Hii sasa ni kucheza na akili za Vijana wa Tanzania!

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Huu mpango wako Mkwere tumeushitukia. Tena sana tu.

Kwamba Mkwere umeona vijana wa Tanzania hatukitaki Chama chako cha matajiri na mafisadi, umeanza harakati za kutuhadaa kwa kuteua vijana kuwa wakuu wa wilaya (na tunategemea utafanya hivyo kwenye baraza la mawaziri).

Tunakupongeza kuwapa vijana nyadhifa. Lakini kwa nini sasa? Kwa nini hamukuwa mukifanya hivyo kabla? Hapa ni mimi tu muathirika wa umasikini wa Tanzania ninaweza kung'amua kuwa unatuhadaa.

Unataka 'kuwatumia' vijana kuwa wapiga debe wa chama chako cha mafisadi kujaribu kuturudisha kwenye kundi la walafi.

Mimi binafsi SITAKI. Mimi na Chadema tu.

Kwanza umeanza kutukatia umeme. Ili marafiki zako wapate dili za kuuza jenereta za Mchina. Majuzi tu ulijitapa kuwa "maji yapo tele, gesi ipo tele, makaa ya mawe yapo tele". Siku moja tu baada ya mbwembwe zako wakati wa kulihutubia Bunge, mgao ukaanza. Leo tunashindwa kuendesha biashara zetu kwa sababu ya mgao.

Hao vijana wako tunajua wametumwa na Chama chako cha mafisadi, kwa hiyo hatutawapa sapoti.

Ushindwe!!
 
ahsante sana mkuu tuna mwezi wa tatu sasa maji hatuyaoni, hatukumchagua ila anatutawala hawezi kutujali kamwe.
 
Kauli "tatizo la maji itakuwa historia" ilikuwa ni wimbo kila mahala alipopita kudunduliza kura. Tangu 31/10/2010 mtaani kwangu hakuna maji.
 
hahaaa Mkwere bana..eti kibinti cha maiak 25 anakipa UDC...halafu aanze kuwaita ngurdoto kwenye semina elekezi..JK bwana yaani huchoki kutupa vibweka
 
Huu mpango wako Mkwere tumeushitukia. Tena sana tu.

Kwamba Mkwere umeona vijana wa Tanzania hatukitaki Chama chako cha matajiri na mafisadi, umeanza harakati za kutuhadaa kwa kuteua vijana kuwa wakuu wa wilaya (na tunategemea utafanya hivyo kwenye baraza la mawaziri).

Tunakupongeza kuwapa vijana nyadhifa. Lakini kwa nini sasa? Kwa nini hamukuwa mukifanya hivyo kabla? Hapa ni mimi tu muathirika wa umasikini wa Tanzania ninaweza kung'amua kuwa unatuhadaa.

Unataka 'kuwatumia' vijana kuwa wapiga debe wa chama chako cha mafisadi kujaribu kuturudisha kwenye kundi la walafi.

Mimi binafsi SITAKI. Mimi na Chadema tu.

Kwanza umeanza kutukatia umeme. Ili marafiki zako wapate dili za kuuza jenereta za Mchina. Majuzi tu ulijitapa kuwa "maji yapo tele, gesi ipo tele, makaa ya mawe yapo tele". Siku moja tu baada ya mbwembwe zako wakati wa kulihutubia Bunge, mgao ukaanza. Leo tunashindwa kuendesha biashara zetu kwa sababu ya mgao.

Hao vijana wako tunajua wametumwa na Chama chako cha mafisadi, kwa hiyo hatutawapa sapoti.

Ushindwe!!

Subiri kwanza KIGOMA pawe DUBAI! si unakumbuka kwenye zile ahadi zake wakati wa kampeni? wewe unasema Umeme/Maji?:whoo:
 
Halafu vijana atakaowapa madaraka ni wa aina mbili tu: watoto wa kutoka familia za vigogo wa CCM, na watoto wa kike ambao hutumika kama nyumba ndogo. Wote ni henchmen wake wasiokuwa na uwezo wa kupinga au kukosoa jambo lolote baya litakaloamuliwa au kutekelezwa na serikali.
 
ni vizuri anawapa vijana maana mwisho wa siku vijana wooote watahamia chadema na watamkimbia hatoamini macho yake
 
wakuu naomba taarifa hizi za uteuzi wa vijana ziambatane na udhibitisho!
 
Back
Top Bottom