Hii sio sheria ni unyanyasaji kwanini wasifanye hivo kwa mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii sio sheria ni unyanyasaji kwanini wasifanye hivo kwa mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MkamaP, May 30, 2010.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Saturday, 29 May 2010 09:17

  Jackline Masinde

  MSICHANA mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, jana aliamiriwa kuvua nguo zilizoonyesha maungu yake ya ndani katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke.

  Amri hiyo ilitolewa na Mwendesha Mashtaka Mrakibu Mwandamizi wa Polisi katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Pandisha Basil, baada ya kukerwa na hatua ya msichana huyo, kuvaa nguo za nusu uchi na ambazo kimsingi, hazipaswi kuvaliwa mahakamani.  Msichana huyo aliyekuwa amevalia mavazi hayo yaliyoshitua idadi kubwa ya watu, alikwenda katika mahakama hiyo, kwa lengo la kutaka kufungua kesi ya madai.

  Hata hivyo mavazi aliyokuwa ameyavalia, yalimlazimisha Pandisha kumwamuru msichana huyo ayavue ili atembee uchi na kushuhudiwa vizuri na watu kama alikuwa anaona fahari kufanya hivyo.

  Msichana huyo, alikuwa amevaliasuruali iliyombana kupita kiasi na 'kitopu' kilichoacha mabega na mgongo wake wazi.

  Lakini pamoja na kuamriwa kuvua nguo zake, msichana huyo hakutii amri mapema, jambo lililomlazimisha Pandisha kutishia kutumia nguvu za kipolisi, ili iwe fundisho kwa watu wengine wanovaa nguo za aina hiyo katika ofisi za serikali.

  Katika tukio hilo, ofisa huyo wa polisi, alishika nguo ya juu ya msichana huyo, akitishia kuwa angemvua kama asingefanya hivyo kwa hiari yake.

  Hata hivyo msichana huyo alimsihi Pandisha asifanye hivyo na kwamba hatarudia kosa la aina hiyo.

  Baadaye ofisa wa polisi alilegeza uzi, hatua iliyotoa fursa kwa msichana huyo kukimbia.


  Baada ya tukio hilo, Mwananchi ilizungumza na ofisa huyo, ambaye alisema sheria zinakataza mavazi kama hayo, kuvaliwa mahakamani.

  "Mtu yeyote anayefika mahakamani ama kufungua kesi au kusikiliza kesi, harusiwi kuvaa nguo za nusu uchi," alisema Pandisha.


  Alisema mahakama hiyo ilikwishatoa tangazo la kuwataka wananchi kuvaa nguo za heshima na kwamba haitawavumilia wale wanaovaa nguo zisizokubalika.
   
 2. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Mafisadi katika serikali ya nguvu mpya ar na kasi mpya ni dhana ya kufikirika they dont exist, they are not there. Go home and sleep! Dont forget to cast your ballot UM mwaka huu! Kura yako ni muhimu sana! Mwambie na jirani yako!
   
 3. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Tatizo kura kwa nani? naamini kura hii ni mhimu tatizo tu ni kwa nani maana hadi saizi naona hakuna option.
   
Loading...