Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,173
Huu mpango wako Mkwere tumeushitukia. Tena sana tu.
Kwamba Mkwere umeona vijana wa Tanzania hatukitaki Chama chako cha matajiri na mafisadi, umeanza harakati za kutuhadaa kwa kuteua vijana kuwa wakuu wa wilaya (na tunategemea utafanya hivyo kwenye baraza la mawaziri).
Tunakupongeza kuwapa vijana nyadhifa. Lakini kwa nini sasa? Kwa nini hamukuwa mukifanya hivyo kabla? Hapa ni mimi tu muathirika wa umasikini wa Tanzania ninaweza kung'amua kuwa unatuhadaa.
Unataka 'kuwatumia' vijana kuwa wapiga debe wa chama chako cha mafisadi kujaribu kuturudisha kwenye kundi la walafi.
Mimi binafsi SITAKI. Mimi na Chadema tu.
Kwanza umeanza kutukatia umeme. Ili marafiki zako wapate dili za kuuza jenereta za Mchina. Majuzi tu ulijitapa kuwa "maji yapo tele, gesi ipo tele, makaa ya mawe yapo tele". Siku moja tu baada ya mbwembwe zako wakati wa kulihutubia Bunge, mgao ukaanza. Leo tunashindwa kuendesha biashara zetu kwa sababu ya mgao.
Hao vijana wako tunajua wametumwa na Chama chako cha mafisadi, kwa hiyo hatutawapa sapoti.
Ushindwe!!