Hii serikali ya kikwete vipi?

GINHU

Member
Feb 7, 2011
68
14
Jana nilisikitishwa na kauli ya Naibu katibu mkuu wa Wizara ya nishati na madini alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari ktk kongamano la wadau wa Umeme.

  • Mwandishi alimuuliza hivi: Mh. Naibu katibu, ni madhara gani ambayo wananchi wameyapata tokea matatizo ya mgao wa umeme yaanze hapa nchini?
  • Naibu katibu mkuu: Sijapata malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi kuhusu madhara waliyoyapata kutokana na matatizo ya umeme. Na ujue ndg mwandishi nchi zetu za dunia ya tatu haziwezi kumaliza matati yote.

Ndg zangu hayo ndo yalikuwa majibu ya mdosi huyu. eti hajui madhara tunayoyapata na hajapokea malalamiko ya wananchi. kweli kazi ipo kwa serikali hii.

Nawasilisha wadau.
 
Hajui faida za umeme ndio maana! Angejua faida za umeme basi jibu lingekuwa ni rahis, angezigeuza tu yaan zikawa kinyume chake! Hivi huyo mtu kama hajui madhara wanayoyapata wananchi anawezaje kulisimamia kidete hili suala kwa maana ya kuondoa huu mgawo? Anasubiri tu mwisho wa mwezi aende kuchungulia kwenye ATM!
 
Huyu bwana ni KAIMU Katibu Mkuu sio NAIBU. Hajui lolote kuhusu siasa za umeme nchi hii. Jamaa alikuwa hazina kwa masuala ya bajeti.
 
serikali ya kukusanya kodi na kuziiba haiwezi kujua faida na hasara za umeme.
wakipewa suti pea tano wanakupa mpaka mahakama.
 
Yaani anasubiri mpaka wananchi wamlalamikie ndio ajue mgawo wa umeme una madhara kwao! Shame on him!
 
hawa ndo wale wanaojiita wamesoma nchi hii. mawazo yao ni kama makalio. 50yrs ya uhuru. Inaudhi sana.
 
Mkuu wa kaya alishasema kuw hajui chanzo cha umasikini wetu. Kwa mantiki hiyo ni vigumu tatizo la umeme kwisha.
 
Kuna msemo usemao aloshiba hamjali mwenye njaa! Vivyo hivo ifahamike kuwa madaraka hupofusha na pia hulevya.
Hivi ni nani anaepaswa kujua kero za wananchi wake, ni wajibu wa baba ndani ya familia kuhakikisha kuwa anahudumia familia yake ipasavyo na si kusubiri eti apelekewe malalamiko. Viongozi wetu wengi wao wa madaraka yamewalevya kwa kiwango cha kutotambua madhara wayapatayo wananchi..

Hivi ni kiongozi gani Tanzania hii asiejua madhara ya mgao wa umeme, mfano kushuka kwa uchumi kupanda kwa gharama za maisha, ukosefu wa ajira nk.. Labda kama kiongozi huyo ameamua kuziba masikio.

Nawomba kuwasilisha!
 
Hii ndiyo maana mgawo hataisha. Sasa kama kiongozi wa ngazi ya juu katika wizara hajui madhara ya mgawo tutegemee nini?
 
Huyu bwana ni KAIMU Katibu Mkuu sio NAIBU. Hajui lolote kuhusu siasa za umeme nchi hii. Jamaa alikuwa hazina kwa masuala ya bajeti.

Mh WildCard yeye kutoka hazina hakujustify kutoa majibu kama mwendawazimu. Hakuna sababu yeyote inayoweza kutolewa ikakidhi haja kuonesha kwamba alichojibu ni sahihi. Hakuna mtanzania mwenye akili timamu asiyejua madhara ya mgao wa umeme.
 
Huyo mh. amesema hajui madhara kwa sababu hajapata malamiko siyo kwa sababu majibu hayatakidhi haja, wewe siyo advocate wake. Na kwa sababu hajui madhara, anaingia katika kundi ulilolitaja hapo kwenye red.

Waandishi wa tz vihiyo kweli.hivi unaweza ukauliza swali la kijinga kama hilo kama kweli ni professional?.mbona yapo maswali mengi ya kuuliza watu hao?.ndio maana jamaa alimjibu kwa dhihaka namna hiyo.hata mkapa anawafaham kuwa ni makanjanja.
 
Tutajuaje sisi wasomaji/wasikilizaji kwamba, majibu ya naibu Katibu Mkuu huyo yalikuwa ya dhihaka? Binafsi sioni kama swali hilo lina tatizo. Maana ukiangalia, muuliza swali hakika alitaka tu kufahamu kwamba, Serikali pamoja na kusababisha kuwepo kwa janga la mgawo wa umeme, ilikuwa vyema pia kutambua sasa athari za janga hilo kwa umma. Maana kujua athari huleta msukumo wa kutafuta njia za kutatua kwa haraka tatizo husika. Aidha, swali hilo pia kwa upande mwingine linakuwa kama linakumbusha hatari ya nchi kuwa gizani pale ambapo madhara yanapowekwa hadharani. Ni sawa na swali walilowahi ulizwa wakuu wetu wa nchi na mashirika ya habari duniani kama BBC kuhusiana na sababu za nchi yetu kuwa masikini. Hivyo basi, sioni sababu kwa wewe kumponda muuliza swali. Maana ni kweli kwamba, wananchi tunatambua madhara ya mgawo wa umeme, lakini je, Serikali yetu inatambua kwa mapana gani? Hilo ni swali la msingi sana kuulizwa.
 
Na pengine serikali ingeenda mbali zaidi kwa kutoa tathmini ya madhara yaliyopatikana. Swali ni la msingi kabisa, naliunga mkono.
 
Huyu bwana ni KAIMU Katibu Mkuu sio NAIBU. Hajui lolote kuhusu siasa za umeme nchi hii. Jamaa alikuwa hazina kwa masuala ya bajeti.

Mkuu, hata muuza nyanya kule buguruni anajua kila kinachoendelea na madhara yake kuhusu umeme, then asijue huyo aliokuwa hazina akideal na masuala ya bajeti? Hawa jamaa wamelewa na wameshindwa ndo mana wanatoa majibu hayo. Kwa majibu haya it means huyu jamaa ni zuzu kuliko Jairo, hao wadau wa umeme katika hiyo mission hawakulalamika hapo? CTI hawakulalamika kweli juu ya umeme? kuna mtanzania kweli anayejua umeme ambaye halalamiki?
 
Waandishi wa tz vihiyo kweli.hivi unaweza ukauliza swali la kijinga kama hilo kama kweli ni professional?.mbona yapo maswali mengi ya kuuliza watu hao?.ndio maana jamaa alimjibu kwa dhihaka namna hiyo.hata mkapa anawafaham kuwa ni makanjanja.

Na wee kihiyo kwelikweli kama hujaona hata umuhimu swali hilo
 
naona alikuwa sahihi kujibu hivyo kwani;
  • kwake mgao haupo aidha stand by generator lipo lina full petrol 24 hrs
  • mara nyingi hawapo nchini wanakuwa nje ya nchi wakikimbia matatizo ya nchi hii likiwemo la umeme
  • hakuteuliwa kuwatumikia wananchi ila ilikuwa ni fadhira kwa jinsi alivyo participate kipindi cha kampeni
  • auje, asijue hakuna analoweza kulifikria au kulifanya ndiyo maana ameamua kutojishughulisha kupenda kujua watu anao waongoza wameadhilika kwa kiwango gani kutokana na mgawo mgumu huu usioisha
TUSHIRIKIANE KUMUOMBA MUNGU MVUA ZINYESHE HILI TATIZO LITAISHA
 
Jana nilisikitishwa na kauli ya Naibu katibu mkuu wa Wizara ya nishati na madini alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari ktk kongamano la wadau wa Umeme.

  • Mwandishi alimuuliza hivi: Mh. Naibu katibu, ni madhara gani ambayo wananchi wameyapata tokea matatizo ya mgao wa umeme yaanze hapa nchini?
  • Naibu katibu mkuu: Sijapata malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi kuhusu madhara waliyoyapata kutokana na matatizo ya umeme. Na ujue ndg mwandishi nchi zetu za dunia ya tatu haziwezi kumaliza matati yote.
Ndg zangu hayo ndo yalikuwa majibu ya mdosi huyu. eti hajui madhara tunayoyapata na hajapokea malalamiko ya wananchi. kweli kazi ipo kwa serikali hii.

Nawasilisha wadau.

That was a stupid answer to a stupid question.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom