Hii sio aina ya maisha niliotaka kuishi, sikutamani kupata mtoto kabla ya ndoa

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,456
17,212
Hii sio aina ya maisha niliotamani kuishi, sikutamani kua na mtoto kabla ya ndoa.

Ni hivi kuna binti nimempa ujauzito, imetokea kwa bahati akashika ujauzito, simpendi maana yake ni kwamba sitamuoa na yeye anajua simpendi na hatukua na mipango ya kuoana ila kapata ujauzito wangu.

Sitamani mwanangu kuja kulelewa na mama au baba mwingine au wajomba wakati baba yake nipo, tumefikiria kuitoa lakini bado sijaafiki kaniomba kama najua sitamuoa basi nimruhusu aitoe.

Binafsi sitaki kushiriki kuua ingawa pia siko tayari kumuoa huyu mrembo,s itaki kua na mtoto kabla ya kuoa, kwa kweli niko njia panda. Sina sababu ya kutokumuoa maana anakidhi vigezo vyangu vyote.

Lakini simpendi na nimejitahidi kutaka kumpenda hisia haziji ila hapa nawaza bora tu nimruhusu aitoe ingawa yeye pia yuko tayari kuzaa hata kama sitamuoa tatizo liko kwangu sikutamani kupata mtoto kabla ya kuoa.

Mawazo yenu tafadhali
 
Samahani sana naomba nitumie neno baya kuwa wewe ni mpuuzi, huwezi kulala na mtu hadi mtiane Mimba halafu sasa hivi uje useme humpendi. Je uko tayari siku moja binti yako naye aje afanyiwe ujinga kama huo?

Keyword.uko tayari kutenda kosa jingine zaidi? Ningekuwa mimi ningemuoa na kumpenda zaidi na ungeona wingi wa baraka toka kwa Mungu baba. Tafadhali chukua ushauri wangu, muoe huyo binti and you will one-day remember me
 
Aisee...anakidhi vigezo vyako vyote halafu humpendi?! Kama humpendi kuna kitu hana hawezi kuwa na vigezo vyako vyote then usimpende.

Mapenzi ni hisia mkuu, kama huna hisia nae huwezi kumpenda, unaweza kufake kua unampenda wakati wa kumtongoza ili kumpata ila ukweli unabaki moyoni mwako kama kweli unampenda au la
 
mambo mengine bana....!!,haya mwambie tu akiuwe hicho kiumbe,kama ni mtoto utapata kwa umpendae
 
The Unknown

Hayo ndio madhara ya kumtongoza mtu kisa nyege za barehe zimekuongoza tu ...ila hauna upendo wa nia ya dhati.
sasa wewe mpaka unawaza kuua kiumbe kisicho na hatia ,

hakika ukithubutu kukiua damu yake itakulilia mpaka mwisho wa dahali.
Unajifanya una visheria eti sitaki kuzaa kabla ya ndoa kwani ukizaa kabla ya hapo unazaa paka? acheni mawazo mgando hayo enyi vjiana wa kileo.
 
Last edited by a moderator:
wavulana wa siku hizi bwana ni shidaaaa! na mabint wamekuwa cheep sana siku hizi utazinije na mtu ambaye hana future na wewe?????????? very sad
 
Hayo ndio madhara ya kumtongoza mtu kisa nyege za barehe zimekuongoza tu ...ila hauna upendo wa nia ya dhati.
sasa wewe mpaka unawaza kuua kiumbe kisicho na hatia , hakika ukithubutu kukiua damu yake itakulilia mpaka mwisho wa dahali.
Unajifanya una visheria eti sitaki kuzaa kabla ya ndoa kwani ukizaa kabla ya hapo unazaa paka? acheni mawazo mgando hayo enyi vjiana wa kileo.

Wewe nani alikudanganya kwamba kila anaetongozwa amependwa,upendo ni jambo lingine na kutongoza ni jambo lingine havihusiani kabisa.
 
wavulana wa siku hizi bwana ni shidaaaa! na mabint wamekuwa cheep sana siku hizi utazinije na mtu ambaye hana future na wewe?????????? very sad

Siku zote maisha yako hivi maana hata huko kabla mabinti walipata mimba bado hawajaolewa kwa hiyo hakuna cha ucheap wa mabinti wa siju hizi,always maisha yamekua hayo.
 
Hayo ndio madhara ya kumtongoza mtu kisa nyege za barehe zimekuongoza tu ...ila hauna upendo wa nia ya dhati.
sasa wewe mpaka unawaza kuua kiumbe kisicho na hatia , hakika ukithubutu kukiua damu yake itakulilia mpaka mwisho wa dahali.
Unajifanya una visheria eti sitaki kuzaa kabla ya ndoa kwani ukizaa kabla ya hapo unazaa paka? acheni mawazo mgando hayo enyi vjiana wa kileo.

Sio siri mkuu mijitu inayojidai haipendi kuzaa nje ya ndoa ilihali wanaendekeza uzinzi sana inanichefua sana... Mtu unajua kwa sheria za dini uzinzi unakatazwa ila watu bado tu
 
Samahani sana naomba nitumie neno baya kuwa wewe ni mpuuzi, huwezi kulala na mtu hadi mtiane Mimba halafu sasa hivi uje useme humpendi. Je uko tayari siku moja binti yako naye aje afanyiwe ujinga kama huo?

Keyword.uko tayari kutenda kosa jingine zaidi? Ningekuwa mimi ningemuoa na kumpenda zaidi na ungeona wingi wa baraka toka kwa Mungu baba. Tafadhali chukua ushauri wangu, muoe huyo binti and you will one-day remember me

Naungana na ww,inakuaje unalala na mtu ambaye hujampenda.Mistake huwa zinatokea hatukatai lakn sio hii.Maybe angesema wameshndwana tabia hapo sawa alafu mtu usiyempenda alafu unafanya nae bila kutumia kinga me siyapata ona
 
kwa maelezo yako unacho taka mimi sikielewi .. Unataka mimba ipotee kimiujiza .. Wewe ushatoa boko, hamna kukimbia ukweli .. Chagua umuoe huyo binti au mtoto Wako alelewe na Baba/mama mwingine au uitoe iyo mimba ..

Hapo hamna njia zaidi ya hizo.. Face the fact usiwape shida watu wa kukupa ushauri .. Me nakushauri lea mwanao usiitoe iyo mimba na wala usiingie kwenye ndoa na mwanamke usiemependa ..
 
Jamani jaman Mama aliniambia MTU akitoa mimba watoto watakaofuata watakuwa na shida shida hivi yaani yule marehem atakuwa anawasumbua wenzake maana ata kuwa na wivu kuwa wale ndo watoto yy si mtoto ndo maana hakustahili kuishi..

. Lakin pia yule mtoto mimba hupata MAUMIVU makali km ni MTU wa kawaida angeweza kuzimia Mara 9... Nakuomba sana mleeni huyo mtoto dhambi ya kuua ni dhambi Kubwa hasa kwa kiumbe kisicho na hatia. Pia km MNA hamu ya kuua njoni mniue
 
Kama anajimudu kiuchumi hapo hamba tatizo acha azae tu then umsaidie kulea mtt lkn km hana uwezo wa kuchumi basi muoe tu for sake of ur child coz mtt maisha atakayoishi mwanao yatakuwa magumu sana ambayo obvious hayatakufurahisha
 
We naeeee!
Ulipokuwa unafungua zipu hukujua kinachoyoka huwa kinatungisha mimba?
Mxxxxxxxxiou
eti sikutaka kuzaa kabla ya kuoa,kwanini udichukue tahadhari ,kuu kabisa ikiwa ni kutokudinda kila ukiona sketi?
Eti simpendi,ulimtongoza ili akusogezee siku mfyuuuuuu!
Oh sitaki kuua,zaa sasa!
Na wasichana mmezidi uboya!mnawabuliaje nguo hizi kurumbizi unajua kabisa hupendwi,jana future nawe,unakipeleka tu unachanua tano ya kirumi matokeo yake ndo hayo!
Azae huyo mtoto kwa manufaa yake!ya afya na maisha!
We nenda utafute umpemdaye!
Utampata tu,mambo ya kuoana out of pity ndo kilasiku kesi humu!
 
Back
Top Bottom