Hii sinema ya mlolongo wa chaguzi ndogo za kutengenezwa hata makada asilia wa CCM hawazipendi

Nsimbi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
1,091
1,202
Ukweli ni kwamba hii sinema ya mlolongo wa chaguzi ndogo za kutengenezwa hata makada asilia wa CCM hawazipendi.

Kamtindo haka kanakula pesa nyingi za umma lakini hatujaona Magufuli akitoa tamko lolote la maana.

Kurudia uchaguzi wa udiwani ana ubunge bila sababu za msingi ni ufujaji mwingine. Hii ni aina mpya ya ufisadi.

Magufuli anajitapa sana kuwa yeye amebana mianya ya ufisadi. Anadai pesa nyingi ilikuwa inaliwa kupitia safari za nje, semina na makongamano yasiyo na tija.

Watanzania wanamshangaa Magufuli kunyamazia upuuzi wa chaguzi ndogo. Ingekuwa JK kafanya hivi watu wangesema msanii huyo...

Rais katia pamba masikioni. Ameonekana mkali kwenye mambo mengine yanayofuja pesa lakini hili la chaguzi 'hewa' Rais amekuwa kama simba aliyelowa maji. Why? Double standard?

Sio siri hili suala la chaguzi ndogo ambapo mpinzani anahamia CCM na kupitishwa kugombea tena ubunge uleule, linawachefua wengi.

Inawezekana JPM ameziba baadhi ya mianya ya wizi Serikalini lakini kwa sasa ni kama na yeye amefungua mlango mpya kupitia ufisadi wa chaguzi ndogo.

Ni kweli demokrasia ina gharama lakini gharama zozote za kipuuzi lazima ziepukwe.

Hakika kwa sasa CCM inapitia wakati mgumu sana. Mambo yanaendeshwa kienyeji na kishamba sana.

Viongozi waliopita kama Mkapa wasingeruhusu ujinga unaoendelea sasa.
 
Back
Top Bottom