Hii si mara ya kwanza Job Ndugai kumtoa nje ya bunge John Mnyika

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Tarehe 19 Juni 2012, John Mnyika akiwa mbunge wa Ubungo (CHADEMA), alitolewa Bungeni kufuatia kauli yake kuwa RAIS KIKWETE NI DHAIFU.

Alipotakiwa kufuta kauli hiyo kwa mujibu wa kanuni ya Bunge ibara ya 73 (2) John Mnyika alikataa; na ndipo Job Ndugai, wakati huo akiwa Naibu Spika akaamua maaskari wamtoe nje.

Na hapo jana, Spika Job Ndugai aliamuru maaskari wa Bunge wamtoe John Mnyika nje ya Bunge kwa kukaidi amri ya kukaa kimya wakati mbunge mwenzie anachangia.

(PICHANI : Maaskari wa Bunge wakimtoa John Mnyika nje ya viwanja vya Bunge tarehe 19 Juni 2012)-Kwa hisani ya Dar 24.

Fukuza watetezi wote wa wezi. Aibu yao wapinzani
Kwani Acacia waliletwa na wapinzani, mikataba muingie nyie miswada mpitishe nyie kwa kura za Ndiooooo hasara eti muwatupie wapinzani, safi sana Lissu kwa kusituka, kawarudishia mpira mhangaike nao.

Lissu aliwaonya tangu mwanzo hii mikataba ni ya kinyonyaji hamkusikia hizi ndizo consequences zake mnaanza kulialia eti mnaibiwa shenzi kabisa.
 
Mkuu;
Hivi hapa, mtetezi wa mwizi ni nani?? Yaani unajiona kuwa una akili nyingi sana. Wezi uwalete wenyewe, uwape ufunguo wa kukuibia, halafu ukakamate vijiko vile vyakula useme huvioni vinavyo liwa. Akija jirani kukuambia ulichoshika sio chakula bali vijiko vyenye mabaki tu ya vyakula useme anamtetea mwizi?? Kamateni basi hizo dhahabu kwanza sio mabaki
 
Mnyika na Tundu wamefundishwa na Mbowe kula hela za lowassa sasa wamenogwa, wanapita huku na huko kuomba wazungu wawalipe ili kupitisha maslahi yao.
Aise lissu ndiye kawaleta acacia hapa tz au syo

Ova
 
Tarehe 19 Juni 2012, John Mnyika akiwa mbunge wa Ubungo (CHADEMA), alitolewa Bungeni kufuatia kauli yake kuwa RAIS KIKWETE NI DHAIFU.

Alipotakiwa kufuta kauli hiyo kwa mujibu wa kanuni ya Bunge ibara ya 73 (2) John Mnyika alikataa; na ndipo Job Ndugai, wakati huo akiwa Naibu Spika akaamua maaskari wamtoe nje.

Na hapo jana, Spika Job Ndugai aliamuru maaskari wa Bunge wamtoe John Mnyika nje ya Bunge kwa kukaidi amri ya kukaa kimya wakati mbunge mwenzie anachangia.

(PICHANI : Maaskari wa Bunge wakimtoa John Mnyika nje ya viwanja vya Bunge tarehe 19 Juni 2012)-Kwa hisani ya Dar 24.

Kawa kibonge.
 
Mnyika na Tundu wamefundishwa na Mbowe kula hela za lowassa sasa wamenogwa, wanapita huku na huko kuomba wazungu wawalipe ili kupitisha maslahi yao.
Kama wapiga debe wa serikali ni dizaini yako tutegemee kuibiwa Madini hadi masihi arudi.
 
Kwani Acacia waliletwa na wapinzani, mikataba muingie nyie miswada mpitishe nyie kwa kura za Ndiooooo hasara eti muwatupie wapinzani, safi sana Lissu kwa kusituka, kawarudishia mpira mhangaike nao.

Lissu aliwaonya tangu mwanzo hii mikataba ni ya kinyonyaji hamkusikia hizi ndizo consequences zake mnaanza kulialia eti mnaibiwa shenzi kabisa.
Aliyewaleta kashtukia mchezo wa kukiuka mkataba, wapinzani wanatetea ukiukaji
 
Mnyika na Tundu wamefundishwa na Mbowe kula hela za lowassa sasa wamenogwa, wanapita huku na huko kuomba wazungu wawalipe ili kupitisha maslahi yao.
Muwe na aibu hata kidogo, hayo muyafanyayo ni sawa na kutembea utupu mbele ya watoto.
Sasa hivi hata mtoto wa darasa la saba anajua ujambazi wa ccm katika nchi hii
 
Mkuu;
Hivi hapa, mtetezi wa mwizi ni nani?? Yaani unajiona kuwa una akili nyingi sana. Wezi uwalete wenyewe, uwape ufunguo wa kukuibia, halafu ukakamate vijiko vile vyakula useme huvioni vinavyo liwa. Akija jirani kukuambia ulichoshika sio chakula bali vijiko vyenye mabaki tu ya vyakula useme anamtetea mwizi?? Kamateni basi hizo dhahabu kwanza sio mabaki
Hoja hapa ni kukiuka mkataba. Habari ya vijiko haihusiani. Haiongelewi kiasi cha mrabaha bali uongo kwenye mkataba uliokuwa declared.
 
Kama umenisoma vizuri ni kuwa, tumuombe Mola wetu, kuonekane kakosa kadogo tu ka kushikia tuwafurumushe bila hata huruma
 
Back
Top Bottom