Hii stori inasikitisha na kuchekesha hapo hapo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii stori inasikitisha na kuchekesha hapo hapo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by i pad3, Apr 18, 2012.

 1. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [h=3]WANUSURIKA KIFO BAADA YA KUFUNGIWA NDANI YA NYUMBA NA KISHA KUCHOMWA MOTO.[/h]


  [​IMG]
  Wanafamilia walionusurika kifo baada ya baada ya kufungiwa ndani ya nyumba na kisha kuchomwa moto, usiku wa saa sita Aprili 14 mwaka huu katika Kitongoji cha Mpakani, Kata ya Nsongwi Mantanji, Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya.
  [​IMG]
  Mashuhuda waliosaidia kuzima na kuiokoa familia iliyonusurika baada ya kufungiwa ndani ya nyumba na kisha kuchomwa moto, usiku wa saa sita Aprili 14 mwaka huu katika Kitongoji cha Mpakani, Kata ya Nsongwi Mantanji, Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya.
  *******
  Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
  Watu 6 wa familia moja wamenusurika kifo baada ya kufungiwa ndani ya nyumba na kisha kuchomwa moto, usiku wa saa sita Aprili 14 mwaka huu katika Kitongoji cha Mpakani, Kata ya Nsongwi Mantanji, Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya.  Sakata hilo limetokea baada ya kijana aitwaye Benard Andeson (25), ambaye ni jirani wa familia hiyo alipokwenda nyumbani katika nyumba hiyo na kufunga kufuli milango ya nyumba hiyo, huku wakiwa wamelala, kisha kuichoma kwa moto na kutokomea kusiko julikana usiku huo.  Walionusurika katika mkasa huo ni pamoja na mama wa familia hiyo Roza Mwanantwale (51), na watoto wake watano Christina Japhet (20), Sakani Jophet (16), Chesco Jopget (14), Onesmo Japhet (11) na Felister Japhet (4).  Wakati wa tukio hilo baba wa familia hakuwepo nyumbani hapo, ambaye anafahamika kwa jina la Bwana Japhet Mwalizi (55), ambaye yupo Nchi ya Malawi akitafuta riziki.  Baada ya kuchoma moto nyumba hiyo Benard pia alifunga milango ya nyumba zote za majirani kwa kufuli, ili wasitoke kutoa msaada lakini alisahau kufunga nyumba moja ya Bwana Rosa Shabani, ambaye alitoka nje na kupiga yowe hivyo baadhi yao walitoka nje na kwenda kutoa msaada.  Wasamalia hao walivunja mlango na kuinusuru familia hiyo na kuokoa baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani katika nyumba hiyo.  Balozi wa shina katika eneo hilo Bwana Rashid William, amesema alisikia sauti katika nyumba hiyo ndipo walipoenda kutoa msaada lakini, lakini ikawa vigumu kuumudu moto huo ulioteketeza kabisa nyumba hiyo, ambapo walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mpakani.  Baada ya kutoa taarifa kwa Mwenyekiti huyo walianza kufanya msako usiku huo huo kumsaka Benard na kufanikiwa kumkamata saa 8 usiku, akijaribu kutoroka kuelekea Iwalanje, umbali wa kilometa 20 kutoka kijijini hapo na kumrejesha.  Mtuhumiwa alikiri kutenda kosa hilo majira ya saa nne usiku, na wananchi hao waliamua kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Uyole, kilichopo mkoani hapa.  Hata hivyo wakazi wa mtaa huo waliamua kuchangishana pesa kwa ajili ya kuisaidia familia hiyo, kuezeka upya nyumba yao ambapo shilingi 167,200 zilipatika papo hapo kwaajili ya kununulia mabati na baadhi yao walijitolea miti na misumari, ili familia hiyo iweze kurudi katika nyumba yao kwani hivi sasa wanapatiwa hifadhi na majirani.  Kabla ya kuchoma moto nyumba hiyo mtuhumiwa Benard alitoa vitisho kwa majirani akiwemo Rosa Shaban, ambapo Aprili 11 mwaka huu, alisema kuwa lazima ale maini yake akimaanisha kuwa atamuua na baadae alienda kwa familia hiyo iliyochomewa nyumba, simu moja baada ya tukio na kutoa vitisho kuwa lazima awatoe duniani.  Sababu ya mtuhumiwa kwenda kutoa vitisho hivyo ni kwa madai kuwa kwanini binti wa familia hiyo Christina Josephat amefanikiwa kuhitimu Kidato cha nne, wakati yeye kashindwa kuhitimu shule.  Wakati huo huo Benard Anderson (25) alishindwa kuendelea na masomo ya kitado cha nne katika Shule ya Sekondari Iwalanje, kutokana na utovu wa nidhamu.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  mmmhh! mazito....
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kweli hapa duniani kuna watu na viatu!
   
 4. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  haswaaa, yaani jamaa kaona kuwa form four ni diiiili .kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo
   
 5. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh kwa kweli huyu kijana ni mbegu mbaya kabisa.
  Anatakiwa apewe adhabu kali sana ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama yake
   
 6. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  i pad3, Sijaona kichekesho ktk story zaidi ya kusikitisha. Ni jinsi gani mtu unachanganyikiwa na maisha na kugeuza roho iwe zaidi ya mnyama.
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Hili sio la kucheka bali kusikitika maana alilolifanya ni jambo la hatari sana
  maana kama ni kifo wangekufa ambao hata hawahusiki kabisa
  Pole sana kwa familia hii
   
 8. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  ha ha ha...very sad kwa familia....siku zao hazikuwa zimepangwa.
  Huyu kijana.....hivi kitu cha arusha(Cannibas Sativa brain charger) kinapatikana mbeya?
   
 9. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  kweli TANZANIA ni nchi ya amani! PATHETIC!
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  wivu wa kimaendeleo huo mdau,stori imeanza na huzun,imeishia kunivunja mbavu
   
 11. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi mwenyewe wakati nasoma nilijua labda mtu kashika na mke wa mwenzake ndio akaamua ateketeze familia. lakini eti kisa kuna mtu kamaliza form four na inawezekana hajafaulu ila kamaliza .WTF????
  NYONGENII HUYU MPUMBAVU HAFAI KUISHI KWENYE JAMII YETU, NYONGELEA MABLI AU AKALIME NA WENZAKE HUKO SEGEREA
   
 12. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huyu kijana atakuwa anatumia masabuli kufikilia kama mkwer*
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  segerea hawalimi,
  aje moro kuna gereza linaitwa MTEGO WA SIMBA, ni ful kilim0
   
 14. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nalijua hili nilishawahi kwenda ku apply uaskari magereza wakaniambia wewe mpumbavu una wani unakuaj huku kufanya nini ondoka hapa , na mkuu wa gereza akanipa mcchongo wa kuja mbele kukamua ..alikua hanijui na wala simjui ni bahati tu.,..kweli pale kuna mfaa huyu mjinga
   
 15. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  i pad3 hapa panahuzunisha na kuchekesha kwa wakati mmoja lakini pia panafunzo ambalo mimi nimeliona na ningependa niwashirikishe wana jf wenzangu.
  a) nimejifunza kuwa wewe ukiwa unafurahia mafanikio yako kuna mwenzako hapendi kuona hata kesho unaiona. hawa wenye wivu wa aina hii hawako huko mby tu bali hata huko ulipo wewe mwana jf. yawezekana kabisa wakawa ni rafiki zako wa karibu ambao kila jion unakaa nao kupata moja baridi moja moto, au unakesha nao kuimba na kusali lakin mioyoni wanakuombea mabaya. Tena wengine ulipofanya sherehe kusherekea kupanda cheo walishiriki tena wakiwa na vihirizi mfukoni kwamba hiyo ofisi ukiingia tu ufe lakin Mungu akasema bado nahitaji huyu anitumikie.

  b)Pia nimeona kama kuna chuki ya ajabu ambayo binadam tunayo nafsin mwetu. Jamani kuna watu wanachuki za wazi ambao kwao wako tayari hata kuona wewe na familia yako mnatoweka hata kama kwao itawagharimu kufungwa au kunyongwa. huyu naye ni mtu hatari lakin hupaswi kumuogopa kama ukwa nia mtu wa sala kulingana na imani yako ila kamwe usimpuuzie. Mtu mwenye chuki huwa kila siku anatamani akumalize ila pia mtu huyu kwasababu ya nia mbaya ya utu wa ndani lazima shetani aliyeko ndani yake atamshawishi aropoke tu, iwe kwa mtu mwingine au kwako mlengwa. Kuna mwandish mmoja aliwah kuandika kuwa " mtu mwenye chuki hawez kujificha kamwe lazima atasema manake nafsi ya kuangamiza mtu asiye na hatia itakuwa ikimsuta" na hata huyu bernad ilimsuta na ndio maana aliwapa alert na ingekuwa wamesoma alama za nyakati wangeweza kuripoti hili.

  c) pia nimejifunza kuwa kosa la mtu mmoja linaweza kuwasababishia wengine matatizo. siyo kwamba binti Christina alikosea kwa kuvumilia hadi kumaliza form iv lakini kwa huyu kijana limekuwa kosa kwake na kwa kosa hilo kataka kuua familia nzima. Jamani hivi hata hofu iliyopotea njia haikuwepo moyoni mwake? hivi ni ujasiri gani alionao huyu kijana. kwakweli ni mkubwa sana, na kama alivyo yeye basi ujue kabisa hata wewe unaweza akaumkosea mtu na akataka kuangamiza wewe na familia yako. sasa kosa la christina hapa hakuna lakin huyu bernard alitafsiri kama kosa. sasa jiulize wewe umeshawah kukosea nani kiukweli halafu hujapatana naye, ilihali hujui anachokiwaza moyoni mwake? jichunguze kweli katika hili.

  kwa kumalizia kwakua binadam tumeumbwa na mioyo iliyofunikwa na funiko nyama hivyo hatuwez kuisoma basi tuwe makin sana katika kuenenda kwetu. tusiwakwaze wenzetu ili kupunguza idadi ya maadui miongoni mwetu. kumbuka maadui wanao jifanya marafiki ni wengi kuliko maadui waukweli.kwahiyo ni bora hawa wakutengeneza ukawapunguza ili ubakiwe na wale usiowajua ambao Mungu anashughulika nao kwa niaba yako.

  a.k.a mother 3G
  CANCELLOR AS USUAL
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hana tofauti na wale wauaji wadogo wa Kimarekani..........................
   
 17. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  oh,sasa wewe ulitaka kuwa kama Mwigamba?kule ulikwenda ryt place in wrong location
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  Hawa ni watu na kandambili


   
 19. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Natabiri hivi:
  Baada ya miaka si mingi Bernard Anderson ataanzisha kanisa na kudai amemshinda pepo mkuu kwa jina la Melikisadeki, pepo aliyemfanya ashindwe kumaliza kidato cha nne, pepo aliyemtuma kuangamiza familia nyingi kwa moto!...Atajifanya amepata experience ya kumshinda pepo huyo hivyo njoo kanisani kwake akumegee ma- Ujuzi.....
   
 20. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Kweli watu tunatoka mbali, yaani una div. I unatafuta nafasi ya kuwa askari magereza? Hivi ule wimbo wa darasa la tatu hukufundishwa weye? When I was a farmer, a farmer, was me....
   
Loading...