Hii njia ni sahihi kujua ukubwa wa eneo kwa heka?

Suala la ramani linahitaji uende kwa mpima ardhi, yeye ndo atakuandalia.

SUKAH
Duh, mpima ardhi anadai kuandaa hiyo ranani nimpe 150,000/ sina hiyo pesa kama kuna njia nyingine naomba nishauri..... siwezi kutumia ms. Word kuandaa ramani???
 
Nilienda halmashauri nikaambiwa na savea....hiko kidude kukodi ni sh 100,000 kwa siku..... gharama za kuandaa ramani na kuprint 200,000 na gharama za mtaalm sh 150, 000/ jumla ya gharama kwa kaz yote 460, 000/= hapo usafiri juu yangu. Nikaondika sijarudi tena hadi leo
Duuhh !!! Sijawai kulipa hizo gharama.
 
Duh, mpima ardhi anadai kuandaa hiyo ranani nimpe 150,000/ sina hiyo pesa kama kuna njia nyingine naomba nishauri..... siwezi kutumia ms. Word kuandaa ramani???
Ms word! Hapana mkuu. Hayo ni mambo ya kitaalamu, ongea vizuri na mpima akufanyie wepesi kidogo.
Hapa itahusika arcGIS au autoCAD.
Hii ni baada ya kutembelea eneo lako na kuchukua coordinates za mipaka ya kiwanja chako.

SUKAH
 
Shukran sana mpima, tupo pamoja.

Hivi vipimo vya heka kuwa 4900 huwa vimekadiriwa katika vipimo vya yard² na sio m², ambapo hatua 1 ya mtu mzima hukadiriwa kuwa sawa na 1 yard.

Kwa hiyo heka 1 hukadiriwa kuwa hatua 70×70 ambayo ni sawa na 4900 yard².

Sasa watu wengine huchukua tape measure na kupima mita 70x70 badala ya yards, hapo sasa ndo makosa yanapoanza kuibuka.

SUKAH
Kwa kweli hiyo elaboration yako imeingia katikati ya ubongo wangu
Asante ndugu
 
Nilienda halmashauri nikaambiwa na savea....hiko kidude kukodi ni sh 100,000 kwa siku..... gharama za kuandaa ramani na kuprint 200,000 na gharama za mtaalm sh 150, 000/ jumla ya gharama kwa kaz yote 460, 000/= hapo usafiri juu yangu. Nikaondika sijarudi tena hadi leo

Kwa site recconaisance tu na data check hata kwa dar es salaam huwa hawafanyi kwa dau kubwa namna hiyo. Try hizo other options kama utashindwa nipe location yako Pm ntakusaidia mtu wa karibu na ulipo akupatie sapoti juu ya suala lako
 
Duh, mpima ardhi anadai kuandaa hiyo ranani nimpe 150,000/ sina hiyo pesa kama kuna njia nyingine naomba nishauri..... siwezi kutumia ms. Word kuandaa ramani???

hapana mkuu, kuna softwares huwa tunatumia kuandaa hizo ramani nazo ni civil autocad 2003 au 2009
 
Ili kupata ukubwa wa eneo Kwa uhakika ni kutumia GPS upate Coordinates ambazo zitaingizwa kwenye software za kucholea ramani kama QGIS,arcGIS au nyingine hapo utapata chochote unachohitaji mfano ukubwa wa eneo, muinuko,slope, contour na vingine vingi kadri ya mahitaji yako.

Mfano hiyo ramani mtu alituma coordinates tu akitokea shambani kwake na ramani kama hiyo inaandaliwa.


Michael Madumba Farmt~3.png
 
Raha ya kumiliki ardhi uwe hata na karamani uchwara tu 😀😀😀

Mtu anitumie coordinates ni mchoree ramani ya eneo lake Bure leo Leo.

Application ya kuchukua coordinates apakue Play Store inaitwa My GPS location angalau apate coordinates kwenye Kila kona.

Screenshot_20230611-120905.png
 
Nilienda halmashauri nikaambiwa na savea....hiko kidude kukodi ni sh 100,000 kwa siku..... gharama za kuandaa ramani na kuprint 200,000 na gharama za mtaalm sh 150, 000/ jumla ya gharama kwa kaz yote 460, 000/= hapo usafiri juu yangu. Nikaondika sijarudi tena hadi leDa
Ramani ulifanikisha Mkuu?
 
Huwezi pata ukubwa wa eneo utaenda chaka vibaya mno.

Lets say ekari ni 70 kwa 70 meters mzingo 70+70+70+70=280
A=70×70=4900
Oky tupunguze meters 35 za upande mmoja tuongeze kwenye upande mwingine iwe 105 kwa 35 mzingo 105+105+35+35=280
A=105×35=3675
Unaona sasa maeneo mawili yenye mzingo sawa but ukubwa wa eneo unatofautiana

Chakufanya hilo eneo mlipime kwa kulikata vipande vipande
Kateni eneo kubwa la mraba, kisha vipande vinavyobakia hata kama ni pembe tatu pimeni hivyo hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini hapo kwenye 4900m square sio sahihi kuwa ni kipimo cha ekali
Kwa ufasaha kabisa kipimo cha ekali ni mita za mraba 4000 na ndio maana huwa tunasema hekta moja ni sawa na 2.5 ekali, na hekta moja ni sawa na mita za mraba 10,000
 
Back
Top Bottom