Hii nyumba ilijengwa mwaka 1509 katika kijiji cha Argentan, Ufaransa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,270
1635729843241.png
 
Kinachofanyika hapo inakarabatiwa na inapigwa rangi mpya lakini iliyochanywa kitaalam ionekane ni rangi ya zamani.

Ni kama mnavyocheza filamu ionekane ya zamani lakini imetengezwa mwaka huu.

Nadhani UNESCO wanahusika hapo.
Maisha ya vigae ni guarantee miaka 100, vigae vya awali vita jua vimebadishwa.
 
Kinachofanyika ni kutunza shape na uhalisia.

Aliyekwenda london miaka 60 iliyopita ukimpeleka london leo wala hapotei na hakuna majengo mapya mapya.
Ila aliyetoka Dar miaka 60 iliyopita ukimleta leo Dar inabidi umuongoze

Mfano pale stone town Zanzibar yale majengo yanahitaji ukarabati bila kubadili muonekano na uhalisia wake.
 
Kifupi kwa wasio elewa. Nyumba hiyo ina miaka 512 mpaka sasa

Ukisoma afrocentric wanadai eti miaka fulani afrika ilikuwa almost the same na huko europe kimaeneleo ilhali ukimulika kiundani watu walikuwa hawana hata vyoo vya kujisaidia.
Mohamed Said
Ndicho alicokiandika Walter Rodney kwenye Howa Europe Underdeveloped africa,: zamani nilikuwa naamini lakini nilipokua na kikomaa nikaona hizi nin0ropaganda tu!

Kama Leo tunasaidi2a kujenga mayundu ya choo!

Tunatembelea Mavi Eight ' ilhali Hali iuna watu wanakunywa maji kwa ushirikaa na nyani nna mbuzi

Kunawatoto wana6embea Km 5+ kuifuataa shule!

Haya ni matusi kwa wazungu!
 
Ustaarabu mkubwa wa Ulaya ulienezwa na dola ya Roma. Uajemi ni wajenzi wa asili na tangu BC walikua na majengo bora na visima vya kuchota na kamba.

Spain na Ureno walipata maendeleo ya Ugiriki ndani ya Roma. Morocco na Algeria walifaidika kutokana na wahamiaji kutoka Uajemi pamoja na ukaribu wao na Ugiriki pamoja na Uturuki.

Hata Senegal na Mali kuliko endelea tangu enzi za Mansah Musa walitumia udongo kujenga lakini majengo ambayo hayakuharibiwa na Wakoloni bado yapo.
 
Kinachofanyika ni kutunza shape na uhalisia.

Aliyekwenda london miaka 60 iliyopita ukimpeleka london leo wala hapotei na hakuna majengo mapya mapya.
Ila aliyetoka Dar miaka 60 iliyopita ukimleta leo Dar inabidi umuongoze

Mfano pale stone town Zanzibar yale majengo yanahitaji ukarabati bila kubadili muonekano na uhalisia wake.
Haya majengo ya mbao Uingereza waliyabomoa mengi baada ya moto wa London Sunday 2, September 1666.
 
Kifupi kwa wasio elewa. Nyumba hiyo ina miaka 512 mpaka sasa

Ukisoma afrocentric wanadai eti miaka fulani afrika ilikuwa almost the same na huko europe kimaeneleo ilhali ukimulika kiundani watu walikuwa hawana hata vyoo vya kujisaidia.
Mohamed Said
Kilwa mji wa Kale mfano wake kulikuwa na majengo yenye vyoo na yamekuja kuvunjwa na Mreno kwa mizinga hadi leo magofu yake yana sehemu ya choo.

Timbuktu kulikuwa na maendeleo makubwa karne ya 11 hata kabla ya hiyo Nyumba haijajengwa. Watu walimiliki vyoo, na majengo ya kila namna. Hadi kulikuwa na chuo kikuu Timbuktu.

Afrika ya magharibi kulikuwa na kiwanda kikubwa cha nguo chenye nguvu kuliko cha Manchester England.

Waliyosema Afrika ilikuwa sawa hawakusosea ni kweli, ila mambo yalibadilika kuanzia karne ya 15 walipoanza kumiminika wageni kutoka mataifa mbalimbali. Hao ndiyo waliharibu kila kitu na hata kuvunja majengo mengine ya kale. Ndiyo maana vitu vingine ushahidi hakuna kwasababu waliharibu kusudi. Mfano Kilwa kuvunjwa dola iliyoendelea hadi kumiliki sarafu yake, hivi sasa ni magofu tu
 
Nakubaliana na wewe kiasi fulani ila si sawa kusema eti tulikaribiana nao kimaendeleo au kiustaarabu. Tulikuwa wapi mpaka waje kuvamia na kuvunja dola zilizokuwa imara na zenye maendeleo unayoyasema?
 
mm nadhani mababu zetu hawakuwa na uelewa wa kutosha
 
Sasa huwezi kujiita umeendelea kiasi cha ku compete na wenzako wakati huna uelewa wa kutosha kifupi gepu lilikuwa kubwa mno na pengine hatukuwahi kulingana nao hata nukta moja.
kabisa ila ufahamu/uelewa ndo mzizi mkubwa wa maendeleo kama hakuna hicho basi panakuwa debe tu
 
Upo sahihi kabisa
 
Nakubaliana na wewe kiasi fulani ila si sawa kusema eti tulikaribiana nao kimaendeleo au kiustaarabu. Tulikuwa wapi mpaka waje kuvamia na kuvunja dola zilizokuwa imara na zenye maendeleo unayoyasema?
Kama wakina socrate na plato na wasomi wengi wakale waulaya wanaotajwa waasisi wa civilization
walikuja kijfunza afrika na wazungu wanakili kwanin isiwezekane kuwa nao sawa kimaendeleo.
Afrika imepotea baada ya kuvamiwa na alexander the great na warumi wakaja kuizika kabisa.
 
Back
Top Bottom