Hii sio sawa, M/kiti CCM kujipigia kampeni huku akiwaziba midomo Vyama pinzani, tafsiri yake ni Nini?

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Wakuu natumai hamjambo!

Kile ambacho mwenye kiti wa CCM Taifa alikifanya Jana huku wapinzani akiwaziba midomo sio fair kabisa!

Hii inatoa tafsiri mbaya Sana, dictatorship government iliyofichwa ndani ya democratic government!

Vyama pinzani hata kufanya mikutano ya mambo yao ya ndani, imekua gumzo, IGP Sirro na jeshi lake wamekuwa mstari wa mbele kukandamiza democracy kwa kisingizio eti MAELEKEZO KUTOKA JUU, huko juu Ni wapi Kama sio kutoka kwa m/kiti CCM Taifa?

Inasikitisha kuona M/kiti CCM Taifa anafurahia na hakemei kuona police wakiangaika na Vyama pinzani, wakiwarunda cell na magerezani, huku kwa upande wake akilindwa na police haohao!

Je, ucha Mungu ndio Huu??

Je, ingekuwa yeye anafanyiwa hivi angejiskiaje??

Hata Maandiko yanatuasa , " Tutoe kibanzi ndani ya macho yetu kabla hatujakosoa uwepo wa vibanzi katika macho ya wengine!
 
Heheh, nafikiri ingependeza awe anazungumzia yaliyopo kwenye hotuba na sio kuzungumza mengine ambayo hayapo

Maana hotuba yake nzuri, ila alivyoanza kuzungumza nje ya hotuba yake yale ya moyoni ni changamoto sana anashindwa kujua lipi la kutamkwa na lipi si la kutamkwa ata jumatatu alipoapisha mawaziri aliteleza kidogo baadhi ya mambo

La mwisho Rais sio lazima kila siku uonekane kwenye Tv jumatatu yeye, jumanne yeye, jana yeye anatakiwa apumzike walau mara moja kwa wiki akionekana sio mbaya na wasaidizi wake muda mwingine wasiende live wawe wanaredord badae watapost
 
Wakuu natumai hamjambo!

Kile ambacho mwenye kiti wa CCM Taifa alikifanya Jana huku wapinzani akiwaziba midomo sio fair kabisa!

Hii inatoa tafsiri mbaya Sana, dictatorship government iliyofichwa ndani ya democratic government!

Vyama pinzani hata kufanya mikutano ya mambo yao ya ndani, imekua gumzo, IGP Sirro na jeshi lake wamekuwa mstari wa mbele kukandamiza democracy kwa kisingizio eti MAELEKEZO KUTOKA JUU, huko juu Ni wapi Kama sio kutoka kwa m/kiti CCM Taifa?

Inasikitisha kuona M/kiti CCM Taifa anafurahia na hakemei kuona police wakiangaika na Vyama pinzani, wakiwarunda cell na magerezani, huku kwa upande wake akilindwa na police haohao!

Je, ucha Mungu ndio Huu??

Je, ingekuwa yeye anafanyiwa hivi angejiskiaje??

Hata Maandiko yanatuasa , " Tutoe kibanzi ndani ya macho yetu kabla hatujakosoa uwepo wa vibanzi katika macho ya wengine!
Unajadili vitu vinavyojulikana?
 
Back
Top Bottom