Hii sio dharau ya muhimili mmoja kwa mwingine ?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Rejea hotuba ya Jk katika maadhimisho ya miaka 50.
Pigia mstari maneno kama haya namnukuu "Vilevile namshukuru Mh. Luhanjo katibu mkuu kiongozi kwa usimamizi na utendaji wake katika kufanikisha sherehe hii" (mwisho nukuu)

Hadi hapo sasa naomba mniulize dharau iko wapi, ni kwamba wote tu-mashahidi kufuatia na matamko ya Bunge lililopita limetoa kauli/tamko kua wale wote wahusika wa Kadhia ya Jairo's scandal waadabishwe ofcz mimi sioni haja ya kuwaorodhesha hapa kwani wote waliotajwa mnawaelewa na asiye waelewa asiwe na haja ya kuendelea kuisoma hii thread yangu kwani hatoelewa mwanzo wala mwisho wa kusudio langu.

Luhanjo ni miongoni mwa waadabishwa, na kama katiba isemavyo kazi kubwa ya Bunge ni kuisimamia serikali.
Sasa iweje msimamizi anaekusimamia anakupa angalizo tenda hiki, acha kile, nawe hutendi ndiyo kwanza unavisifia vile ambavyo msimamizi wako kakwambia sio havifai tu, kakwambie viadabishe! .

Hii sio dharau iliyopevuka? Hii sio dharau iliyotukuka?

Je? Huyu msimamizi hajaliona hili? Kama hajaliona sitakua na imani kama macho anayo! Kabla sijamuuliza MENO! Kwamba akiona ata'respond? Ubavu anao?

Mimi sijui.
 
Duh, ipo kazi !
Jana wakati naangalia tv ,ilikuwa itv na badaye tbc nliona tangazo moja ambalo nimeendelea kulitafakari hadi leo hii sijalielewa.

Hilo tangazo linahusu ofisi ya CAG(mkaguzi mkuu wa serikali)akiwa anaonyesha jinsi anavyoaminiwa na mashirika na taasisi mbalimbali hasa za nje.

Inaweza ikawa ni tafsiri yangu mbaya tu lakini nilihisi kama vile Bunge ndiye mlengwa wa tangazo lile.kwamba kwanini lihoji utendaji wa cag kwa sifa zile.
Anyway ninaweza kuwa si sahihi lakini coincedence hiyo du !na kama ni kweli basi ipo kazi !!!!!
 
Hivi "Mwenye Mamlaka" alipewa siku ngapi awe amemwajibisha Luhanjo?
 
kawezi kumwadabisha luhanjo.kwani hata yeye ajiamini kama ni safi au salama.
:A S 465:
 
Duh, ipo kazi !
Jana wakati naangalia tv ,ilikuwa itv na badaye tbc nliona tangazo moja ambalo nimeendelea kulitafakari hadi leo hii sijalielewa.

Hilo tangazo linahusu ofisi ya CAG(mkaguzi mkuu wa serikali)akiwa anaonyesha jinsi anavyoaminiwa na mashirika na taasisi mbalimbali hasa za nje.

Inaweza ikawa ni tafsiri yangu mbaya tu lakini nilihisi kama vile Bunge ndiye mlengwa wa tangazo lile.kwamba kwanini lihoji utendaji wa cag kwa sifa zile.
Anyway ninaweza kuwa si sahihi lakini coincedence hiyo du !na kama ni kweli basi ipo kazi !!!!!

Nitajaribu kulifatilia tangazo hilo kwakua kanuni 1 ya matangazo ni marudio.
 
Back
Top Bottom