Hii sheri kandamizi ya kikoloni ya kuweka watu wasio na hatia ndani masaa 24 ndiyo inayo fanya wakuu wa mikoa na wilaya wajione miungu ,iondolewe.

kichongeochuma

JF-Expert Member
Jan 21, 2024
519
997
Hii sheria ni ya kipuuzi kabisa ndiyo inayo fanya hawa wakuu wa mikoa wajione wanaweza kufanya lolote kwa mtu yeyote wakati wowote, naamini endapo bunge letu lingekuwa ni bunge kweli la wananchi huo ujinga ungefutuliwa mbali

Hii inamfanya mkuu wa mkoa ajione yeye ni mungu maana anaweza fanya lolote akiamini ananguvu ya kukuweka ndani bila kuulizwa , ni sheria ya kinyanyasaji sana hii.
 
😂😂😂😂Rules are rules!Without rules,we are all savages.Ni vema sheria ziwepo ili kuheshimiana bila kuumizana.Ni busara tu itamalaki malangoni mwa hao waitumiayo sheria hiyo.
 
Ni sheria ya kipuuzi tuu, mbona wapo viongozi ambao hawana mamlaka ya kutumia sheria hiyo lakini wanaheshimika vizuri sana na mamlaka zao zinaheshimika , tuondoe kwanza mawazo ya kikoloni vichwani kuamini kwamba vyombo vya ulinzi ndio njia ya uongozi.

Ukitenda haki huna haja wa kutumia sheria kandamizi, hawa wakuu wa mikoa na wilaya huwa ni wapuuzi sana na hasa ukikutana na wale wenye vichwa kama cha makonda

R.I.P mkulima MWAMWINDI uliukataa ujinga wa mkuu wa mkoa IRINGA DR. KLERUU miaka hiyo ukamtandika risasi hapo hapo baada ya kuleta ubabe kwenye maisha yako binafsi.
 
Hakuna sheria ya kipuuzi ila kuna watumiaji wa sheria hizo ndiyo wapuuzi.Chunguza kwa umakini utaona.Bonafide claim of right!
 
Kwani hii sheria inafanya mkuu wa Wilaya amuweke mtu yeyote ndani?

Si mpaka uyakoroge? Ukiyatimba yanakutimba
Hapana inavyo tumika sasa sivyo ilivyo kuwa inatakiwa itumike ,kwa sasa ilivyo na hawa wakuu wetu wa mikoa walio kosa weledi anaweza kukuweka ndani hata mkiwa na visa binafsi vya wanawake huko bar.
 
Hakuna sheria ya kipuuzi ila kuna watumiaji wa sheria hizo ndiyo wapuuzi.Chunguza kwa umakini utaona.Bonafide claim of right!
Mkuu wa mkoa au wilaya anaweza kukutukana matusi ya nguoni na uki react unawekwa ndani tena zaid ya masaa 24unaweza wekwa hata wiki ,hili nina ushahidi nalo.
 
Kuwekwa ndani siyo shida.Kwa nini kiongozi akutukane mbele ya kadamnasi?Amekosa sifa ya uongozi,hekima,busara,staha na amejaa uhayawani.Mlevi wa madaraka huyo.Watakuja kupigwa makofi na vichaa kama mimi wanipige risasi nife hadi nifariki.
 
Hapana inavyo tumika sasa sivyo ilivyo kuwa inatakiwa itumike ,kwa sasa ilivyo na hawa wakuu wetu wa mikoa walio kosa weledi anaweza kukuweka ndani hata mkiwa na visa binafsi vya wanawake huko bar.
Hivi,unajua hata Mtendaji wa kijiji/mtaa/kata ana mamlaka ya kuitumia hiyo sheria?Una-go kabatini 24 hours halafu anakutoa.Ikimpendeza una-go kabatini tena kufungiwa.😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom