Hii si ajabu kuruhusu mikusanyiko ya ibada na kuzuia watu kuwazika wapendwa wao!, Hawajui kuwa mazishi pia ni ibada? RIP Fili Karashani, tumekuzika!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,571
Wanabodi,

Niko mitaa ya Kinondoni Makaburini, nimekuja kumzika Nguli Mzee Fili Karashani, ila wakati mwili wanazikwa kule kaburini, wengi wetu tunazikia huku umekaa viti vya juu hapa Break Point, sio kwa kupenda, bali tumelazimika...

Tangu kuanza kwa hili janga la Corona, leo nimekutana na tukio la ajabu hapa Makaburini Kinondoni!.

Nilidhani ile amri ya kuzikwa na watu 10 tuu ni kwa wale marehemu waliokufa kwa nanii!, na wale wanaozikwa na serikali huku wapimaji wamevalia PPE, kumbe I was wrong!.

Leo tasnia ya habari tumemzika mmoja wa ma Legend wa Habari nchini Tanzania, Mzee Fili Karashani, ambaye amekufa kifo cha kawaida, tumeaga mwili kwa misa na heshima za mwisho nyumbani, tukaja Kinondoni Makaburini kumsindikiza katika makao yake ya milele.

Kufika Makaburini Kinondoni, tunashangaa kuambiwa mwisho watu 20!. Ndugu 10 na wazikaji 10!.

Naomba kuuliza, let's be honest, hii sio ajabu kweli, kama serikali yetu imeruhusu mikusanyiko ya kwenye nyumba za ibada, bado tunatumia public transport, iweje, wanazuia mikusanyiko kwenye mazishi na kuzua watu kuwazika wapendwa wao ambao hawajafa Kwa Corona?. Hawajui kuwa hata mazishi ni ibada?.

Kiukweli kuna vitu vya kijinga jinga tunafanya ambavyo havina logic kabisa!, na ni vitu kama hivi ndio tunachompendea rais Magufuli, ni scientist, hataki ujinga ujinga, anataka logic itumike, tena asinge kemea kwa nini Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda azikwe Mtwara kwa lazima, wakati kwao ni Moshi, mpaka leo watu wangekuwa wanazikwa na serikali, usiku usiku!. Nyie Watendaji wa serikali, yaani kila kitu ni mpaka rais aingilie?, hamuwezi kutumia tuu logic na kujiongeza nyie wenyewe kuwa serikali iliposema mazishi yatahudhuriwa na watu 10 ni vile vifo vya nanii tuu?, hii ya kuzuia watu hata vifo vya kawaida ni kutisha tuu watu, sio kila anayekufa kipindi hiki cha nanii, ni nanii!.

Hata hivyo, kama mtu ulidhamiria kumzika mpendwa wako, na ukafika makaburini, ukazuiliwa kukuzika, unakuwa umetimiza wajibu wako na ibada yako, umezika!.

RIP Nguli wa Habari, Mzee Fili Karashani, Tumekuzika!.

Paskali
 
Kwahiyo unataka kujifanya haujui kuwa issue ya ibada imetumika kisiasa toka janga hili lianze? Corona ilipoingia tu, watu walikuwa wanapiga mahesabu ya kampeni tayari na wala siyo eti kukabiliana nayo...Maghufuli uzuri ama ubaya wake, anawafahamu watanzania haswa na anajuwa kucheza na akili zetu.
 
Paschal...
Kwenye maziko kuna hatari zaidi.
Sent using iphone pro max
What are the differences za mikusanyiko ya ibada na mikusanyiko ya mazishi?!. Mazishi pia ni ibada!.
Hii ingekuwa na logic kama tungezuia mikusanyiko ya ibada!.

Huku ndiko kutishana kwenyewe rais Magufuli anakokataa, sio kila anayekufa amekufa kwa Corona, kwanini azikwe kikorona Corona?.
P
 
What are the differences za mikusanyiko ya ibada na mikusanyiko ya mazishi?!. Mazishi pia ni ibada!.
Hii ingekuwa na logic kama tungezuia mikusanyiko ya ibada!.
Huku ndiko kutishana kwenyewe rais Magufuli anakokataa, sio kila anayekufa amekufa kwa Corona, kwanini azikwe kikorona Corona?.
P
Subiri uone watakavyompigia kampeni kwa kulinda ugali wao, labda itokee maambukizi yazidi na vifo.
 
Back
Top Bottom