Hii si sawa hata kidogo kwa wafanyakazi Migodini

Imurumunyungu

Senior Member
Nov 27, 2011
108
17
Jamani wanaJF ni kwamba biashara yote ya dhahabu inafanyika kwa sarafu ya US DOLLAR.Maexpert wote wanalipwa kwa US D lakini wazawa ambao ni watanzania wanalipa kwa thamani ya TZ SHILLINGs ila mameneja woote wa kibongo wao wanalipwa kwa US D.Hili ni tatizo la wafanyakazi,wawekezaji au Serikali yetu.Tufanyaje sasa ili kutatua hili tatizo au uonevu huu?.
 
Uonevu kwa wafanyakazi wa kibongo wanaolipwa kwa shilingi au kwa mameneja wanaolipwa US dollar? Na wewe ulipenda ulipwe dola au unawaonea huruma hao wanaolipwa dola, sijakusoma mkuu, fafanua tuchangie vyema.

Ila nadhani lengo lako ni kusema kila money transaction ifanyike kwa shilingi sio?
 
wafanya kazi wote pasiwepo na tabaka wote walipwe kwa US DOLLAR na cyo shilingi kama ilivyo sasa hivi.Transaction itafanywa na mabenki yetu kuendana na thamani halisi ya US D.
 
Kama wanauza interms of dollar kwa nini wanawalipa in tshs?
Unless kama wanatumia equivalence ya existing exchange rate!
 
We endelea kupokea hizo hela za madafu,hakuna wa kukutetea hapa. kama tu MLIMANI CITY tunanunua kwa dolllar lakini mishahara yetu ni kwa shilingi unadhani hii inamaanisha nini? Wanataka uendelee kupoke hizo chenji chenji ili wakutumie ipasavyo kwa mda mrefu kabwa mapafu hayajakumaliza.......Maana **** majamaa yanafanya kazi ngumu kule BULYANHULU dah! Mtu anaenda UNDERGROUND mbali wa kutoka Mianzini hadi sakina(kwa wa kazi wa ARUSHA ) au Magomeni hadi Karakoo(DSM) au Mabatini hadi Makoroboi(MWANZA) malipo sasa dah! ndiyo maana Miners wengi wa Tanzania wanategemea sana fedha za NSSF kuliko mishahara.
IMAGINE: Mtu unaenda kazini saa 12:00 unatoka saa 12:00 unafanya kazi kwenye Vumbi unalipwa Tsh 800,000/= .
Kunasehemu wanaita 4700,4430,3980(BULYANHULU) dah! niliwahi kuishiwa nguvu dah kidogo ni danje, nikawaambia kama hii ndiyo kazi acheni niende kulima michembe kwetu dah! hadi unaona shule haina maana................Komaeni tu wa Tanzania
 
Kinachotakiwa hapa ni kwamba malipo halisi kuendana na thamani ya dollar.Siyo wanavyolipa sasa hivi yaani USD Moja kwa TSH 1000/=.Huu ni ufisadi wa hali ya juu saana unaofanywa na hawa wawekezaji.
 
Jamani wanaJF ni kwamba biashara yote ya dhahabu inafanyika kwa sarafu ya US DOLLAR.Maexpert wote wanalipwa kwa US D lakini wazawa ambao ni watanzania wanalipa kwa thamani ya TZ SHILLINGs ila mameneja woote wa kibongo wao wanalipwa kwa US D.Hili ni tatizo la wafanyakazi,wawekezaji au Serikali yetu.Tufanyaje sasa ili kutatua hili tatizo au uonevu huu?.

Acha muoze tu mapafu maana ma miners huwa manajidai sana na mko kushoto sana na siasa na huwa hata kura hampigagi nyie.
 
Vijana wa migodn hamtaki kupiga kura mko bize,kufeni tu na silikosis ili watoto wenu ndo wapate akiri
 
Back
Top Bottom