Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,860
Kweli sisi watanzania ni wavivu wa kupindukia.Kuna hii tabia ya wanawake wa kitanzania ambayo kwa kiasi fulani inachangiwa na uvivu ukiacha maswala ya usalama wa mhusika.Usalama hapa unatumika tu kama kisingizio cha kuhalalisha hii tabia kwa baadhi ya wanawake.Wapo wachache kama huko vijjini, n.k ambako usalama wakati wa usiku ni mdogo hivyo wanalazimika hata kama hawapendi.
Tabia ninayoiongelea hapa ni ile ya wanawake kujisitiri haja ndogo kwenye makopo wakati wa usiku na kumwagu uchafu huo nyakati za asubuhi.Hakika hii tabia inanikera sana na huwa nashangaa kwanini jambo hili limekuwa ni kama utamaduni wa kawaida kabisa na hata wala haliongelewi!
Tabia hii kwa kiasi fulani inatokana na uvivu tu wa mtu kutoka nje wakati wa usiku kwa kisingizio cha usalama mdogo.Unakuta nyumba ina uzio mzuri tu na gate juu lakini bado kina dada /wanawake hawa wanajisaidia kwenye makopo na kutupa uchafu wao nyakati za asubuhi na ole wako ukutanenao hiyo asubuhi utatamani hata kutapika.
Nimeisha nyumba za kupanga na kushuhudia hali hii na pia nimeshuhudia hali hii nikiwa katika nyumba moja(self contained) ambayo wanafunzi tulipanga tukiwa chuoni.Pamoja na kwamba choo kiko ndani,lakini baadhi ya kina dada walikuwa bado wanaendeleza hii tabia ingawa wakitoka ni warembo huwezi amini!
Nachojiuliza hivi hii tabia iko katika nchi nyingine za dunia hii?Tabia hii mbona inafumbiwa macho kama vile ni jambo sahihi kabisa?Kiafya tabii ni nzuri kweli?Umeshawahi kumsikia bwana afya au bibi afya yoyote akizungumzia tabia hii?Kwanini tunaona hii tabia ni jambo tu la kawaida katika jamii yetu?Hivi mtu huoni kinyaa kujisaidia katika kopo na kulala na uchafu usiku mzima?
Wakati umefika tabia hii ianze kupigwa vita.Huu ni utamaduni wa aibu kwa mtanzania na unapaswa kufika mwisho.
Tabia hii jamani inakera sana muiache!