Hii Sasa Balaa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii Sasa Balaa!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amanikwenu, Jan 13, 2010.

 1. A

  Amanikwenu Senior Member

  #1
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Jana nilitembelewa na jirani yangu mmoja na akanieleza kuwa watoto wake wawili wamefaulu mtihani wa darasa la saba na wamechaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya Zinga iliyoko wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani. Hii ni moja ya shule zetu za kata.
  Kitu kilichonistua na kunishangaza katika maelezo yake ni kuwa, pamoja na mambo mengine kama hela ya mlinzi; uji; kuni; ada; karatasi, kila Mwanafunzi anatakiwa AENDE NA KITI NA MEZA YAKE SIKU YA KUFUNGUA SHULE TAREHE 18/01/2010.
  Je huu ni utaratibu wa nchi zima kwa shule zetu za kata au ni kwa shule hii ya ZINGA pekee?
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hali ndio hiyo kwa Tanzania nzima tena hata kwenye Private Schools zenye majina. Nilidhani ni wakati mzuri sasa serikali ikaunda chombo kinachofanana na EWURA/SUMATRA/TCRA kwenye elimu pia. Vinginevyo iipe meno TEA ifanye kazi hiyo.
  Kuna ndugu yangu mmoja kampeleka mwanae BAOBAB. Kwenye Invoice yao ya karo upo mchango wa laki moja ya jengo! Yaani mzazi achangie kumjengea mmiliki binafsi.
  Nikamshauri akishachangia aombe shares ili naye awe na umiliki wa kiwango fulani. Karo ya BAOBAB mbali na mchango huo ni milioni mbili na nusu (2,500.000/=) kwa mwaka wa kwanza.
   
 3. M

  MalaikaMweupe Member

  #3
  Jan 13, 2010
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ufisadi umeshamiri kila sekta,lakini sikutegemea sekta binafsi! Wakati umefika wa watu kufichua maovu haya,kama unaona ni kitu cha ajabu na usipokikemea au kukisema watu wakasikia,basi hali hii itaendelea milele! Shule binafsi nyingi wanafanya mambo ya ajabu,lakini wazazi na walezi hawasemi,sijui ni kwanini. Niliwahi kusikia mzazi mmoja anasema alihudhuria mkutano wa wazazi katika shule moja,na alishangaa kuona wazazi wanashauri ada ipandishwe! akaona aubu kupinga.
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mzee kwenye bold hapo umeongea point hata mimi niliwaza the same, ila swali ni moja tu unawajua wenye hizo shule???
   
 5. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Binafsi utaratibu wa kuchangishana katika fixed assets unabidi uangaliwe upya. Maana kama mtu unasaidia katika cost halafu huwezi realise profit huo ni WIZI. Siwezi kuchangia huduma ninayopata halafu tena nachangia na running cost ya service provider.

  Michango ya kanisani, mashuleni, mtaani, yote ni wizi mtupu!

  Michango ya makanisani mbali na sadaka ninamaanisha michango ya kusaidia ujenzi wa shule, mabenchi nk.

  Kama mtu amejiita local investor halafu anatumia pesa za watu, huo ni WIZI! MWIZI MKUBWA!
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  ....the show continues!!!!
  Ma-ghembe hebu baelezee bananji hii mradi ya mendeleo kwa mishule yetu ni ya nini tena vile? SEDP na PEDP,

  haya, kama huna jibu nenda kachume fimbo uje nayo hapa sasa hivi!!
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tukitaka kuwafahamu ni rahisi tu. Yupo anayewapa usajili pale wizarani. Lililo wazi ni kwamba WANASIASA wetu wengi sana wamewekeza kwenye miradi hii ya shule. Ndio maana wanafanya wanavyotaka. Wengine kwenye uwekezaji huu wa mashule ni watumishi waandamizi serikalini. Kazi ipo. Hili hata kulipeleka BUNGENI ni kazi bure. Wabunge wengi wetu wanamililki au ni wawekezaji humo. Tufanyeje? Elimu bora inatolewa huko sasa hivi. Primary na Secondary za serikali zinahujumiwa kwelikweli. Walimu wazuri waliosoma kwa gharama zetu wanakimbilia huko.
   
 8. A

  Amanikwenu Senior Member

  #8
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WildCard,

  Nakuunga sana mkono kwenye hili la kuwa na Tanzania Education Regulatory Authority (TERA). Ila bado tatizo langu linabaki palepale. Hivi kweli tumeshindwa kununua madawati ya kutosha kwa ajili ya shule zetu za sekondari za kata wakati bajeti ya sekta ya elimu kwa mwaka huu wa fedha ni zaidi ya shilingi bilioni 1,743. Kama tumeshindwa madawati je vitabu tutaweza? Aliye na breakdown ya bajeti ya elimu naomba atusaidie katika hili.
  Pia ni muhimu sana Waziri muhusika akatoa kauli ya serikali kuhusu wanafunzi wa shule zetu za kata kutakiwa kwenda na kiti na meza shuleni wanaopoanza kidato cha kwanza.
   
 9. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 771
  Trophy Points: 280
  Na bado kuna siku titaambiwa inabidi tuingie kwa wallet kuwalipa walimu!

  YOU CANT TAX UNTAXABLE SOCIETY
   
 10. O

  Omumura JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yapo malalamiko mengi ya jinsi usajili wa kulipua unavyofanyika pale wizarani.Kwamfano, kule tanga kuna chuo fulani cha ualimu kisicho na kiwango kimelalamikiwa sana na wananchi lakini mkubwa wa wizara kwakuwa ni kabila moja na mwenye chuo hakijafungwa na mambo yanaendelee, ndo elimu ya bongo hiyo!
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Jan 13, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hii ndio serikali ya tanzania bwana.Mambo yote mtelezo
   
 12. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160

  Hii ndiyo sera safi ya CCM kwamba kila kata lazima kuwe na sekondary ifikapo 2010 na haya ndiyo matunda yake.

  Shule za kata za style kama Zinga zipo nyingi sana.
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mbona hicho chomo kipo wanaitwa Wakaguzi wa Elimu hata hapo wizarani kitengo hicho kipo na kina bajeti yake tatizo linabaki palepale mambo yanaendeshwa kisiasa zaidi.

  Hizi shule za kata zinaruhusiwa kuanza siku waziri anapotembelea kuweka jiwe la msingi bila kujua itaisha lini kujengwa walimu watapatikana wapi madawati na kadhalika. Shule nyingi hasa hizi za kata zilianzishwa haraka haraka ili kuwafurahisha wadhamini Tanzania ionekane imepiga hatua katika elimu matokeo yake ndo kuleta walimu wa Voda fasta umemaliza form two yako unapelekwa kozi ya ualimu mwezi mmoja next month ni mwl. haijalishi kama ulichelewa kwenda chuo kwa wiki mbili twende tu nasikia kuna wengine walikuwa wanawakuta wenzao wiki ya mwisho wanaagwa na kujiunga nao.

  Hii ndio elimu ya Tz iko kisiasa zaidi matokeo yake shule inakuwa na walimu wawili tu tena hawajui hata ethics za ualimu.
   
 14. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Siyo serikali bali sema hii ndio hulka ya watanzania. Hizi shule binafsi walianza vizuri tena serikali ikawapa nafuu ya kodi lakini SUSTAINABILITY inawashinda.

  Hata hizo 'Academy' zenye majina makubwa kumbe ilikuwa nguvu ya soda, hawalipi wafanyakazi wao vizuri kama ambavyo ungetegemea kwenye private sector; tangia ajira za walimu zilipopatikana serikalini, nyingi ya shule hizi siku hizi ni dhofulhali!
   
 15. kui

  kui JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 6,478
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
  LOL!....ar u for real? kiti na meza tena, litakuwa darasa au warehouse kila mtu akenda na furniture zake?
   
 16. Glucky

  Glucky Senior Member

  #16
  Jan 14, 2010
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  in such kind of situation other peoples are building houses of 1.2 billion and their kids are in up countries. is there any equality.
   
 17. American lady

  American lady Member

  #17
  Jan 14, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mola tusaide ss wanyonge shule tunapenda ila uwezo wetu
   
 18. M

  Mndamba Member

  #18
  Jan 14, 2010
  Joined: Jun 22, 2007
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Big "NO" Mwanangwa. Wanasema hata vidole hutofautiana urefu japo vyote ni vidole. Katika mazingira kama haya kuna umuhimu wa mabadiliko.
   
 19. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Shule za serikali kweli huu utaratibu uangaliwe upya.

  Kwa shule binafsi sioni tatizo la kupanga bei yoyote wanayotaka kama soko lipo, ndo biashara inavyoenda. Pale IST ni kama $13,000 na watu bado wanalipa.
   
 20. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Ni kweli tunahitaji regulator kwenye hii biashara ya shule. Wamiliki wanadai hela kwa nguvu tena sio hiari .Eti mtoto atarudishwa shule kama hajalipa mchango wa majengo. Hata wamiliki wangekuwa marais wote wastaaf na J.K juu, hawana haki juu ya haya.

  Tunahitaji mtu kama Dokta Magufuli. Period
   
Loading...