Hii picha nimeipenda sbb inanikumbusha mbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii picha nimeipenda sbb inanikumbusha mbali

Discussion in 'Jamii Photos' started by cheusimangala, Apr 12, 2010.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  Weee sema chochote upendacho kuhusu hii picha lkn mie imenikumbusha mbali sana back to 80's wakati niko mtoto, hasa wakati wa xmas mama yetu alikuwa ananunua kitambaa cha aina moja wote kuanzia dada zangu hadi mimi tunashonewa kitambaa hicho hicho hadi mshono mmoja.

  Viatu mnanunuliwa vikubwa kidogo eti ili ukuwe navyo mbele unajazia na karatasi ili vitoshe.
  mkishakula pilau na double cola mnapewa hela muende mjini mkatembee,basi nilikuwa najiona nimependezaa,usoni mmepakwa mafuta ya rays mnang'aa kama kioo.

  Mkienda kutembea mjini mtu unatembea kama kiwete maana viatu vinaumiza..aah nafurahi kuwa mtu mzima maana leo hii nisivyopenda nguo za kushona.leo nikiamua kuvaa leging na skin jeans hakuna wakunichagulia.

  Utu uzima raha jamani.
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  mshukuru pia mama yako kwa kukupeleka shule!!

  Picha safi sana hii love ya mama bana....anamtanguliza mtoto mbele,
  wamjini wanawaacha watoto nyuma!!
   
 3. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  halafu mama na mtoto wanaonekana wana amani mpaka basi yaani! lol!
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Nimekubali mama kumbe kwa umri tunakaribiana, nilifikiri we wa juzi tu!
   
 5. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mi mkongwe bwana usiniangushe mi sio wa juzi.
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Sawasawa mama!
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ila raba mtoni zimekukaa mama! Na huo mguu, acha tu!
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Cheusi huo mguu umemzingua Babuyao, hajui kuwa WANYALUKOLO ndio matende yao yalivyo!!
   
 9. father-xmas

  father-xmas JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kwa body ya huyo mama.....huo mguu umejazia vyakutosha kabisa....ukizidi yatakuwa matende...!
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Those days were days bana, sikukuu ilikuwa kweli sikukuu sare nyumba nzima, jioni mnaenda kutembea somewhere. kwa jirani km wana nguo mpya nyie hamna daaaaaaaaaaaaah sikukuu inakuwa mbaya mnooooo
   
 11. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Such a lovely pic !!! with green n enrich soil !!! It's remind me a lots on those days !! thanx cheusi !
   
 12. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  hahaa we acha tu xmas moja fundi alifanikiwa kushona nguo za ndugu zangu wote lkn yangu akachelewa hivyo nikaambiwa nitaivaa tar 26 instead kwa hiyo nivae ya xmas iliyopita!nililia siku hiyo yaani!hahaa kazi kwelikweli!
   
 13. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  wa mjini malezi ya bata .... anajua kutotoa tu wala hajui kulea kijijini malezi ya kuku... wa huku mjini ukiwauliza anakwambia bwana eee nilikuwa kwenye starehe zangu ndio ukapatikakana wewe wala sikupanga
   
 14. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  eheeeee umenikumbusha mabli mno... enzi hizo kipindi cha x mas na mwaka mpya nikiona maza karudi na box tu basi na jua ndani kuna MOKA na sis nae ana SKUNA zake... pia najua kuna mashati ya ndege na suruali za mchelemchele na zina mikanda ya kama mpira ina pad ya treni.... hahhhhhhh tumetoka mbaliiiii..... siku hiyo unatembea kama unanyata... hukai ovyo na wala hushiki chochote ovyo..... ila mkirudi tu nguo unaishia kuziona kwenye kabati mpaka upatikane mtoko... baada ya sikukuu kama mbili tatu ndio zinakuja mpya zingine..
   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  People...kuna kitu hapa....Jana mwanaJF fulani alitoa picha fulani ya members wawili wakiwa wadogo, na walikuwa eneo hilihili...Je hamuongezi 1 na 1 mkapata 8?

  [​IMG]


  linganisha na hii hapa chini!

  [​IMG]
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Cheusimangala umetoa wapi picha yangu lakini???:):D
  Mod naomba uitoe kwenye web yako nisijepata matatizo ya kifamilia
   
 17. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  jamani fl1 si uliniruhusu mwenyewe niichukue kwenye ile albam yako!lol
   
 18. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nasikia eti hao mabrazamen hapo juu ni chrispin na kaizer enzi zao zakutesa!
   
 19. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  umenichekesha!unakumbuka mashati ya ujiuji?kazi kweli.
   
 20. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Cheu...kumbe nawe umekula chumvi kidogo!!!!
   
Loading...