tz ni za kuichafua zaidi, habari nzuri hazipewi kipaumbele na mbaya zaidi hizi media ya Kenya zina ushirikiano na media za kimataifa, habari itayoandikwa TheEastAfrican, utaikuta BBC na media nyingi kubwa hivyo hivyo.

Solution ni Tz kuwekeza haswa katika media, tuwe na vyombo vikubwa kama Azam media nyingi, serikali ilichukulie hili ni kama suala la usalama wa Taifa, waondoe makodi na changamoto zote ili media industry bongo ikue. Kwa wana usalama wanajua propaganda ni sehemu ya vita, ni lazima tuwe na uwezo wa kufikisha taarifa sahihi na salama kwa nchi yetu Africa na duniani kwa ujumla, hata ka Rwanda kanatushinda kwa propaganda kweli ?

Watanzania bwana!!yaani kuutaarifu umma Wa Kenya yanayofanywa na Tanzania na wanachama wengine Wa EAC imekuwa ni kuchafuliwa??!!!!

Tatizo letu hatupendi kuukubali ukweli,tumezoea kupindishapindisha mambo!!just imagine Mkuu Wa nchi tu anakuwa muongomuongo unategemea mini kwa wananchi wake??!
 

From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
2,085
2,000
Kumbe niwatu waliuza NGO,MBE .hapo nimekuelewa .lakini siyupo alosema wauzwe .au nimahakama iliamuru wauzwe .
Hahahaha Abdallahkova naomba uache kunitafuta maneno. Hahahaha

Figisu zilianza kwenya Bomba la mafuta kutoka Uganda, initially lile Bomba lilikuwa litandazwe Kenya na sio bongo kupitia Tanga.

Figisu zikaenda mpaka kwenye ng'ombe wa Masai kupigwa mnada nchini kwa sababu walilisha ng'ombe wao Tanzania.

Mara pale namanga upande wa Kenya wakasema gesi isiingie kutokea Tanzania.

Mara mahindi ya kutoka Zambia kuingia Kenya yasipite bongo kwa sababu kuna wafanyabiashara wa kibongo sio waaminifu, wanapitisha mahindi ya kibongo kama vile yametoka Zambia.

Mara Rais wetu Magufuli amempokea Raila kiongozi wa upinzani zaidi ya mara mbili nyumbani kwake Chato, ilhali Rais wa Kenya alivyovuka border Namanga hakupokelewa na Rais.

Ni drama tu!!!!! Japo Juzi Rais Magufuli akiwa Uganda alisema yeye na Kenyatta hawana shida na urafiki uko pale pale.
 

kenyamanyori

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
735
500
Mimi naona tofauti na media za Kenya na Tanzania ni kuwa waandishi wa Kenya wana andika news kwa kuzingatia weledi wa media ill hali huku kwetu waandishi wana ripoti matukio.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom