Hii picha ilipigwa mwaka 1843 na wamissionari wa Kiingereza walipofika Magila, Muheza

1844 tulikuwa tunatoa wapi nguo.
Jamii chache zilijua kuvuma nguo, lakini wa jumla nguo ziliagizwa kutoka nje. Biashara ya misafara kutoka pwani kwenda bara ilipeleka idadi kubwa za nguo katika maeneo yote yaliyokuwa karibu na njia za misafara. Bidhaa kuu zilizoingizwa zilikuwa nguo, waya, lule za kioo, pamoja na bunduki, baruti (na pombe kali kidogo kwa machifu). Msafara uliweza kuwa na wapagazi 1000 hadi 2000.

Njia kuu za misafara zilikuwa 1) bonde la Pagani kwenye kaskazini kuelekea ziwani Viktoria, 2) Bagamoyo / Saadani kwenda Tabora - Ujiji, 3) Kilwa kufuata Rovuma hadi Ziwa Nyasa.
Viwanda vya nguo huko Uhindi, Marekani na Ulaya vilizalisha kwa ajili ya soko la Afrika. Ilhali hawakuwa na pesa, futi kadhaa za kitambaa zilikuwa bei ya kununulia pembde za ndovu na watumwa, waliorudishwa tena pwani.

Kwa hiyo nguo zilipatikana tu, angalau karibu na njia za misafara.
 
1843!!kulikuwa na watu!!Miaka 178!iliyopita!!
Kwahiyo miaka 100 ijayo hata watoto wangu wenye miaka 17 hawatakuwepo!!
This is very mind troubling!?!
Dunia kweli tunapita!?!
Na siajabu kunawa na taxi za helicopter, Mbezi Mbagala dakika 10
 
Hakika Mkwawa hakuandika barua. Hakuwa msomi. Tena hakushirikiana na watemi wengine.
Kinyume chake, alijenga milki yake kwa kushambulia majirani. Mwaka 1888 (mwaka wa vita ya Abushiri), Mkwawa alishambulia tena Wasangu na kupora Wakonde.
Mwaka 1890 alijaribu kuwasiliana na Wajerumani waliowahi kuendelea bara, baada ya kushinda Abushiri na Bwana Heri kwenye pwani mwaka 1889.
Maswasiliamo yalishidikana.
Mwaka 1891 kamanda Mjerumani Zelewski aliamua kushambulia Wahehe akashindwa huko Lugalo.
Wakati wa mapigano ya Mkwawa dhidi ya Wajeumani, Abushiri hakuishi tena na Bwana Heri alipatana nao.
Unabishabisha kijinga tu,mkwawa aliandika kwa kiswahili akitumia maandishi ya kiarabu,hiyo picha maarufu ya mkwawa kavaa kanzu na kilemba(kiremba) unadhani alivipataje!?
 
Johann Krapf, Mjerumani, alianzisha Anglican Church, kanisa la Ufalme wa Uingereza?
Alikuwa Mjerumani na Mlutheri, lakini alitumwa Afrika na Shirika la misioni ya Kianglikana CMS. Wakati wake walikuwapo ambao hawakusisitiza udhehebu kuliko yale waliyoona kama "kujenga ufalme wa kristo".

Johann Ludwig Krapf (11 Januari 181026 Novemba 1881) alikuwa mmisionari wa kwanza wa Uprotestanti nchini Kenya katika karne ya 19 akatunga kamusi ya kwanza ya lugha ya Kiswahili.
...

Ethiopia 1837-1842​

Mwaka 1836 alikutana na mwakilishi wa Church Missionary Society (CMS) aliyemkaribisha kufanya kazi na CMS. Misioni ya Basel ilimpa ruhsa akapokea wito wa kwenda Ethiopia. Krapf alianza mara moja kujiandaa akisoma Ge’ez (lugha ya Kale ya Ethiopia) na Kiamhari (lugha ya kisasa ya Wakristo katika nyanda za juu Ethiopia).

1837-1842 Krapf alifanya kazi ya umisionari huko Ethiopia. Mpango wa misioni ya CMS ilikuwa kuwaamsha Wakristo Waorthodoksi kwa matumaini ya kwamba watakuwa wenyewe wamisionari bora kwa wenzao Wapagani au Waislamu.

Lakini Krapf hakuelewa vema Ukristo wa kiorthodoksi wa Waamhari. Alishindwa kuelewa maana ya liturgia, mila na desturi nyingi. Hakuelewa hasa kwa nini Wakristo Waorthodoksi walisoma Biblia katika lugha ya kale ya Ge’ez hata wasipoelewa lugha hiyo badala ya kutumia tafsiri ya Kiamahari aliyokuwa amefanya.

Hivyo Krapf alijisikia amevutwa zaidi na Wagalla – hili ni jina la zamani za watu wanaojulikana leo kama Waoromo au Borana. Wagalla kwa jumla walikuwa wakifuata dini zao za kiasili, athira za kiislamu zikianza kuonekana. Krapf alijifunza lugha yao alianza kutafsiri sehemu za Agano Jipya katika Kigalla (Kioromo).

Mwaka 1842 Krapf alipaswa kuondoka Ethiopia pamoja na wamisionari wengine wa Kiprotestanti, akiwa na ndoto ya kurudi na kufanya kazi kati ya Wagalla. Alikaa muda kidogo Kairo (Misri) akafunga ndoa, bibiarusi alikuwa amemfuata kutoka Ujerumani.

Wakati ule kwake nyumbani Tübingen Chuo Kikuu kilikuwa kimefuata taarifa zake na 1842 kikampa cheo cha udaktari (PhD) kwa ajili ya utafiti wake katika lugha na historia ya Ethiopia.


Afrika ya Mashariki 1844-1853​

Ethiopia ilikuwa imefunga milango yake, hivyo Krapf aliwaza njia nyingine. Alikuwa amesikia ya kuwa Wagalla waliwahi kufika hadi pwani za Afrika ya Mashariki. Hivyo akasafiri hadi Zanzibar kwa lengo la kuwafikia Wagalla kupitia eneo la Kenya ya leo. Sultani Seyyed Said alimpa ruhusa ya kuanzisha kituo cha misheni huko Mombasa.

Mwaka 1844 Krapf alifika Mombasa akianza mara moja kujifunza Kiswahili pamoja na lugha ya wazalendo wa eneo la Mijikenda. Huko mke na mtoto waliugua malaria wakafa. Krapf alihamia Rabai iliyoko katika vilima juu ya Mombasa penye joto kidogo akaanzisha kituo cha Rabai Mpya.

Mwaka 1846 mmisionari mwingine (Johannes Rebmann) alikuja kufanya kazi pamoja naye. Huko Rabai Mpya Krapf alitunga kamusi na sarufi ya kwanza ya Kiswahili.

Krapf na Rebmann walikuwa Wazungu wa kwanza walioona milima yenye theluji Afrika. Rebmann aliona Kilimanjaro, Krapf aliona Mlima wa Kenya. Taarifa zao zilipofika Ulaya zilichekwa na wataalamu waliodai milima yenye theluji haiwezekani Afrika.

Krapf aliendelea kuwa na matatizo ya afya akarudi Ujerumani mwaka 1853.


Urithi wake​

Hadi kifo chake aliendelea kuboresha vitabu vyake kuhusu utamaduni na lugha za mataifa mbalimbali ya Afrika. Kwa jumla aliandika kamusi au kutafsiri sehemu za Biblia katika lugha zifuatazo: Ge’ez, Kiamhari, Kioromo, Kiswahili, Ki-mijikenda, Kikamba, Kimasai.

Ludwig Krapf alitoa mchango mkubwa sana katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili kwani aliweza kutafsiri Injili ya Luka na ya Mathayo ,pia aliweza kuandika sarufi ya Kiswahili inayohusu jamii ya Wasambaa.

Nyumba yake huko New Rabai imekuwa makumbusho chini ya Museums of Kenya. Jengo la Ubalozi wa Kijerumani huko Nairobi limepewa jina lake.

Krapf alikuwa Mlutheri, lakini Kanisa Anglikana linamkumbuka kama mwanzilishi wa madhehebu yake nchini Kenya.
(soma yote: Ludwig Krapf - Wikipedia, kamusi elezo huru )
 
Unabishabisha kijinga tu,mkwawa aliandika kwa kiswahili akitumia maandishi ya kiarabu,hiyo picha maarufu ya mkwawa kavaa kanzu na kilemba(kiremba) unadhani alivipataje!?
Kumbe kanzu inaandika? Kaka nilikuomba mara kadhaa lete ushahidi kwamba kuna barua za Mkwawa. Bila shaka zimejadiliwa tayari na wataalamu mbalimbali, kama zipo. na nimeshakuambia, hakika hakuweza kuwaandikia barua watu kama Abushiri (aliyekufa tayari) au Bwana Heri (aliyehamia upande wa maadui).
 
Kumbe kanzu inaandika? Kaka nilikuomba mara kadhaa lete ushahidi kwamba kuna barua za Mkwawa. Bila shaka zimejadiliwa tayari na wataalamu mbalimbali, kama zipo. na nimeshakuambia, hakika hakuweza kuwaandikia barua watu kama Abushiri (aliyekufa tayari) au Bwana Heri (aliyehamia upande wa maadui).
Nimekwambia barua za mkwawa zipo kwenye makumbusho ya mkwawa iringa,unataka niende iringa nikupigie picha niweke humu!!?
 
Asante kwa historia, nilishafika mara kadhaa magila, na kuna kanisa la Anglican na Shule pia ambayo ipo chini ya kanisa.
 
Back
Top Bottom