Hii tabia ya Kenyan media kutunga uongo kuhusu Tanzania ikiachwa, kuna siku watatutia vidole machoni!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,291
2,000
Wanabodi,

Sio mara moja au mara mbili, kumekuwa na negative publicity kuhusu Tanzania kwenye media za kwao, mara wamtukane rais wetu, mara watutukane Watanzania, etc, na sisi Watanzania kwa vile ni wapenda Amani, siku zote tunajinyamazia tuu bila kuwajibu, sasa imefikia hatua media za Kenya, zikisoma habari yoyote ya maendeleo kwenye reginal intergration kutokea Tanzania, wataipindua na kuireport negative.

Mfano hai ni wiki iliyopita nimehudhuria mkutano wa UNCTAD uliofanyika Tanzania, ni media za Tanzania tuu ndio zilialikwa.

Magazeti ya Daily News na Citizen, yakaripoti mkutano huo very positively
Story ya Daily News ni hii DRC, Uganda engaged on road user fee
na Story ya the Citizen ni hii New railway projected to reduce transport costs

Media mbili za Kenya zikai pick that story from the Citizen, zikaipika, kuigeuza na kuitungia uongo kwa kuongeza majungu ambayo hayakuzungumzwa popote!.
Angalia hapa kilichoripotiwa Tanzania Locks Out Kenya in New Border Deal
na pia angalia hapa kilichoripotiwa Tanzania omits Kenya from preferential transport deal

Kwa mimi nilikuwepo, hicho kilichoripotiwa na media za Kenya ni uzushi na uongo mtupu!.

Kwa nini Tanzania tunapozushiwa vitu vya uongo kwa lengo la kutuharibia tuu, huwa tunanyamaza tuu bila kujibu?. Hawa Wakenya, tukiendelea kuwanyamazia tuu, utafikia wakati, watatutia vidole machoni!.

Paskali.
Rejea za baadhi ya mambo tuliozushiwa tukanyamaza.
‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"
Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi!
Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu Magufuli kuwa ni Dikteta!
Huku sio kudhalilishwa kwa Rais wetu na Media za Nje? Je, watanzania tukubali, Tukae kimya?
Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!
 

From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
2,085
2,000
Sidhani kama ni ubovu wa media per se, japo najua inawezekana ni mbegu zinazo ota baada ya uhusiano wa Kenya na Tanzania kuwa shaky siku za hivi karibuni.
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,329
2,000
Unataka nani asilinyamazie?

Hapa nchini kwetu tu yanafanyika hayo na uchochezi juu.. wananchi wanashangilia na wao kuandika uongo mitandaoni juu ya utawala..

Sasa unafikiri kweli hawa wakenya hawayaoni hayo? Waambie waweke ya kiudaku udaku hapo paaa wananchi watawanyoosha sana sana..

Nchini hapa badala ya kutumia mitandao kupaishana hata kibiashata n.k.
watu ni kushushana na kuandika uongo.. hao hawana tofauti na wengi hata upinzani kwa uongo.. na wanajua wa TZ ya kihivyo wengi akili walaaaaa hazichangamki
 

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,241
2,000
Mbona sijaona kilichopikwa hapo, wamechagua namna ya kuiripoti tu, ili iwe relevant kwa nchi yao

Mfano mpo kwenye patnership kampuni tatu, A, B na C...mbili kati ya hizo, sema A na B mkakubalina kuanzisha mradi pamoja, mkamuacha C

Sasa wawakilishi wa A na B watairipoti kwa wafanyakazi na wadau wao kuwa kuwa ''kwa pamoja, Kampuni A na B tumekubaliana kushirikiana kwenye miradi kadhaa''

Sasa C kuripoti kwa wafanyakazi na wadau wake atasema, ''Kampuni A na B wameamua kututenga kwenye mradi wao'' na bado wakawa sahihi.. kwa sababu mlikuwa patners mwanzo
 

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,590
2,000
Kwani hizo habari ni za uongo? Au ndio mbinu za fanani kufinkisha ujumbe kwa hadhira bila kumkwaza kiranja mkuu
 

mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
3,815
2,000
Hii ni tatizo la muda mrefu, nenda gazeti la TheEastAfrican, habari zote zinazohusu Tz ni za kuichafua zaidi, habari nzuri hazipewi kipaumbele na mbaya zaidi hizi media ya Kenya zina ushirikiano na media za kimataifa, habari itayoandikwa TheEastAfrican, utaikuta BBC na media nyingi kubwa hivyo hivyo.

Solution ni Tz kuwekeza haswa katika media, tuwe na vyombo vikubwa kama Azam media nyingi, serikali ilichukulie hili ni kama suala la usalama wa Taifa, waondoe makodi na changamoto zote ili media industry bongo ikue. Kwa wana usalama wanajua propaganda ni sehemu ya vita, ni lazima tuwe na uwezo wa kufikisha taarifa sahihi na salama kwa nchi yetu Africa na duniani kwa ujumla, hata ka Rwanda kanatushinda kwa propaganda kweli ?
 

mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
3,815
2,000
Mbona sijaona kilichopikwa hapo, wamechagua namna ya kuiripoti tu, ili iwe relevant kwa nchi yao

Mfano mpo kwenye patnership kampuni tatu, A, B na C...mbili kati ya hizo, sema A na B mkakubalina kuanzisha mradi pamoja, mkamuacha C

Sasa wawakilishi wa A na B watairipoti kwa wafanyakazi na wadau wao kuwa kuwa ''kwa pamoja, Kampuni A na B tumekubaliana kushirikiana kwenye miradi kadhaa''

Sasa C kuripoti kwa wafanyakazi na wadau wake atasema, ''Kampuni A na B wameamua kututenga kwenye mradi wao'' na bado wakawa sahihi.. kwa sababu mlikuwa patners mwanzo

Hayo jamaa ni waongo sana, ngoja nikupe mfano mwepesi tu wa wiki iliyopita, Morogoro kuna wakenya wawili walikamatwa kwa kosa la kujifanya ni mawakala wa TRA, ila magazeti ya Kenya wali igeuza ile habari wakawa wamekamatwa kwa kuwa hawana work permit, unaona sasa huo uchonganishi na unafiki ?
 

MTOCHORO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
4,496
2,000
Lipi la uongo hapo nani hajui Tanzania ni wanafiki toka mtu hadi serekali.
Mbona husemi wanavyoandikaga ukweli kwamba Tanzania ni mazuzu
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,970
2,000
Wanabodi, sio mara moja au mara mbili, kumekuwa na negative publicity kuhusu Tanzania kwenye media za kwao, mara wamtukane rais wetu, mara watutukane Watanzania, etc, na sisi Watanzania kwa vile ni wapenda Amani, siku zote tunajinyamazia tuu bila kuwajibu, sasa imefikia hatua media za Kenya, zikisoma habari yoyote ya maendeleo kwenye reginal intergration kutokea Tanzania, wataipindua na kuireport negative.

Mkuu Pascal, twapaswa tusikie vibaya sana juu ya Wakenya ambao wanatuandika vibaya kwenye media na ku-react kuliko nchi jirani wanaouwa raia wetu?

Labda tukiri kwa ujumla kwamba kuna weakness ambazo nchi jirani wameziona juu ya uongozi wa nchi yetu na hawana heshima tena na taifa letu. Na wanaona sisi wenyewe tumegawanyika hatuheshimiani wala kustahiana tena. Tunatukanana, tunafungana, tunapigana ovyo. So kwa nini iwe issue wao wakitutukana kidogo? Huwezi kusema mambo mazuri juu ya jirani yak0 ambae kila siku ndani ya nyumba yake ni matusi, uonevu, ogomvi, unyanyasaji, ubabe, kuuana, kufungana, nk. Ni ulevi tu wa kisiasa, madaraka na uongozi ndio tumeshupalia. That is how they see us now.

Kumbuka kuheshimiwa ni matokeo ya aina na staili ya uongozi ulionao katika nchi. Enzi za Nyerere unaambiwa nchi kama USA, UK Germany nk walikuwa wanakuwa makini sana kuangalia aina ya balozi waliemteua kuja kuwakilisha nchi zao hapa kwetu, kwa sababu waliwaambia wazi kwamba unaenda kuwa balozi katika nchi ya kiongozi mmoja makini na mwenye busara sana. Siku hizi hata messenger tunanaeletwa kama Balozi wa hizi nchi, na hawaoni tatizo.
 

DrLove69

JF-Expert Member
Jan 20, 2018
3,117
2,000
Wanafiki ni sisi Watanzania ambao kutwa tunainyea na kuivua nguo Tanzania yetu. Wanachofanya hao waandishi wa Kenya ni kunata na biti na kutembelea mrindimo huo huo tunaopiga Watanzania.
Mpaka hapo tutakapoilinda kwa kuienzi na kuiheshimu Mama Tanzania, manyang'au wataendelea kutunyea utosini.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,545
2,000
Unataka nani asilinyamazie?

Hapa nchini kwetu tu yanafanyika hayo na uchochezi juu.. wananchi wanashangilia na wao kuandika uongo mitandaoni juu ya utawala..

Sasa unafikiri kweli hawa wakenya hawayaoni hayo? Waambie waweke ya kiudaku udaku hapo paaa wananchi watawanyoosha sana sana..

Nchini hapa badala ya kutumia mitandao kupaishana hata kibiashata n.k.
watu ni kushushana na kuandika uongo.. hao hawana tofauti na wengi hata upinzani kwa uongo.. na wanajua wa TZ ya kihivyo wengi akili walaaaaa hazichangamki

Watawala wanawafanyia vipi wananchi wanaptofautiana nao mitizamo? Ukishaijua tabia ya watawala kwa wanaowatawala utajua kwanini kuna hii shida.
 

Mcben100

JF-Expert Member
Apr 8, 2013
358
500
Sasa wamechoka kusifiwa ndani wanataka wasifiwe na nje. Serikali ya saiv ipo km mwanamke inataka tu sifa ooh baby we mzur sana, yan umependeza leo. Sasa saiv sifa zinataka kuvuka border. Kwan wasipokusifia unabadilika nin au unapugukiwa na nin.

Fanyeni kazi acheni kutafuta sifa za kulazimisha. Wananchi wakipata maendeleo, uchumi ukiboreka ukitawala kwa kufata katiba na sheria sifa zitakuja zenyewe. Nyie mmeharib mahusiano mazur yaliokuepo afu bado unataka wakusifie, its insane. Unaminya uhuru wakujieleza, juhudi zako umeelekeza kwenye kuua upinzan halali kikatiba, hutak kukosolewa afu unataka watu wasikuite dikteta.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom